IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

Polisi kuna shida ya nidhamu. Utomvu wa nidhamu kwa askari wadogo kama mauaji kule Mtwara ni kielelezo cha hali halisi huko juu. Hili la Wankyo ni tukio la aibu mno kijeshi!

Ni dhamira ya kutaka madaraka ya mkuu wa jeshi la Polisi! Hii case inaweza kumuweka pabaya mno huyu RPC.

Nafikiri toka Sirro alalamike kuwa wapo makamanda waliona wao walifaa kuliko yeye na hili la juzi, ni muhimu hili Jeshi litazamwe upya kurudisha nidhamu. Ni jeshi muhimu mno na kilelezo cha ulinzi wa Taifa lolote!

Hapa tupa kule unampenda Sirro au humpendi, Jeshi lina mipaka yake ya nidhamu. Ni hatari mtu wa cheo kile kuongea vile hadharani! Kesho akisema anatamani Urais? Hatari! Hatari! Hatari!

Mungu ibariki Tanzania [emoji1241]
 
Kwa jinsi ulivyo na ulivoandika hufai kuwa staff wa jf umedhihirisha uwezo wako Mdogo wa kutafakari na kung'amua Mambo pia ujuhi umuhimu wa kukaa kimya ili usionekane mjinga
umeamua tu kunisakama ila hoja huna , halafu unapaswa kufahamu kwamba sijawahi kuhofia madongo duni kama hayo yako
 
Polisi kuna shida ya nidhamu. Utomvu wa nidhamu kwa askari wadogo kama mauaji kule Mtwara ni kielelezo cha hali halisi huko juu. Hili la Wankyo ni tukio la aibu mno kijeshi...
Sirro hastahili hiyo heshima kutokana na ukweli unaoufahamu
 
Pole zake ACP Wankyo, waswahili wanasema kama ipo, ipo tu!

Binafsi sijaona kosa la Wankyo kiasi cha kuanza kufanyiwa uchunguzi mitaani na mitandaoni wamejaa vibaka kibao bado wanatapeli watu, kwanini hao ndio wasiwafanyie uchunguzi?

After all, ikumbukwe kuwa wakati wa sherehe za kuagana kama hizo watu huwa wanakunywa pombe, hivyo kutoa kauli kama hizo ni jambo la kawaida kabisa hivyo Siro alipaswa kuwa mvumilivu wa kauli kama hizo!
 
Subiri kina masifa wenye mkoa wao watakujibu😀
 
WENYE MADARAKA kumbukeni VYEO ni Kama KOTI kuna KUVAA na KUVUA
 
nani amuwajibishe yule anaetaka kutawala miaka kumi mbele bila kidhibiti cha uchafuzi😄😄


hii inchi ukiwa na katucheo kubali msujudiaji mambo ya uropokaji sasa unafanana na Assistant officer😄😄
 
Kumekucha kumekucha wacha aende huko akakoroge chai na kalamu utamtukanaje mkunga na uzazi ungalipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…