IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

Taarifa zilizopo ni kwamba RPC KAGERA ambaye ametoka Pwani na kupelekwa mkoa Kagera ndugu Wankyo nadhani kauli ya jana ya kuhitaji ukuu wa Jeshi la Polisi imemuungiza matatani hii imeonesha hana nidhamu ya hali ya juu ndani ya jeshi hivyo basi staff officer aliyepo mkoa wa Rukwa ameteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera na Wankyo amepelekwa makao makuu ya jeshi mkoani DODOMA ambapo ni mji mkuu wa tanzania.

Ikumbukwe kuwa kauli aliyotoa jana kiutendaji ndani ya jeshi la polisi huku akijuwa mkuu wake wa kazi yupo na anafanya kazi hakustahili kusema kuwa mkuu wake wa kazi anafanya kazi ila yeye akipewa ukuu wa jeshi anaweza kufanya vizuri zaidi hii imeonesha kuwa nafasi aliyeteuliwa na amri jeshi mkuu hatoshi kuliongoza jeshi hivyo basi kwa kuwa jeshi huongozwa kwa nidhamu ya hali ya juu ndiyo maana mabadiliko hayo yamefanyika ili akae makao makuu ajifunze nidhamu pamoja na kuandika vipeperushi mabalimbali vinavyolihusu jeshi la polisi.

Pia soma: Wankyo Nyigesa RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

View attachment 2168097
ACP Wankyo Nyigesa Alikosa kuwa IGP ubunge kwenye Jimbo lake unamsubiri akistaafu Jeshi.
 
Kama Kuna kiongozi awe waziri, spika au jaji aliyechoka kazi, aje atamke kwamba atawania urais 2025.
Atajua hajui kabla hakujacha
Hizi nidhamu za uwoga wenzetu kunyaland walishaachana nazo......siasa zao ziko open sana mtu yoyote anaweza kum challenge kiongozi wa juu akiwemo rais kisiasa, tukiendeleza hizi siasa za uwoga na unafiki hatutafika kokote...
 
Kwanini huu uzi umeletwa kwenye jukwaa la siasa badala ya kule kwingine?
 
Haina shida, lakini ameonesha ulazima wa Jeshi la Polisi kuwa nidhamu. Haiwezekani subordinate aongee namna ile halafu aachiwe kirahisirahisi. Ile Kauli iliwahi kutolewa na JPM akiwa Mkuu wa Majeshi wakati ule ambapo IGP Ernest Mangu asingeweza kumwajibisha.
Mmmmh, JPM aliwahi kuwa mkuu wa majeshi ya wapi mkuu?
 
Bangi siyo mboga Wakyo nahisi aliipuliza nyingi ikamshinda kuhimili, halafu ukizingatia ni homeboy wa Sirro wote wanatoka Kanda maalumu, na Bila Sirro Wakyo asingekuwa hapo alipo kiukweli alikosea sana Hana adabu hata angekuwa mtumishi au mfanyakazi wa sekta binafsi huo ni utovu wa nidhamu
Unajua kuna mtu mwingine anaweza akawa hataki nafasi fulani hivyo akaamua kuitosa kiaina hata kama ni nzuri.

Tukumbuke hata kipindi cha Jpm wapo ilizungumzwa kuwa atakayejitosa kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge basi watapoteza nafasi zao lakini bado wakajitokeza kina Mwanry, Ole Sendeka nk

Maana kwa akili ya kawaida tu huwezi kuropoka vile kama Wankyo
 
Unajua kuna mtu mwingine anaweza akawa hataki nafasi fulani hivyo akaamua kuitosa kiaina hata kama ni nzuri. Tukumbuke hata kipindi cha Jpm wapo ilizungumzwa kuwa atakayejitosa kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge basi watapoteza nafasi zao lakini bado wakajitokeza kina Mwanry, Ole Sendeka nk
Vyeo vya utumishi haviombwi, ingekuwa kuwa IGP lazima ugombee hapo sawa, ila kitendo Cha kuomba Rais akuteuwe ilihali unajua IGP yupo maana yake unatangaza uasi Kwa IGP aliyepo mamlakani, kutukabari kuwa Wakyo amemkosea Sirro na ameikosea taasisi ya Urais
 
Back
Top Bottom