IGP Sirro ana wakati mgumu kujifanya Mwanasiasa, ataishia pabaya

IGP Sirro ana wakati mgumu kujifanya Mwanasiasa, ataishia pabaya

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Hatuta shangaa IGP Sirro kubadilishwa inaelekea hakuna mtu ambaye anamwamini lakini kibaya zaidi amejiingiza sana kwenye siasa waziwazi.

Sirro atatumika na Rais Samia kujisafisha kwa mambo ya ajabu yaliyotokea haya ni mambo ambayo yatamfanya Rais Samia amtoe Sirro

1. Mbowe: Suala la Mbowe linaelekea kutoa aibu kubwa kwa mfumo mzima wa mahakama na siasa zetu. Lakini kwa kusafisha mambo Raisi Samia atasema yeye hakuagiza Polisi kumkamata Mbowe na hakutaka kuingilia mahakama. Vilevile kitendo cha Sirro kufanya mkutano kwa kumjadili Mbowe alikosea sana. Lakini kitendo cha Polisi kumkamata Mbowe Mwanza wakati wa mkutano ndiyo msumari wa mwisho kwa Sirro. Kesi yote imeonekana ni siasa tu. Kumtoa Sirro itakuwa rahisi sana.

2. Askofu Gwajima: Sirro asije kufikiria Rais Samia atampongeza kwa kitendo na vijimaneno alivyo mwambia waziri wa Afya. Sirro hapa kakosea sana angetakiwa kunyamaza na kuwaachia watu wa chini yake. Kitendo cha kisifa alichofanya ili ashangiliwe na watu ni kitendo cha kisiasa lakini wanasiasa wote makini wamenyamaza yeye ndiyo anajiingiza kwenye mjadala ambao ni kama vile anatoa maagizo Askofu Gwajima asikamatwe.

3. Lissu, Mo na wizi wa kura haya yote yametokea kipindi cha Sirro. Hii ni sababu mojawapo ya Sirro kutolewa.

4. Sirro hajawahi kuheshimiwa na maboss wake wa Polisi alionekana kama ni mtu wa maguvu asiye na maarifa. Huyu ni IGP wa Magu lakini Rais mwingine asingeweza kumchagua huyu kuwa mkuu wa Polisi. Sirro anafikiri yeye ni smart lakini ukweli ni kwamba yeye ni mtendaji tu sio smart hivyo.

5. Rais Samia atamchagua mkuu wa kupambana na rushwa kama IGP muda si mrefu
 
Back
Top Bottom