IGP Sirro: Askari mmoja analinda watu 2000

Wakati wa JPM haya maneno mbona hukuyasema
 
Askari fanyeni kazi zenu za kulinda raia na Mali zake haiwezekani tuwalipe halafu kazi tufanye sisi!
Nalog off
 
Bajeti imesha pitishwa kamanda Sirro unasubiri nini kuajiri vijana wapya kutoka huko jkt walio jazana humu mtaani?
 
Polisi hawajawahi kuwa wengi hata ukichanganya majeshi yote nchini na wale waliokwishastaafu hawawezi kufika milioni 10! Hivyo ajira ya watu hawa ingezingatia upembuzi yakinifu was mtu anayestahili kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao, tofauti na sasa ambapo ni baba kantuma kuanzia wanaopelekwa vyuoni na wanaofundisha kwenye vyuo hivyo wote hawana wito wa kazi ya kulinda raia bali kugeuza nafasi zao kitega uchumi.

Kwa sasa chanzo kikuu cha uhalifu wa aina zote Tanzania ni polisi ingewezekana usafi ukafanyika wa kutosha ndani ya jeshi hilo tusingeonauhalifu popote na hata kulinda sungusungu kusingekuwepo.
 
Tuna askari police kama elfu 28 hivi Tanzania
 
Ok tuje barabarani inakuwaje Kuna idadi kubwa ya traffic barabarani yaan kila baada ya km 5 traffic lakin vituon hawafiki hata Askari 20
 
Kwahiyo sungu sungu ndio watakamilisha usalama wa nchi
 
Bosi wake aliyepumzishwa si alikuwa hataki polisi jamii, na kuwa ni lazima polisi aogopwe na wananchi, sio kushirikiana nao! Igp analinda wananchi wangapi? Hawawezi kulinda ila kuwabambikia kila kesi wanaweza.
 
Askari atatulindaje akiwa kituoni, sisi tunalindwa na Mungu. Hao askari uchwara wa Sirro kila tukivamiwa na wabeba machine huwa wanafika Massa kadhaa baada ya majambazi kutikomea kusikojulikana.
Ongeza sautiiiiii
 
Kama hujui phylosofia ya uhalifu huwezi kumwelewa afande Sirro.Waizi tupo nao mitaani na majumbani tunapaswa tuwadhibiti kwa kuwa tunawajua na tunakaa nao.Hebu kila mtanzania kuanzia kesho ahakikishe hakuna mwizi nyumbani kwake kama hatutamaliza uhalifu kwa asilimia 75 ili ibakie domestic violence ambayo polisi hawezi kuizuia.Acheni kucoment msiyoyajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…