IGP Sirro awaonya wahuni wanaotaka kuvuruga Msiba wa Mzee Mkapa

IGP Sirro awaonya wahuni wanaotaka kuvuruga Msiba wa Mzee Mkapa

Troll JF

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
7,804
Reaction score
12,237
IGP AWAONYA WALIOPANGA KUVURUGA SHUGHULI YA MAZISHI YA MZEE MKAPA
“Kama kuna watu wanataka kuiharibu hii shughuli yetu tutawashughulikia,” – Kauli ya IGP Simon Sirro akiwaonya wanaopanga kuvuruga shughuli ya mazishi ya Mzee Mkapa.

Ikiumbukwe mapema ya leo Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vilizuia Kundi kubwa la Wahuni waliotaka kuingia uwanjani baada ya Rais Magufuli kuwasili.

Hapa IGP ameteleza, siyo kila Tamko ni lazima litamkwe.. Na siyo kila Tamko ni lazima liambatane na vitisho..
 
anaongea na maruhani, maana ukitafakari hakuna umuhimu wowote kufanya fujo kwenye mazishi, ni uongo Wa kiwango cha changarawe!
 
Hivi ktk hali ya kawaida nani anaweza kufanya fujo kwenye mazishi tena ya rais mstaafu? Labda awe siyo mtanzania
Wanashangaza, wanafanya watu wajinga sana kuwa wataamini kila wasemalo. Hivi nani awezaye fanya fujo hizo msibani kweli?
Ni sawa na tumsikie paroko au mchungaji anatangaza kanisani "jumapili ijayo waumini waliopanga kunya humu ibadani wata shughulikiwa" halafu watu waamini
 
Vitu vingine ni kutiana ujinga na kweli wanawapata wadanganyika
Wanashangaza, wanafanya watu wajinga sana kuwa wataamini kila wasemalo. Hivi nani awezaye fanya fujo hizo msibani kweli?
Ni sawa na tumsikie paroko au mchungaji anatangaza kanisani "jumapili ijayo waumini waliopanga kunya humu ibadani wata shughulikiwa" halafu watu waamini
 
Makamanda pasi na kejeli afahamishwe afande IGP mshikamano na utayari wetu sote kama Watanzania katika kumsindikiza mzee wetu kwa amani.

Kwa hakika baadhi yetu tuliofika mapema zaidi pale uwanjani leo, tuliwawakilisha vilivyo makamanda wengine wote ambao hawakuweza kuipata nafasi ile ya kuingia ndani ya uwanja kwa shughuli ya leo.

Ahakikishiwe afande IGP ushirikiano, mshikamano na hata kuwakilishana kwetu kutakavyokuwa ikibi hadi Lupaso.

Apumzike kwa amani rais wetu mzee Mkapa.
 
Hivi ktk hali ya kawaida nani anaweza kufanya fujo kwenye mazishi tena ya rais mstaafu? Labda awe siyo mtanzania
Kama siyo mtanzania ndiyo ataogopa zaidi. Mimi naamini hakuna binadamu mwenye mawazo ya kufanya fujo msibani
 
Siro mbona anataka kujiondolea heshima? Hivi kuna mwenye timamu anaweza kuvuruga shughuli za msiba?

Kuvuruga shughuli za msiba wanafanyaje? Watazuia asizikwe? Watapiga kelele wakati wa ibada ya kumsindikiza? Wataondoka na mwili wa marehemu? Watawazuia watu wasimzike marehemu? Hata sielewi anayetaka kuvuruga shughuli ya maziko ya mtu kama Rais mstaafu, mtanzania mwenzetu, aliyetutoka ghafla, atafanyaje hasa!
 
Wanashangaza, wanafanya watu wajinga sana kuwa wataamini kila wasemalo. Hivi nani awezaye fanya fujo hizo msibani kweli?
Ni sawa na tumsikie paroko au mchungaji anatangaza kanisani "jumapili ijayo waumini waliopanga kunya humu ibadani wata shughulikiwa" halafu watu waamini
Mbona uwanja wa uhuru mlitaka kuingia wakati rais ameshaingia? Then mkaanza kudanganya dunia kuwa mmezuiwa wakati makosa ni yenu?
 
Hakuna mtu wa aina hiyo vinginevyo awe ni kichaa labda ameenda kuokota mabaki ya chakula.
Kama siyo mtanzania ndiyo ataogopa zaidi. Mimi naamini hakuna binadamu mwenye mawazo ya kufanya fujo msibani
 
Back
Top Bottom