IGP Sirro, hakuna anayekuunga Mkono

IGP Sirro, hakuna anayekuunga Mkono

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Kwa matamshi yako ya juzi na ulivyolishughulikia suala la marehemu Hamza, hakuna anayekuunga mkono. Kila mtanzania mwenye akili, mpenda haki, ukiacha wanaojikomba wapate mlo wao (wanafiki), watu wema, wapenda haki wanakulaani kwa matamshi yako.

Unaonekana kuwatetea mapolisi pamoja na kuwa wamejijengea sifa ya kuonea watu , kula rushwa na maovu mengine (ingawa siyo wote but by a majority wako hivyo).

Rais wako alionya juu ya uonevu na kutumia nguvu kupita kasi, UKAMPUUZA.
 
Kwa kumbukumbu zangu sijawah kushuhudia chadema wakimuunga IGP yeyote
Na hata akija mwingne chadema msitegemee mserereko tena ajaye ni bora siro
Mwisho wa siku sijawahi kuona mtu yeyote ambaye ni msimamizi wa sheria akapendwa na watu.

Polisi dunia nzima hawapendwi na watu.

Hata Walimu wa nidhamu huko mashuleni HAWAPENDWI.

Kwahiyo mimi sioni cha kujadili hapa zaidi ya umbeya na upuuzi tu.
 
Kwa kumbukumbu zangu sijawah kushuhudia chadema wakimuunga IGP yeyote
Na hata akija mwingne chadema msitegemee mserereko tena ajaye ni bora siro
Duu wanaotoa mada wote and wanaokoment ni CDM? acha fikra hizo laa hutafaidi Jamii forums
 
Iko hivi chadema mnalichukia jeshi la polisi juzi tumepoteza askari wanne kutokana na kushambuliwa na gaidi lkn chadema mkashangilia
Mtalipwa sawasawa na matendo yenu nikuhabarishe tu chuma kinachokuja mtamkumbuka siro
Nasty, Akili za ki-CCM, Chadema imetoka wapi katika andiko hili
 
Tatizo linaanza pale kigezo cha kujiunga na polisi hadi uwe na division 4 au umefeli
Mwisho wa siku afadhali hata hao Polisi, wanasiasa ambao ndio mabingwa wa kutukana polisi wao hata kuandika majina yao kwenye form za uchaguzi HAWAJUI
 
Kwa matamshi yako ya juzi na ulivyolishughulikia suala la marehemu Hamza, hakuna anayekuunga mkono. Kila mtanzania mwenye akili, mpenda haki, ukiacha wanaojikomba wapate mlo wao (wanafiki), watu wema, wapenda haki wanakulaani kwa matamshi yako.

Unaonekana kuwatetea mapolisi pamoja na kuwa wamejijengea sifa ya kuonea watu , kula rushwa na maovu mengine (ingawa siyo wote but by a majority wako hivyo).

Rais wako alionya juu ya uonevu na kutumia nguvu kupita kasi, UKAMPUUZA.
Sirro jiulize kwanini HAMZA hakuua RAIA zaidi ya POLISI WAKO?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ajabu kweli, ajabu zaidi ni wale wanasiasa wamekaa miaka zaidi ya 60 kwenye utawala lakini wameshindwa maliza tatizo la madawati shuleni, maji
Na ujinga zaidi ni kuendelea kufyatua watoto halafu wanaenda kukaa chini huko madarasani huku kazi yako mfyatuaji ni kunywa pombe na kulaumu watu.
 
Na ujinga zaidi ni kuendelea kufyatua watoto halafu wanaenda kukaa chini huko madarasani huku kazi yako mfyatuaji ni kunywa pombe na kulaumu watu.

Ni ujinga zaidi kutumia wanywa pombe na wafyatua watoto kama mtaji wa kura. Huku fika ikijulikana hawawezi patiwa
 
Tukio lilitokea alhamisi ya wiki iliyopita limeniumiza sana kufa kwa Bw. Hamza na askari polisi. Niwatakie pole kwa wafiwa wote.

Kama raia niliye na haki ya kutoa maoni, yangu ni haya: Lililoniumiza zaidi ni kufa kwa Hamza. Baada ya kugundua sababu ya kuchukua maamuzi yaliyowashitua wa-Tz ni kudhulumiwa madini yake iliniumiza sana.

Mazishi yake wamehudhuria watu tofauti na kila aliyepata nafasi ya kuhojiwa kuhusu Hamza maisha yake yanaonyesha hakuwa ni mwenye dosari na watu alikuwa ni mtu wa watu. Niliumia siku ya tukio lilitokea mpaka usiku nilishindwa kulala vizuri.

Mpaka muda huu naandika kifo cha Hamza kimeniumiza na kinaniumiza sana! Kimenitia simanzi mnoo! Dhulma aliyofanyiwa imemfanya achukue maamuzi aliyoyachukua ambayo yameleta mshituko ndani ya Taifa.

Siro anaulaghai umma wa waTz kwa maslahi ya kutetea ukosefu wa nidhamu wa askari wake. Askari hawana nidhamu kwa asilimia kubwa. Nchi yetu inafahamika jinsi ilivyo na haya ni maisha watu wanapoteza gharama za aina tofauti katika utafutaji wao. Jasho, damu na machozi yanawatoka katika utafutaji.

Askari polisi wamemfanyia dhulma. Wasitu-push raia tukavuka mipaka ya kushindwa kuhimili hasira zetu. Wengine hawana matatizo na mtu. Wakishvurugwa kipimo watakachokifikia kitaleta viulizo vingi, hususani kwa wapole. Na Hamza ndivyo alivyokuwa, ni mpole. Tunapenda amani, tunapenda amani.

Mwengine ukishakipoteza chake alichokipigania kwa nguvu kubwa haoni hasara ya yeye kujitoa liwalo na liwe kwa nguvu kubwa. Polisi wachunge jeshi lao liwe na nidhamu.

Sina chama.
 
Ni ujinga zaidi kutumia wanywa pombe na wafyatua watoto kama mtaji wa kura. Huku fika ikijulikana hawawezi patiwa
Maisha yako ni jukumu lako kwa asilimia 100. Ukikubali kuwa mtaji wa Mwanasiasa yeyote kwa ahadi kwamba atakufanyia chochote huo ni upumbavu wako mwenyewe.
 
Tunao muunga sirro tupo wengi.hii nchi wapumbavu kama nyie mko wachache sana yani huyu ni gaidi kaenda kuuwa askari wetu hivi kama mmoja wa wale askari waliouliwa angekuwa ni ndugu yako unayemtegemea ungekuja kuongea upuuzi kama huu!?
 
Back
Top Bottom