Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kesho akiwashauri warudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao.
Ameeleza kuwa, baadhi ya viongozi wamekuwa wakihamasisha wapiga kura walinde kura, kitendo ambacho amesema ni dalili ya kufanya fujo.
Amesema kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanaolinda kura ni Mawakala ambao kila Chama imepeleka.
Amesema, "Kuna Vyama vinajiona vimeshashindwa kwahiyo malengo na nia iliyopo ni kufanya fujo. Niwaombe sana Viongozi wa Siasa, wakati huu si wakati wa kufanya fujo"
Kuhusu Zanzibar, Sirro amesema karibu watu 42 wamekamatwa Pemba kwa madai ya kuwashambulia Polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana
Ameeleza kuwa, mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo na hatarajii kuwe na vifo vyovyote, akisisitiza wasingependa Uchaguzi ambao unasababisha maisha ya watu kupotea
Wala hakuna haja ya kukaa kituoni kulinda Kura kwasababu vituo vya kura vipo kwenye makazi ya watu hata camera za nyumba za jirani zitalinda Kura hata Mimi kwangu natazama kituo Cha kupiga kura dirishani kila kitu kinachoendelea naangalizia dirishani kwangu yaani hii technology ni shida Sana.
Mwambie Sirro, tunapiga kura na kulinda kura zetu. Kulinda kura sio kufanya fujo na kama wanataka watuue wote. Tulizaliwa siku moja na tutakufa siku moja. Imetosha kwa kweli!
Magufuli wako yupo kwenye taratibu za kuanza kuchunguzwa na ICC pamoja na kutolewa hati ya kukamatwa.
Tumeshasema kama mtaweza tuuweni tu wote, tulizaliwa siku moja na sote siku moja tutakufa. Kesho tunapiga kura na kuzilinda, full stop
Haki haiombwi babulai inapiganiwa acha walinde kura zao ccm hawana haja ya kulinda,wana policcm na necccm watawasaidia kuiba za wengine wawaongezee maana huwaga hazitoshi miaka yote.
Wala hakuna haja ya kukaa kituoni kulinda Kura kwasababu vituo vya kura vipo kwenye makazi ya watu hata camera za nyumba zajirani zitalinda Kura hata Mimi kwangu natazama kituo Cha kupiga kura dirishani kila kitu kinachoendelea naangalizia dirishani kwangu yaani hii technology ni shida Sana.
Hao polisi waliomwaga kila kona nchi hii kwanini wasingepewa kazi ya kuzuia hizo dalili kwenye hivyo vituo? wakae na hao wanaolinda kura halafu tuone kama patakuwa na vurugu.