Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Kukaa na kulinda kura ni dalili ya kufanya vurugu, baada ya kupiga kura rudini nyumbani

Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Kukaa na kulinda kura ni dalili ya kufanya vurugu, baada ya kupiga kura rudini nyumbani

Piga kura yako rudi nyumbani, utaratibu wa mawakala unatosha kabisa kulinda kura za kila chama
Mungu ibariki Tanzania
Ni kweli wapiga kura wasikae kwenye kituo, lakini wanaruhusiwa kukaa mita 200 nje ya kituo. Ndiyo sheria. Tusiwalazimishe kwenda nyumbani kama hawataki, na wanataka kukaa hapo penye mita 200 nje ya kituo. Polisi wawaangalie, kama wako umbali usiopungua mita 200 wawaache!
 
Nilimaanisha waliokwishapiga kura wanaruhusiwa kukaa umbali usiopungua mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura - kisheria!
 
Mwambie Sirro, tunapiga kura na kulinda kura zetu. Kulinda kura sio kufanya fujo na kama wanataka watuue wote. Tulizaliwa siku moja na tutakufa siku moja. Imetosha kwa kweli!
Naona unaandika script za igizo la kishujaa😂.
 
Mwambie Sirro, tunapiga kura na kulinda kura zetu. Kulinda kura sio kufanya fujo na kama wanataka watuue wote. Tulizaliwa siku moja na tutakufa siku moja. Imetosha kwa kweli!
Labda utakuwa unalinda kura hapa JF
 
Yeye ndio apige salute arudi nyumbani.

Tutawakomba mavi kesho
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kesho akiwashauri warudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao....
Huhitaji Kumaliza la Saba Kujua Tunachosubiri kama Nchi ni kujia Magu anashibda kwa Asilimia ngapi... Maana ushibdi Haupingikii ulikuwepo Upo na Kesho unatimilizwa.

Tangazo hili Kwenye Akili na Majukumu watalielewa Ila Wahuni na Wapuuzi Watakuwa wabishi ndio mtao kula kipigo cha mbwa mwizii
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchiniTanzania IGP Simon Sirro amekanusha kutokea mauaji na
badala yake amesema jeshi hilo limewakamata vijana 42 kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa Pemba hapo jana.

Chanzo: bbc swahili
Screenshot_20201027-171608_Twitter.jpg
 
Inspekta Jenerali wa polisi Simon Sirro amesema watu 42 wamekatwa Zanzibar wakihusishwa na tuhuma za kuwashambulia polisi waliokuwa kwenye majukumu yao.

Hakuna vifo vilivyoripotiwa, amemaliza afande Sirro.

Maendeleo hayana vyama!
Sirro ni muongo anajua watu wameuwawa na anajua idadi ya watu waliouwawa. Na sisi tunajua na tuna ushahidi kamili. Tutalipiza kisasi.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kesho akiwashauri warudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao.

Ameeleza kuwa, baadhi ya viongozi wamekuwa wakihamasisha wapiga kura walinde kura, kitendo ambacho amesema ni dalili ya kufanya fujo.

Amesema kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanaolinda kura ni Mawakala ambao kila Chama imepeleka.

Amesema, "Kuna Vyama vinajiona vimeshashindwa kwahiyo malengo na nia iliyopo ni kufanya fujo. Niwaombe sana Viongozi wa Siasa, wakati huu si wakati wa kufanya fujo"

Kuhusu Zanzibar, Sirro amesema karibu watu 42 wamekamatwa Pemba kwa madai ya kuwashambulia Polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana

Ameeleza kuwa, mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo na hatarajii kuwe na vifo vyovyote, akisisitiza wasingependa Uchaguzi ambao unasababisha maisha ya watu kupotea

View attachment 1613634

Naomba kueleweshwa:-

Kazi ya Polisi ni KUSAMBAZA MASANDUKU YA KURA au KULINDA MASANDUKU YA KURA?

ITAFIKA MAHALI HATA BENKI , BADALA YA KULINDA, WATATAKA KUHAKIKI FOMU ZA KUCHUKUA au KUWEKA PESA KUTOKA KWA WATEJA WA MABENKI HAPA TANZANIA.
 
Haturudi nyumbani kama mmepanga kutuua mbona ni sawa tu?

Tutapiga kura na kubakia vituoni. Tuko tayari kwa lolote.
 
Naomba kueleweshwa:-

Kazi ya Polisi ni KUSAMBAZA MASANDUKU YA KURA au KULINDA MASANDUKU YA KURA?

ITAFIKA MAHALI HATA BENKI , BADALA YA KULINDA, WATATAKA KUHAKIKI FOMU ZA KUCHUKUA au KUWEKA PESA KUTOKA KWA WATEJA WA MABENKI HAPA TANZANIA.

siku moja utataka kujua kazi ya walimu ni kufundisha au kutunga mitihani!!!!!maana wanatumia muda mwingi kutunga.
 
Kuzuia wasimamizi,mawakala kuingia na simu ,kutowapa nalala. Ya matokeo ya Kura mawakala na kusambaza wanajeshi mitaani zote ni dalili za wizi wakura .ndio mama kulinda Kura muhimu
 
Mwambie Sirro, tunapiga kura na kulinda kura zetu. Kulinda kura sio kufanya fujo na kama wanataka watuue wote. Tulizaliwa siku moja na tutakufa siku moja. Imetosha kwa kweli!
Unapotosha wenzako, kesho nasubilia picha ukiwa na wenzako mkilinda kura
 
Back
Top Bottom