IGP Sirro: Nimeumia sana kuwasikia Wanafunzi wakiniambia hawajaenda shule kwa sababu wanaogopa kuuawa na Wamasai hapa Kilindi

IGP Sirro: Nimeumia sana kuwasikia Wanafunzi wakiniambia hawajaenda shule kwa sababu wanaogopa kuuawa na Wamasai hapa Kilindi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
IGP Sirro amefanya ukaguzi wa kushtukiza wilayani Kilindi ambako wananchi sita wameuawa katika mapigano kati ya Wakulima na wafugaji.

Sirro amesema alijisikua maumivu moyoni baada ya kuelezwa na wanafunzi kuwa wameshindwa kwenda shule wakihofia kuuliwa na wamasai.

IGP Sirro ameahidi kupeleka kikosi maalumu cha askari kutoka Tanga mjini na Morogoro ili wakaimarishe ulinzi wilayani hapo na askari waliokaa Kilindi kwa muda mrefu ameahidi kuondoka nao.

Aidha Sirro amewataka wote walioshiriki kufanya mauwaji ya watu hao 6 kujisali!isha mara moja.

Sirro-kilindi.jpg


Chanzo: Star TV
 
Suluhu ya kudumu ya hii ishu ni nini?
Ardhi ni lazima ipimwe na kuwekewa mipaka kisheria.

Kutengwa maeneo maalum/ mapori ya wafugaji kuchunga.

Sheria zilizopo zitiliwe mkazo na kutekelezwa kwa ufasaha mfano ile ya kupiga marufuku kusafirisha mifugo kwa kuwatembeza.

Ziundwe kamati za ulinzi mpaka huko mashinani zitakazoshirikisha pande zote mbili husika (wafugaji na wakulima).

Elimu ya ufugaji wa kisasa na yenye tija.

Kuwepo na maridhiano baina ya pande mbili zenye kuhusika na migogoro.

Mamlaka ijitahidi kupeleka mahitaji muhimu ya kijamii kwenye maeneo yaliyoathirika na mgogoro.

Hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika kuchochea na kutekeleza vitendo vya jinai,ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Hao wafugaji tena wakimasai akili zao hazitofautiani sana na hiyo mifugo yao.

Wakulima ni kama yatima kwenye maeneo yenye wafugaji wa kimasai.

Wanafanya lolote halafu wanauza mifugo "kurefusha kamba za Polisi"
 
Hizo land use plan na climate change. Huwa mnajifunza INTELIJENSIA yake? Kulinda amani ni zaidi ya kubeba AK47 Rethink
 
Back
Top Bottom