Kamanda Sirro, kuna clip inatrend kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha jeshi lako la polisi likivamia mkutano halali kabisa wa chama cha ACT wazalendo.
Mkutano wao huo wa amani na wa ndani ulikuwa ungali ukiendelea huku wananchi wakiwa wanaimba nyimbo kumkaribisha kiongozi wao wa chama, ghafla polisi wakajitokeza na kuvamia mkutano huo huku mmoja akotoa maelekezo yakionyesha Zitto aondolewe kwa nguvu.
Wakati huohuo Polisi ikiendelea kuwasumbua wapinzani kufanya shughuli zao halali zilizoko kwa mujibu wa katiba, Chama cha mapinduzi chenyewe kimeonekana kuendelea kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa na yeyote.
Tunalaani matendo haya ya polisi, ningependa kumueleza IGP Sirro, Si vizuri jeshi la polisi kufanya mambo kama Mob, tunapojaribu kujenga Taifa letu.
Vyama vya upinzani vipo kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba, na vina haki ya kufanya siasa kwa uwazi kabisa bila kubughudhiwa na Yeyote.
Kitendo cha polisi mara kwa mara kusumbuasumbua wapinzani, au kutoa matamko ya kuashiria kuwa linatumika kisiasa, ni mambo ya kihuni, aibu na hayafai hata kidogo. Hayo mambo hayawezi kuleta heshima kwa jeshi la polisi nchini.
Tunalitaka jeshi la polisi kuacha mara moja matendo haya aibu na yasiyokuwa ya kiungwana hata kidogo.
Hayo mambo hayalifai jeshi la polisi, hayo mambo hufanywa na mobs lakini si kwa jeshi la polisi linalopaswa kuheshimiwa
IGP Sirro unafeli sana kwenye angle hii, usikubali kutumika kisiasa!
Hii video ya uvamizi wa mkutano wa ACT huko Kilwa inasikitisha sana
Policcm! Ni jeshi lisilo na tofauti kabisa na lile la enzi za Mkoloni. Limejikita zaidi kuibeba Ccm huku likiwakandamiza wapinzani na wale wote wanao tofautiana na Ccm au Serikali ya Ccm.
Aibu kwenu Polisi! maana mnafahamu fika mnachokifanya siyo sahihi. Ila kwa makusudi kabisa mnajitoa ufahamu.
Hili jeshi lililokamilisha ripoti batili ya shambulizi la Mbowe ndani ya siku tatu. Ripoti ya kujeruhiwa kwa Lissu inamsubiri mwenyewe arudi. Kama Lissu angekufa katika lile shambulizi je?
Kamanda siro ni mchapakazi sana,,tena wanajf ndo mlipiga debe apewe u IGP toka enzi za jk,mlitaka apewe U igp,leo munageuka tena?,,,
Chapa kazi kamanda
Hivi vitu mbona vipo sana Afrika huko mkuu! Sema mnakosa kumbukumbu labda,yanayofanywa na Polisi ni kua nchi imetekwa na wadhalimu,wananchi wamepokwa mamlaka na Uhuru wao. Kuna tofauti gani wakati wa ukoloni na wakati katika haki na Uhuru wa mtu mweusi apo Afrika?
Kuna kila dalili kuwa huenda kuwa polisi itabidi cv ionyeshe mtu ni Chama gani,kuna dalili hyo --inaskitisha sana kuona uonevu huu ukifanyika waziwaz ktk nchi hii...