IGP Sirro, Tafadhali usiligeuze jeshi la polisi kama mob

Wewe huna akili!Usichokijua ni kwamba Sirro hana makosa,yeye huwa analazimishwa kutoka juu kufanya hayo maovu!
 
Kwa hakika CCM imefika pabaya sana katika matumizi ya hili jeshi! Naskia wanaotoaga taarifa za vikao au shuguli za wapinzani ni wanachama wa CCM na hasa mabalozi na wenyeviti wa mitaa. Ndio maana kila siku utasikia haya mambo ya kukamatwa wapinzani kila kona! Nilikuwa nasubiri kwa hamu nisikie sababu ambayo jeshi la polis litaitoa kuhusu kukamatwa akina Zitto na mashtaka watakayofungulia! Walikuwa katika kikao cha ndani cha kupokea wanachama, Je hapa walikuwa na kosa gani? Mbona wakati hayo yakiendelea siku hiyohiyo vyombo vya habari vilimuonyesha Polepole akiwa na Tulia Ackson wakifanya mikutano wanafunzi wa vyuo vikuu kule Mbeya na tena sio wabunge wala viongozi wa eneo hilo! Si huko tu katika maeneo mengi tu CCM wameonekana katika vyombo vya habari wakifanya shughuli za siasa, huku wengine kama mbunge wa Ruangwa wakianzisha ziara za kampeni na huku wakitumia miradi ya serikali kufanyia siasa! Najiuliza huu ubaguzi wa kisiasa tunaoujenga Tanzania utatufikisha wapi! Sidhani kama kwa mwendo huu tuna safari ndefu ya amani yetu! CCM na serikali yake wanaamini matumizi makubwa ya vyombo vya dola ndio njia ya kulinda amani , lakini kiukweli mtazamo huu si sahihi hata kidogo! Kilichopo sasa sio utii wa amri na maagizo ya vyombo vya dola , bali ni woga na uvumilivu tu wa wananchi, hivi vyote huwa vina ukomo wake kadri ukandamizaji unavyozidi!
 
Hili jeshi lililokamilisha ripoti batili ya shambulizi la Mbowe ndani ya siku tatu. Ripoti ya kujeruhiwa kwa Lissu inamsubiri mwenyewe arudi. Kama Lissu angekufa katika lile shambulizi je?
Hatuna jeshi la polisi, tuna an organized crimes - gang chini ya mwamvuli wa jeshi la polisi. Naomba sana uonevu uendelee kutokea, maana ndiyo tuelekeavyo kwenye ukombozi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Km hawakuomba kibali unamlaumu vipi IGP?
Hivi huko Police huwa kuna file LA kutunzia barua za kuomba vibali vya kufanya mikutano ya kisiasa?Je,IGP anaweza kutuonyesha hilo file tulione lilivyojaa barua za vikao vilivyoruhusiwa kufanywa na CCM kutoka kwa OCD wa wilaya yoyote hapa Tanzania?
Tunadhani CCM huwa hawaombi vibali,sheria inataka chama kinachotaka kufanya mkutano kutoa taarifa na kuomba ulinzi wa Polisi na siyo vibali.
Sheria zinapovunjwa na wasimamizi wake,huhatarisha na kurahisisha uvunjifu wa Amani. Nchi hii kama siyo hekima ya wapinzani, damu ingeshamwagika sehemu nyingi hapa Tanzania. Police Brutality is at the peak,Judiciary has became a Toothless Organism,we are done.No one is safe.
 
Hizo ni porojo tu
 
Paka hugeuka chui akifungiwa katika chumba cha adhabu ya kipigo,ukitaka jaribu uone.CCM wanawatumia Polisi vibaya nao wamekubali hilo.Yatakayokuja kutokea huko mbeleni hawayaoni maana wamevaa Tinted Wooden Goggles.
Aibu hii baadaye itakuwa juu yetu sote kwa kutokuchukua hatua mapema.
Wanasheria na Mawakili wasomi,tuokoeni wenzenu.
 
Ni kwali kabisa wanasheria na mawakili wasomi wanaweza kutuokoa! Lakini pia mfumo wetu wa mahakama sio huru! Na hapa nazani tunahitaji njia nyingine mbadala na mkato kama wanayoitumia wao CCM! Rejea utata wa maamuzi katika kesi mbalimbali zilifunguliwa na wapinzani! Mfano hii kesi ya hapa majuzi iliyofunguliwa na CHADEMA dhidi ya Spika Ndugai kuhusu kuutambua ubunge wa Mwambe! Mfano mwingine zile kesi nyingi zilizofunguliwa na uongozi halali wa CUF upande wa Maalim Seif dhidi ya upande wa Lipumba ambao ulikuwa batili, ikiwemo ya wale wabunge 8 wa CUF waliovuliwa ubunge isivyo halali na Lipumba! Ukifuatilia hayo yote na mauzauza mengine ya hukumu dhidi ya kesi za wapinzani, utaona hata kwenda mahakama za hapa nchini ni kupoteza muda labda mahakama za nje ya nchi kama ile ya EAC!
 
Tunahitaji kusaidiwa na yeyote,iwe ni hapahapa nyumbani au nje.Tunahitaji Uhuru wa Tanzania na matunda yake tufaidi sote.Sasa hivi tulikofikia kwenye haki ni CCM pekee.
 
Huwa wanahudhuria kweli hata mikutano ya kimataifa kweli?Hawa ili wajifunze,wanazidiwa hata na polisi wa Malawi huwezi kuta wanatumiwa na chama chochote.
Haya Mambo ya kuwafanya watu wazoee kukamatwa si tija Wala uhai kwa taifa.
Yule bwana ndie anaewaagiza ametuharibia Sana taifa letu.
 
Haya matukio na picha za hivi siyo nzuri kabisa kwa afya na mustakabali wa taifa.
Sijawahi kumkubali zitto lakini clip hii imenipa hasira sana dhidi ya hao wanaopenyzwa ndani ya jeshi la Polisi ili kufanikisha agenda za la kulijaza hofu taifa.
 
Vikosi maalum. Vinaweza kufanya lolote wakati wowote. Hii ndio mbinu ya mwisho kabisa kwa ccm ambayo nayo inaelekea kufeli.
 
Haya matukio na picha za hivi siyo nzuri kabisa kwa afya na mustakabali wa taifa.
Sijawahi kumkubali zitto lakini clip hii imenipa hasira sana dhidi ya hao wanaopenyzwa ndani ya jeshi la Polisi ili kufanikisha agenda za la kulijaza hofu taifa.
Na lengo ni threatening kama ilivyokuwa kwa akina Esta Bulaya na Halima.
 
Kwa awamu hii ya tano hakuna tofauti na wakati wa Carl peters na ukoloni wa mwingereza. Hofu hofu hofu. Wizi wizi wizi. Ua ua ua. Piga piga piga.
 
Kama jeshi linataka kumkaba mtuhumiwa aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30! Si ishara nzuri kwa taifa kwa mtendewa kugeuzwa jambazi.
 
Hatuna jeshi la polisi, tuna an organized crimes - gang chini ya mwamvuli wa jeshi la polisi. Naomba sana uonevu uendelee kutokea, maana ndiyo tuelekeavyo kwenye ukombozi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hizo ni porojo tu
Anayetupeleka kusiko anaitwa NDULI MAGU.
 
Kamanda siro ni mchapakazi sana,,tena wanajf ndo mlipiga debe apewe u IGP toka enzi za jk,mlitaka apewe U igp,leo munageuka tena?,,,
Chapa kazi kamanda
Amegeukwa baada ya kugeukwa
 
Kwa awamu hii ya tano hakuna tofauti na wakati wa Carl peters na ukoloni wa mwingereza. Hofu hofu hofu. Wizi wizi wizi. Ua ua ua. Piga piga piga.
Heri ya wakoloni na makaburu walitutawala kwa kutuletea maendeleo tuliyaona kuliko Hawa wakoloni weusi wa kisukuma, mnyoosho mwanzo mwisho wanatutawala huku wakituletea ufukara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…