IGP sirro wawajibishe wakuu wa vituo vya polisi Katavi

IGP sirro wawajibishe wakuu wa vituo vya polisi Katavi

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
11,432
Reaction score
24,596
Wakuu salama,

Kumeibuka wimbi la watoto wadogo miaka 15-17 kwa Dar wakiitwa panya road huku katavi wamekuwa na vikundi vya vijana hao (damu chafu, mazombi, watoto wa kaburi moja, fulldoz, avengers, changanyikeni), wakishirikiana na baadhi ya polisi wasio waaminifu kufanya vitendo vya kipuuzi mtaani

Zaidi ya miezi mi 5 Hali ya usalama mitaa ya katavi haiko vyema, polisi wanaofanya doria wamekuwa na kawaida ya kukaa vijiwe vya pombe badala ya kuzunguka kuimarisha usalama wa raia

Watoto hawa wakipigwa ama kukamatwa na raia polisi wamekuwa wakiiwaachia na kurudi uraiani kuendeleza vurugu

IGP sirro ondoa wote wanaohusika na ulinzi na usalama katavi wameshindwa kazi maana vikundi hivi vimekuwa vikifanya matukio mchana kweupe wakiwa na silaha za jadi
 
Si mlisema wa mikoani mpo ngangari iweje tena mnatolewa kamasi na vijukuu vyenu??
 
Wakuu salama,
Kumeibuka wimbi la watoto wadogo miaka 15-17 kwa Dar wakiitwa panya road huku katavi wamekuwa na vikundi vya vijana hao (damu chafu, mazombi, watoto wa kaburi moja,fulldoz, avengers,changanyikeni,) wakishirikiana na baadhi ya polisi wasio waaminifu kufanya vitendo vya kipuuzi mtaani

Zaidi ya miezi mi 5 Hali ya usalama mitaa ya katavi haiko vyema, polisi wanaofanya doria wamekuwa na kawaida ya kukaa vijiwe vya pombe badala ya kuzunguka kuimarisha usalama wa raia

Watoto hawa wakipigwa ama kukamatwa na raia polisi wamekuwa wakiiwaachia na kurudi uraiani kuendeleza vurugu

IGP sirro ondoa wote wanaohusika na ulinzi na usalama katavi wameshindwa kazi maana vikundi hivi vimekuwa vikifanya matukio mchana kweupe wakiwa na silaha za jadi
Yeye mwenyewe Sirro alipaswa kujiuzulu kutokana na utendaji mbovu wa taasisi anayoiongoza.
 
Kwani huko petrol ina bei gan kama mnaona polisi wameshindwa mnavitafuta mnavipiga moto vinakimbia vyenyewe
 
Hapo ndipo mnapofeli,yaani watoto mnashindwa kuwadhibiti?

Kamateni kadhaa muwatolee mfano wenzao,hakyanani wataogopa.

Kama wazazi wao wamewashinda,ulimwengu uchukue nafasi ya baba na mama.

Nijuavyo ulimwengu haujawahi kushindwa kumfundisha mtu.
 
Si mlisema wa mikoani mpo ngangari iweje tena mnatolewa kamasi na vijukuu vyenu??
Mkuu Hawa watoto wako wengi mno huwezi ua wote, tumeshatia vilema watoto wa kutosha wengine tukiwapeleka polisi kesho wanarudi
 
Hapo ndipo mnapofeli,yaani watoto mnashindwa kuwadhibiti?
Kamateni kadhaa muwatolee mfano wenzao,hakyanani wataogopa.Kama wazazi wao wamewashinda,ulimwengu uchukue nafasi ya baba na mama.Nijuavyo ulimwengu haujawahi kushindwa kumfundisha mtu.
Mkuu tuko kwenye mipango Iyo si muda utasikia mauaji ya watoto Katavi
 
Mkuu tuko kwenye mipango Iyo si muda utasikia mauaji ya watoto Katavi
Msiwaue,ila wapeni kichapo cha hatari,mi naogopaga sana kuua.Wapimbwe na wafipa pamoja na wasukuma wa huko mnafeli sana,au(hao watoto) ni zao la wale wa kule kambi ya wakimbizi.... kwamba wana asili ya Burundi?
 
Hawa watoto wapuuzi sana mkuu wanajiunga makundi walianza taratibu kuiba chuma chakavu, wameng'oa sana misaraba, sa hivi wamehamia kupora watu na polisi wapo
 
Polisi/wazazi wanavitetea hivi vitoto imebaki kuviua tu, kuna bwana mmoja vilimzinga akavigonanisha vichwa vikazimia amepewa kesi ya kutaka kuu na ipo kituoni mpaka sasa.

Ifike sehemu kama askari hawawezi kazi Basi wasiwe kizingindi kwa wanaume wanapotaka vifunza adabu hivi vitoto.
 
Leo polisi wamefanya doria kukamata vijana wenye makundi makundi yasiyo eleweka

Naona ni baada ya kuwasema humu
 
Back
Top Bottom