IGP Wambura awataka Watendaji wa Dawati kutanua wigo wa mashirikiano

IGP Wambura awataka Watendaji wa Dawati kutanua wigo wa mashirikiano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchin IGP Camillus Wambura amewataka Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kuendelea kutanua wigo wa mashirikiano na wadau mbalimbali katika kukomesha na kudhibiti wimbi la vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vinavyojitokeza kwenye jamii.

IGP Wambura ameyasema hayo wakati akifunga kikao cha watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilichofanyika jijini Dodoma ambapo pia amewataka watendaji hao kukahakikisha wanaendelea kutoa elimu ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwa makundi yote kwenye jamii.

Naye kamishna wa Polisi Jamii CP Faustine Shilogile amewataka watendaji wa Dawati la Jinsia kuendelea kutoa huduma bora kwa mteja ikiwa sambamba na kuyazingatia mafunzo waliyopatiwa ili jamii iweze kuondokana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa Watoto.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-12-13 at 19.05.10.mp4
    20.4 MB
Naye huyu yupo kama sanamu tu! Hivi anafanya kazi gani duniani
 
Back
Top Bottom