Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Nimesikiliza kwa umakini Mbowe, Lissu na Mnyika kuwa wamepigwa sana na Jeshi la Polisi.Mbowe amedai kuwa hawataenda kuripoti katika vituo vya Polisi kwa madai kuwa ni kesi hewa. Asante babanMbowe, Lissu na Mnyika wameeleza katika madai yao kuwa CP Awadhi Haji alimfokea RPC wa Mbeya kwa kuwalea lea akina Lissu hadi akaingia kazini mwenyewe. Nimesikitishwa sana na kitendo kilichofanywa na RPC Mbeya kushindwa kuwajibika na kutekeleza maelekezo ya kiongozi wake.
Mbeya ni sehemu ambayo inategemewa sana na CHADEMA kuanzisha vuguvugu, sasa ukiwa kamanda muoga muoga basi wewe hufai kuwa sehemu ya serikali.
Hiki kipindi cha kuelekea kwenye chaguzi tunahitaji makamanda wa Polisi wa mikoa na wilaya wenye uzalendo wa kweli, wanaojua nini maana ya maadui wa usalama wa Taifa, wanaotii serikali bila kulazimishwa, wanaojua kuwa kulinda nchi sio kazi ya lelemama.RPC Mbeya umenikwaza sana.Nakushauri IGP Wambura makamanda waoga waoga kama RPC wa Mbeya weka pembeni na uteue Kamanda mwingine ambaye ataweza kuufanya mji wa Mbeya utulie.
Kama sio CP mwenyewe kwenda Mbeya basi RPC alishakwishashindwa kutekeleza majukumu yake na Bavicha wangefanya wanayoweza kufanya.
IGP Wambura nakuomba sana huu ndio wakati sasa wa kulinda usalama wa nchi, fanya tathmini ya makamanda wako kama wana msaada kwako, njia pekee ya kupata utendaji kazi sahihi wa Makamanda wako wa mikoa na wilaya ni kuwauliza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, wao wanajua utendaji kazi wa Makamanda wao.Pata tathmini kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ili upangue uanze moja, huko tuendako kwa hali ninavyoiona ni ngumu.
Zipo nchi zinapenda kuona tukifarakana, nchi hizo zinafurahi kuona Chadema wakitukana viongozi na kutaka kuharibu amani na utulivu ndani ya nchi. Hatukubali hatukubali. Hawa Chadema mpango wao sio kushika dola wala nini, mpango wao ni kumkwamisha Rais Samia asijenge uchumi wa nchi.
Wameona miradi katika mashule, miundombinu ya barabara, mawasiliano, afya, kilimo, mifugo nk, sasa wana nini cha kusema zaidi ya kutafuta jambo ili waonekane wameonewa. We Mbowe unalalamika wakati hata kibao hujapigwa, We Mbowe hebu muogope Mungu wewe baba, wewe unaweza kutamba kweli umeteswa kuliko Professa Lipumba?
Wakati Lipumba anafanya haya unayoyanya wewe ss hivi alikumbana na balaa sio la kawaida, Lipumba hadi leo mkono wake mbovu, Lipumba ana makovu kibao mwilini, wewe hata shati hujachaniwa unalalamika kila siku kwenye media.We Mbowe acha hizo bwana.
Mwisho, unawadanganya wenzako wasiripoti kwenye vituo vya Polisi, unajua madhara yake, wasipoenda halafu wakakamatwa kwenye mawilaya yao utaenda kuwasaidia? Mbona unawafanya watu wajinga wengi baba.
Sasa nyie mlioambiwa msiende kuripoti akili za kuambiwa changanyeni na za kwenu.Ole wenu msiende.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - CHADEMA: Tutafungua kesi dhidi ya Sisty Nyahoza na Awadh Haji juu ya kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA