Small letter
JF-Expert Member
- Jun 7, 2024
- 280
- 177
Afande IGP Wambura, Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni ,taratibu na tamaduni mbalimbali zilizopo.
Iweje Leo watu waamue tu kuwaibia Watanzania wenzao na ninyi mliopewa dhamana ya ulinzi wao na mali zao mkae kimya?
Mfano, hawa wanajiita Mkopo Fasta walimpigia simu ndugu yangu wakamshawishi akope TZS 50,000 atalipa TZS 57,000 kwa wiki moja.
Alipoapply ule mkopo wakamkata elfu 16 wakampatia 34,000 tu.
Leo wametuma meseji kwangu na kwa watu wote walio kwenye simu yake kuwa wanamdai 153,000 na wanañitaka Mimi nimpigie simu ili awalipe ili hali namba yake wanayo.
Nikawauliza wakati huyo anakopa mlinipigia kutaka concern yangu kama rafiki au ndugu yake kama mnavyofanya Leo?
Nikawauliza pia kama wao wanafahamu gharama ya kumdhalilisha mtu mitandaoni kama wanavyofanya kwani kukopa ni Siri kati ya Mkopa na Mkopesha.
Ombi langu kwako Afande IGP.
Kwakuwa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba alishakiri kuwa BOT haijawahi kutoa leseni kwa hawa watu na wanachokifanya ni Wizi,Utapeli na Udhalishaji tu kwa raia,
Tafadhali Kamata hawa watu na wafikisheni mahakamani kwa mujibu wa Sheria ili wakasajili hizo Biashara zao na wafanye Biashara kwa Misingi ya Kisheria huku wakithamini faragha na utu wa watu.
Why umpatie mtu TZS 34,000 uje umdai TZS 153,000 tena kwa kumdhalilisha kwa Kila mtu.
HIVI TANZANIA TUNAKWENDA WAPI?