Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
IGUNGA: "MBUNGE NGASSA KUPIGA KAMBI JIMBONI KWA SIKU THELATHINI"
📌 Kufanya Ziara kwenye Vitongoji vyote vya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi
📌 Kukutana na Wananchi wa Kata Kumi na Sita za Jimbo la Igunga
Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa Anaanza Ziara ya Kikazi Jimboni kwa ajili ya;
1. Kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti kwa Wananchi.
2. Kuona Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
3. Kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwenye maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
4. Kuhamasisha Wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024
5. Kusikiliza Kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi
6. Kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Jimbo (NGASSA CUP 2024)
Wananchi Wote Mnakaribishwa. Mikutano itafanyika kuanzia ngazi ya Makundi ya Kijamii, Vitongoji, Mitaa, Vijiji na Kata kwenye maeneo yaliyoandaliwa na Viongozi.
"KAZI NA MAENDELEO"
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga