Elections 2010 Igunga wakisahihisha makosa yao tutawasamehe... ?

Elections 2010 Igunga wakisahihisha makosa yao tutawasamehe... ?

Maneno yako Mkuu yangekuwa yanaweza kuwafikia vijana wa Igunga wenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 45 tungeona mabadiliko makubwa sana Igunga ambayo pia ingetoa mwamko mpya kwa zone kubwa na muhimu sana kwa Taifa [Kwa Makabila ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wanyiramba na kwa kiasi Wanyaturu].Tatizo tulilonalo kwa makabila hayo ni mfumo wao wa maisha wa kijadi wa kuwa very royal pasipo kupinga kwa mwenye madalaka japo mhusika atendewi haki na mwenye madaraka.

Upole wa kitabia wa makabila hayo na mfumo wa utawala toka ukoloni na mpaka Serikali huru,tatizo limeendelea kuwepo kwa makabila hayo la kufuata maamuzi ya watawwala [order] pasipo kuhoji na ukitokea kuhoji au kupingana na kiongozi basi wewe ni tatizo kijamii,Na kwa kiwango kikubwa wazee wa kijadi au kijamii wakisimama na kusema kwa umoja wao basi sauti yao ni maamuzi ya jamii.

Umbumbu wa kiufahamu wa wenyeji wa vijijini wa makabila hayo imekuwa sumu hata katika maisha ya kawaida ya kusujudia watawala.Imewagalimu sana kwa majimbo mengi umeona hata aina [silika] ya Wabunge wanawaowachagua kama yule mheshimiwa wa Bastora.

Kwa kiwango kikubwa ninavyowajua makabila hayo ambayo kwa kiwango kikubwa wapiga kura wake walio wengi ni Wanawake na kwa tabia ya makabila hayo iliyowazi ni kuwa kiongozi wa familia ni Mwanamke,basi tegemea ushindi mwingine wa CCM wa Kisayansi.
DSN

Sijui unazungumzia Wasukuma wepi tusiowajua sisi, unaposema kiongozi wa familia wa wasukuma, wanyamwezi, wanyaturu ni mwanamke nakushangaa sana, kwa makabila uliyoyataja mwanamke hahesabiki kabisa kama sehemu ya familia sembuse kuwa kiongozi, hadi leo mtoto wa kike hatambuliki hata katika masuala ya urithi wa familia, mfano mdogo tu wanaume wakiwa wanajadili jambo fulani la kifamilia au kijamii mwanamke hatakiwi kuwepo sehemu ile hata kama akiwepo hatakiwi kuchangia chochote wana msemo 'wewe mwanamke utatuambia nini nenda jikoni'.

Bado mfumo dume unatawala sana makabila hayo na kiongozi wa familia bado ni mwanamme, labda sema kutokana na mwingiliano wa tabia za makabila mbalimbali na uchumi tegemezi kwenye familia siku hizi mwenye sauti ni yule mwenye nguvu ya uchumi awe kijana, mwanamke au mwanamme.

Nakubaliana nawe kuhusu upole wa makabila hayo lakini elewa mtu mpole akiamua kubadilika ni vigumu sana kum- convince otherwise, mfano ni matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambayo yaliishtua hata CCM, wabunge wengi wa upinzani wametoka sehemu hizo na kura nyingi za urais za upinzani zimetokea kule, jiulize Mwanza na Shinyanga ya miaka ya Nyerere ulinganishe na leo labda Tabora ya kina Rage ambayo nayo tunaweza kuanza kuona mabadiliko kwenye uchaguzi huu.
 
Mwanakijiji tafadhali sana naomba hii itoke kwenye magazeti ya kila siku na toleo moja maalum siku ya jumapili, wapiganaji wajitahidi gazeti lisambazwe igunga hata bure badala ya kurusha chopa tu!

Huu ujumbe unasomeka vyema na wana Igunga wanajuwa kusoma na kuandika.
 
View attachment 38036

UAMUZI wa wapiga kura wa Igunga mwaka 1994 ndio uliotupatia Rostam. Ni uamuzi huo huo ndio uliotupatia Rostam mwaka 1995 na ni uamuzi ule ule ndio uliomrudisha tena mwaka 2000. Ni uamuzi wa wapiga kura wa Igunga mwaka 2005 uliomrudisha tena Rostam tena akiwa meneja wa kampeni ya Rais Kikwete. Naam, ni uamuzi wa wananchi wa Igunga uliomrudisha tena Rostam mwaka 2010 kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 70. Ni wao wananchi wa Igunga waliolipatia taifa Rostam Aziz. Ni wao waliofanya kosa hili na kulirudia mara nne, tena kwa furaha.


Rostam alipoingia bungeni alikwenda na kupigania maslahi ya chama chake na ya biashara zake. Kwa kutumia migongo iliyopindika na nyuso zilizochoka za wana Igunga alikwenda bungeni na huko akajitengenezea mtandao wa watu wenye kuamini itikadi yake na matokeo yake ni kuwa siasa za Tanzania zikachafuliwa rasmi. Si kwa makosa ya Rostam peke yake tu, tukisema hivyo tutakuwa hatumtendei haki bali kwa kushirikiana na wabunge wengine na viongozi wengine wa CCM kututengenezea mfumo mbovu, dhalimu wa utawala.


Ni mfumo huu ambao umeendelea kuligawa taifa kati ya wale walio nacho na wale wasiokuwa nacho, wale wenye madaraka na wale wasio na madaraka, wale wenye nguvu na wale walio dhaifu. Ni mfumo ambao RA (kama anavyojulikana na wengi) ameshiriki kuujenga.
Hakuna wakati wowote ambapo RA amewahi kusimama kuukosoa mfumo huu au hata kuonesha kuwa anajua madhara yake.
Tunaambiwa ni miongoni mwa wabunge wa chache ambao hawajawahi kuuliza maswali bungeni au hata kumbana waziri fulani. Alikataa bungeni kama mahali pa kufanyia biashara, kukutana na washirika mbalimbali, kukubaliana madili ya hapa na pale na hatimaye alipochoka aliweka manyanga chini na kulaani "siasa uchwara" za majitaka.


Lakini wakati wote huo alikuwepo mwana Igunga ambaye angeweza kutoa changamoto kwa Rostam na kuonesha uzalendo wa kupigania wananchi wake kwelikweli. Tangu mwaka 1994 mwana Igunga huyo alijionesha kuwa anata nia ya kuwatumia wananchi wa Igunga. Aliionesha nia hiyo hadi mwaka 2010 lakini mara zote hizo alikubali kukaa pembeni na kimya mbele ya RA. Huyu si mwingine bali ni Dk. Dalaly Kafumu. Dk. Kafumu alikubali kukaa pembeni – japo kwa manung'uniko – kumpisha RA. Hajawahi kusimama na kuwahimiza wananchi wake kumkataa RA kwa sababu ya mambo ambayo yalikuwa yanaendelea kitaifa. Aliamua kula njama ya ukimya akifurahia nafasi yake kwenye vyeo vya juu akiwa ni Kamishna wa Madini nchini.


Kama kweli Kafumu alikuwa na nia ya kupigania masilahi ya watu wa Igunga angeweza kabisa kujitoa CCM na kusimama dhidi ya Rostam. Hakufanya hivyo. Kafumu angeweza kusema kuwa RA hajawa kichocheo cha maendeleo Igunga na amekuwa tatizo kwa taifa. Kwamba kuhusishwa kwake kwa kashfa mbalimbali kulikuwa kunaletea CCM sifa mbaya. Hakufanya hivyo. Kwanini? Kwa sababu wote wako chama kimoja na masilahi yao yamefungamana na yale ya chama.


Ndiyo maana hadi leo Kafumu hajasimama kuzungumzia vita dhidi ya ufisadi au msimamo wake kuhusu wahusika wa kashfa za madini. Hajasimama kuonesha yuko upande upi katika vita ya magamba ndani ya chama chake. Na badala yake yeye kama baadhi ya viongozi wa CCM wameamua kuchukua ukimya ule ule ili wasijulikane wako upande gani. Kafumu aliamua kuipenda CCM na kazi yake zaidi kuliko kuwapigania wananchi wa Igunga. Kwa maneno mengine kama RA asingeamua kujiuzulu baada ya kuzidiwa na shinikizo la kisiasa Kafumu angeendelea kula bata kwenye ofisi yake huku akisubiri mwaka 2015 au 2020. Kweli huyu ni kiongozi ambaye Igunga wanamtaka?

Ndipo hapa basi wananchi wa Igunga wanapaswa kutambua. Kufanya kosa (mwaka 1994) si kosa. Kurudia kosa (1995) ni kosa, kulirudia kosa tena (2000) ni kosa kubwa.


Lakini kulirudia kosa kubwa (2005, 2010) si kosa tena ni uzembe wa kufikiria. Iweje mtu analima kwa mtindo ule ule, na shamba lile lile na mavuno yanazidi kupungua na yeye anaendelea kulima vile vile akitarajia labda mambo yatabadilika? Kama nyumba imeanza kuwa na nyufa mwenye nyumba akiendelea kupiga magoti kuwa nyufa zisitokee ukuta ukianguka atalalamika kuwa "sala" zake hazikusikilizwa? Wananchi wa Igunga wanahitaji malaika gani atoke ahera madukani kuja kuwaambia kuwa wamefanya makosa vya kutosha?


Lakini kinachonisumbua miye zaidi ni kuwa hivi wanapopiga kura hawajui matokeo yake kwa taifa? Hivi hadi leo hii wapo watu ambao wanafikiria kupiga kura ya mbunge ni swala la mahali tu? Wapo watu wanaotaka wananchi wa Igunga wapige kura kwa kuangalia masilahi ya Igunga peke yake. Haya ni makosa. Maamuzi ya Igunga yanaathari kubwa sana kwa taifa kama wakichagua vibaya.


Tayari tunaona maamuzi yao yalivyogusa taifa kwa miaka hii karibu 18. Uamuzi wa wana Igunga utagusa taifa kwa namna nyingine tena.
Ni kwa sababu hiyo naamini kuwa wananchi wa Igunga wamepewa nafasi ya pekee ya kusahihisha makosa yao. Nafasi ya kutakafakari na kutambua kuwa ni maamuzi yao ndio ambayo yamechangia sana kuleta matatizo ya kisiasa nchini. Wazee, kina mama na vijana wa Igunga ambao walishabikia ubunge wa RA na ambao pasipo haya wala hisia ya hatia waling'ata alipowaambia anajiuzulu ndio hawa ambao waliweza kufurahia kidogo lakini kwa gharama kubwa sana kwa taifa.


Yawezekana kabisa kama wananchi wa Igunga wangechagua kwa umakini na kwa usahihi mwaka 1994 yawezekana kabisa kashfa za Richmond, EPA na Dowans zisingetikisa taifa hivi. Yawezekana kabisa kama wananchi wa Igunga wangefanya uchaguzi sahihi yawezekana hata utawala mzima uliopo madarakani sasa hivi usingekuwepo. Hivyo nafasi hii ni ya kihistoria kwa wana Igunga. Ni nafasi ambayo inahoji kama wametambua thamani yao na thamani ya utu wao. Ni nafasi ambayo inahoji kama wako tayari kufanya maamuzi ambayo matokeo yake wanayatarajia. Kwamba, wako tayari kuamua kubadilisha mwelekeo wa jimbo lao na mwelekeo wa Tanzania kwa kumchagua mgombea ambaye chama chake kinawakilisha mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini.


Je, wanajua kuwa wanaposhika lile karatasi la kura ni kwamba wameushika utu wao mkononi mwao? Je, wanajua kuwa mpiga kura anaposhika karatasi ya kura ameshikilia njozi zake, matamanio yake, maisha ya watoto wake na taifa lake kwenye vidole vyake? Je, anajua anapopiga kura hiyo anapigia kura hatima ya maisha yake?


Hivyo, siku ya Jumapili wananchi wa Igunga watakuwa wamepewa nafasi ya kuamua wanataka kufanya nini na utu wao. Wanaweza kuamua kuendelea na watu kutoka chama kile kile, chenye sera zile zile zilizoshindwa au wakaamua kuwa sehemu ya mabadiliko na hivyo kuweka historia ya aina yake mkoani Tabora ambako tangu zamani sana kilikuwa kiini cha fikra za mabadiliko. Wananchi wa Igunga watapewa nafasi ya kuamua wanataka kuuza utu wao kwa sababu wametishwa, kwa sababu wanaogopa au wako tayari kupigia kura yao kwa gharama yoyote ile?


Njia pekee ni kuwa wananchi wa Igunga wanaitwa na historia kujitokeza mwa maelfu yao kupigia kura maisha yao. Wanaitwa kama ni malaika toka Mbinguni wajitokeze bila kujali kejeli, bila kujali maneno, bila hata kujali polisi na mitutu yao kuamua kutumia haki pekee ya uhuru wao ya kuamua kiongozi wanayemtaka. Wananchi wa Igunga wanaitwa kutokukaa nyumbani na kuombea wengine "wawachagulie" kiongozi wao. Ni witu mtakatifu, wito wa utu wao.


Hivyo, kwetu sisi wengine tunawaita kuwa sehemu ya mabadiliko. Wafanye uamuzi ambao unaendana na matamanio ya wananchi wenzao. Lakini bado wana uhuru ule ule. Wakiamua wanaweza kurudia kosa lile lile mara ya tano! Hakuna tofauti kati ya Rostam na Kafumu. Hakuna. Wote wamelelewa na mfumo ule ule na mitazamo yao kuhusu Tanzania ni ile ile. Lakini wananchi wa Igunga wanaweza kabisa kuamua kurudia kosa hilo hilo, sisi tutawalaumu lakini hatuna jinsi bali kuheshimu uamuzi wao wa makosa.


Lakini wakiamua kubadilika na kutuma ujumbe usio na utata kwa watawala kuwa Igunga ya sasa si ya 1994 au ya 2005 basi watakuwa wametuma ujumbe ambao unaweza hata kukisaidia CCM katika jitihada zake za kujivua gamba. Wakitumia haki hii kukataa geresha, vitisho, udini, na siasa za dharau wanaweza kujikuta wamefungua ukurasa mpya katika historia yao.


Na wakisahihisha makosa yao hayo ambayo yameligharibu taifa hivi, na sisi wengine tutawasemehe. Wajitokeze kupiga kura, walinde kura zao zote zihesabiwe na wafurahie ushindi na kuwa tayari kuanza ngwe mpya ya siasa Igunga.


Naomba nijisahihishe mimi mwenyewe kwanza. Nimesema kwa kirefu kuhusu "wananchi wa Igunga" na kuwa "wapiga kura wa Igunga" wasahihishe makosa yao. Ukweli ni kuwa watu pekee wanaotakiwa kusahihisha makosa haya ni wana CCM na mashabiki wa CCM waliompigia kura mgombea wa CCM na kuliletea matatizo taifa kwa karibu miaka 18. Hawa wajisahihishe na hapo ndio tutafikiria kuwasamehe.


Kila la heri!

Article inakosa mfuto kwa kupersonalize issue ya ufisadi arround one person "ROSTAM" na kusahau role played by other key participants Lowassa, etc..

You are always at very front attacking personalities of certain group of citizen in Tanzania..

Hatuna sababu ya kukuamini kwamba unaendeleza fikra zako za kijumuiya hapa pia...
 
Article inakosa mfuto kwa kupersonalize issue ya ufisadi arround one person "ROSTAM" na kusahau role played by other key participants Lowassa, etc..

You are always at very front attacking personalities of certain group of citizen in Tanzania..

Hatuna sababu ya kukuamini kwamba unaendeleza fikra zako za kijumuiya hapa pia...
Nilitegemea baada ya comment yako utachangia chochote.
 
Nilitegemea baada ya comment yako utachangia chochote.

Nichangie nini wakati issue ya ufisadi in fact si ufisadi hasa unaolengwa ila personalities of certain group of citizen...

Wananchi wana haki ya kumchagua yeyote tu lakini ...si kwasbabu ana nia ya kupambana na ufisadi..hoax

wapiganaji wenyewe kina (Sitta, Mwakyembe, Mwanakijiji ect) kimya baada ya doawans kuuziwa mmerakani..

So the fight was about certain group of citizen period..lakini mkiliwa na mzungu poa tu..
 
......

wapiganaji wenyewe kina ( J M Kikwete ,Sitta, Mwakyembe, Mwanakijiji ect) kimya baada ya doawans kuuziwa mmerakani..

Nimemuongeza Rais wetu JK kama mpiganaji number moja wa ufisadi sabau so far Liyumba, Mramba, Yona wana kesi za kujibu.

Je

  • Hizo ndizo "personalities" na certain group of citzen wanaolengwa kwa ufisaidi wa tanzania?
  • Personality gani ya Kitanzania aliyonayo RA tofauti na hao wengine wachache nlitaja hapo juu kumfanya asitakiwe kusemwa au kuwa criticized?
  • Kwa nini kutajwa kwa RA iwe mwiba kwako?
Ebu fafanua
 
Kwa mtazamo wangu kuna mambo mengi yanayoathiri siasa za Tanzania. La kwanza kabisa siasa za Tanzania hazijakaa katika mwelekeo wa kuwapa wapiga kura usahihi wa amchague nani na kwa sababu gani. Nachukulia mifano ya nchi nyingine ambazo makundi siasa ya nchi hizo yanaeleweka kiuchumi (nichague mjamaa au mbepari?), kiutamaduni (nichague mhafidhina au mliberali?), kidini (nichague mkatoliki au mprotestanti?). Na ndio maana kwa kesi ya Igunga ilikuwa rahisi sana kwa Rostam kukaa pale muda mrefu. Watu wa Igunga hawakuwa na sababu ya kumkataa kwa sababu hawana dira ya wanataka wafike wapi na Rostam atawafikishaje pale. Na kwa vile Rostam ni tajiri aliweza kuwapofusha watu wa Igunga kwa kuwatuliza kinamna pale watu fulani fulani walipomwendea na kumpigia magoti (siasa za kifalme) wakimwomba awape hiki na hiki (maskini ataomba nini kama si unga na mchele wa siku moja?).

La pili mimi naona kama siasa za Tanzania kwa ujumla wa nchi na kimajimbo hazitabiriki kwa sasa na zinabadilika kievolution (mabadiliko ya pole pole kadiri muda unavyosonga kutegemea na watu husika na kwa sababu tofauti). Kwa mfano siasa za bukoba ni tofauti na siasa za iringa. Siasa za ubungo ni tofauti na ilala. Ili ni jambo ambalo linanishangaza hata mimi, na nitawaachia watu wa political science wafanye uchambuzi wao wanafahamu kuliko mimi. Lakini component ya dini huwezi kuipuuza. Waislam wanapenda sana block vote na sehemu zenye waislamu wengi usitegemee kupata kura nyingi kama ukipuuza matakwa yao.

Yapo mambo mengine pia kama hela za chama au mgombea husika, elimu ya wapiga kura eneo husika, historia ya mgombea kwenye jimbo hilo, akili na charisma ya mgombea (hii inaeleza ubunge wa watu kama Lissu, Zitto, Mnyika, Kafulila, ingawa hawakuwa matajiri na wanatoka vyama vya upinzani; naweza pia kusema kwamba kati ya mtaji wa Chadema kisiasa ni kuvutia vijana wenye charisma), vyote hivyo vinaelezea kwamba siasa za Tanzania sio monolithic, hazitabiriki, lakini zinatoa matumaini kwamba huko mbele chama lege lege haikitakuwa na nafasi kwenye mioyo ya watanzania walio wengi.
 
Ni kweli kujisahihisha kwao ndiko kutasababisha watu kuwasamehe,lakini yawezekana wakaamuwa kujisahihisha kwa kumchagua tena mgombea wa Ccm wakifikiri kuwa huyu si RA ni sura nyingine kabisa,Je katika masahihisho kama hayo wataweza kusamehewa?

tatizo nilionalo Igunga kwa sasa kuwa kutakuwa na mgawanyo wa Kura na hicho ndicho kitacho wapa ushindi wana magamba kama hivi vyama vingeweza kuunganisha nguvu basi magamba wangekuwa mashakani sana

lakini acha tusubiri tarehe husika ndio utakuwa mwanzo wa msamaha ama la

wakichagu ccm hatutawasamehe kamwe kwani watakuwa wameonyesha kiburi kikubwa sana
 
Back
Top Bottom