Ihefu Sport Club yaingia ligi kuu Tanzania

Hasa wakicheza na mabingwa wa ngao ya jamii, mabingwa wa Nchi na mabingwa wa FA Simba Sports Club
 
Hili Jina Ihefu Iwapo Sijakosea Linatokana Na Ardhi Chepechepe Kuanzia Hilo Eneo La Mbalari
Ahsante... Naomba nisaidie kwa ufasaha historia kamili ya club na jina pia....
 
Mbao imeniuma kama ilivyoniuma Stand united kipindi kile.
 
Ningependa kujua maana ya hilo jina Ihefu na historia ya hii club. Itapendeza sn sn
Timu ya waburushi wa Mbarali,walinunua timu iliyokuwa ikiitwa Wenda FC ya Mbalizi ikiwa daraja la pili kisha wakabadili jina na kuiita Ihefu.

Wakapigana kupanda mpaka daraja la kwanza na sasa ligi kuu.

Wanaojua zaidi watajazia..asante.
 
Timu ya waburushi wa Mbalali,walinunua timu iliyokuwa ikiitwa Wenda FC ya Mbalizi ikiwa daraja la pili kisha wakabadili jina na kuiita Ihefu.

Wakapigana kupanda mpaka daraja la kwanza na sasa ligi kuu.

Wanaojua zaidi watajazia..asante.
Ahsante mkuu kwa summary.... wenda fc nilikua naijua. Inamaana waliponunua ikaendelea kuwa mbarali kwa maana ya mbeya mjini au ilihamishiwa Mbarali mpaka inapopanda Daraja sasa?
 
nmekumbuka sana ni kweli
 
na kingne napenda kujuaaa inamaana kwa sasa wenda fc haiwez kuwepo kama ikianzishwa upyaa
 
Ahsante mkuu kwa summary.... wenda fc nilikua naijua. Inamaana waliponunua ikaendelea kuwa mbarali kwa maana ya mbeya mjini au ilihamishiwa Mbarali mpaka inapopanda Daraja sasa?
Ilihamishiwa Mbarali toka iliponunuliwa mkuu,kumbuka Mbarali sio Mbeya Mjini bali wilaya inayojitegema ikiwa mkoani Mbeya na makao yake makuu ni Rujewa.

Mapambano yote yamefanyikia huko huko kwa walima mpunga.
 
Ilihamishiwa Mbarali toka iliponunuliwa mkuu,kumbuka Mbalali sio Mbeya Mjini bali wilaya inayojitegema ikiwa mkoani Mbeya na makao yake makuu ni Rujewa.

Mapambano yote yamefanyikia huko huko kwa walima mpunga.
Hii ihefu ina uhusiano gani na Masanja? Ni mmoja wa wawekezaji?
 
Yaani kwa nn ihame prison na sio timu nyingine hapo ndo cjaelewa
Tanzania Prisons ni timu ya jeshi la magereza na jeshi la magereza lipo tz nzima sasa pale mbeya sasahivi wana timu tatu ligi kuu ndio maana nikasema kwanini wahame
 
Ahsante... Naomba nisaidie kwa ufasaha historia kamili ya club na jina pia....
Mkuu
Kwakifupi Historia Yake Siijui, Ila Wajuzi Wanakuja Kukujuza Muda Siyo Mrefu Sana
 
Tanzania Prisons ni timu ya jeshi la magereza na jeshi la magereza lipo tz nzima sasa pale mbeya sasahivi wana timu tatu ligi kuu ndio maana nikasema kwanini wahame
Sawa mkuu watakua wamekusikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…