Ijue 40 anayofanyiwa marehemu

Ijue 40 anayofanyiwa marehemu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Wengi huwa aidha tumewahi kuandaa shughuli ya 40, kwa marehemu wetu au tumewahi kushiriki ufanyikaji wa 40, kwa majirani au rafiki zatu katika kumaliza msiba!

Shughuli hii imekuwa ikifanyika sana na dini zote mbili kwa maana waisilam na Wakristo pia.

Ipo hivi:

Watu wengi wamekuwa wakifanya lakini ukiwauliza wanafanya 40 kwa ajili ya nini,hawajui, hata ukiwauliza kwa nini 40, pia hawajui.

Imani ya kufanya 40 haijanza jana wala majuzi tokea mababu kwa mababu huko nyuma, ni imani ambayo kiukweli sio hasa ya kidini bali inafungamana na mila za Kiafrika.

Kufanya 40, kumekuja kutokana na imani kuwa MTU akifa, roho hupelekwa mbinguni kwa Muumbaji wake ambae ndie mmiliki, mwili huzikwa na huko huteketea kwa kuoza, ila nafsi ambayo ndio kivuli hubakia ulimwenguni ikizagaa zagaa. Kivuli hicho huendelea kubakia maeneo ambapo kilikuwa kinaishi kwa muda wa siku 40 ndipo kinaondoka na kwenda kuungana na wafu/vinvuli vyenzie kwa utaratibu ambao Mungu kauweka au tuseme ukoo wenu umeweka.

Kufanya 40, ni kumuwaga marehemu kuwa sasa kaondoka kweli kweli na ameanza maisha mapya aendako. Hili lina kama ukweli sababu mtoto mdogo akifiwa na mama yake au baba ake huendelea kumwona na huwa akilia sana sababu anamwona na hapo ndio maana wazee wetu walikuwa wana mfunga kauzi ka sanda mkononi ili kuondoa ile hali ya kumwona mama au baba ake alie fariki!

Vivuli ivo vikikusanyika sehemu fulani ndipo hutengeneza kitu kinaitwa mizimu! Hivo Basi mizimu ni nafsi au vinvuli vya mababu zetu waliokufa zamani.
 
Ni kweli.

Ila tu ni kwamba iyo safari siyo ya kuungana na mizimu hapana ni safari ya kuungana na Roho nyinginezo au niseme ni back to the source, original home, to the all souls to God.

Matanga ni baada ya Mwili kuoza.

Total disconnection.
 
Asili ya aroibani imetoka misri, kule kulikuwa na sheria ya kiongozi au mfalme akiafa ikifika cku ya 40 hufanyiwa mila fulani za kwo sasa mwisho wa cku ndio nasi tukaanza kufanya hivyo.
Kwa nini wasubiri siku 40 na siyo pungufu au zaidi?

Maana naona ni kama unapingana na mleta uzi kwa sababu alizozitoa!
 
Miye nilijua kichwa ile mifupa inajiachia, kila sehemu inaachia
 
Back
Top Bottom