Ijue 40 anayofanyiwa marehemu

Ijue 40 anayofanyiwa marehemu

Wengi huwa aidha tumewahi kuandaa shughuli ya 40, kwa marehemu wetu au tumewahi kushiriki ufanyikaji wa 40, kwa majirani au rafiki zatu katika kumaliza msiba!

Shughuli hii imekuwa ikifanyika sana na dini zote mbili kwa maana waisilam na Wakristo pia.

Ipo hivi:

Watu wengi wamekuwa wakifanya lakini ukiwauliza wanafanya 40 kwa ajili ya nini,hawajui, hata ukiwauliza kwa nini 40, pia hawajui.

Imani ya kufanya 40 haijanza jana wala majuzi tokea mababu kwa mababu huko nyuma, ni imani ambayo kiukweli sio hasa ya kidini bali inafungamana na mila za Kiafrika.

Kufanya 40, kumekuja kutokana na imani kuwa MTU akifa, roho hupelekwa mbinguni kwa Muumbaji wake ambae ndie mmiliki, mwili huzikwa na huko huteketea kwa kuoza, ila nafsi ambayo ndio kivuli hubakia ulimwenguni ikizagaa zagaa. Kivuli hicho huendelea kubakia maeneo ambapo kilikuwa kinaishi kwa muda wa siku 40 ndipo kinaondoka na kwenda kuungana na wafu/vinvuli vyenzie kwa utaratibu ambao Mungu kauweka au tuseme ukoo wenu umeweka.

Kufanya 40, ni kumuwaga marehemu kuwa sasa kaondoka kweli kweli na ameanza maisha mapya aendako. Hili lina kama ukweli sababu mtoto mdogo akifiwa na mama yake au baba ake huendelea kumwona na huwa akilia sana sababu anamwona na hapo ndio maana wazee wetu walikuwa wana mfunga kauzi ka sanda mkononi ili kuondoa ile hali ya kumwona mama au baba ake alie fariki!

Vivuli ivo vikikusanyika sehemu fulani ndipo hutengeneza kitu kinaitwa mizimu! Hivo Basi mizimu ni nafsi au vinvuli vya mababu zetu waliokufa zamani.
Sio kweli. Mizimu ni roho za mashetani zenye kuvaa sura ya watu ambayo wazee wao walikuwa wanayaabudu na kuyatolea sadaka. Hupata uhalali baada ya wazee wa hizo koo kuweka maagano either kwa maneno au sadaka na kujinasua ni kuyatengua na kutafuta maagano yao kwa jina la YESU na kwa damu ya Yesu pekee. In short tu, roho humrudia muumba aliyeitoa na mwili utarudi mavumbini wala haibaki siku 40 so hizo arobaini ni sawa na Ibada za wafu kwa mashetani.
 
Ndio hiyo hiyo 40 ,siri nayo ni nini? wew ulisema 40 ni kwenye kifo tu ndio maana nikauliza kwenye watoto kuzaliwa mbona na wao wana hiyo 40 ya kutolewa nje?
Tulipishana kidogo mkuu, sio kwamba nilisema 40 ipo kwenye kifo tu isipokuwa niliegemea hapo kwa kina.

Mwizi akikamatwa tunasema za mwizi ni 40

Wazungu wana msemo wao wanasema life starts at 40 nk
 
Sio kweli. Mizimu ni roho za mashetani zenye kuvaa sura ya watu ambayo wazee wao walikuwa wanayaabudu na kuyatolea sadaka. Hupata uhalali baada ya wazee wa hizo koo kuweka maagano either kwa maneno au sadaka na kujinasua ni kuyatengua na kutafuta maagano yao kwa jina la YESU na kwa damu ya Yesu pekee. In short tu, roho humrudia muumba aliyeitoa na mwili utarudi mavumbini wala haibaki siku 40 so hizo arobaini ni sawa na Ibada za wafu kwa mashetani.
imani yako nzuri sana na nimeipenda. Mwalimu wako wa dini aliyekufundisha sunday school aliifanya vyema kazi yake. Je watakatifu na mitume wa dini za kikristo, kiislamu, kibudha na kihindu ni akina nani hao?
 
Back
Top Bottom