Ijue bahari: Baharini kuna misitu mikubwa yenye miti mikubwa ya kutosha kuchana mbao kama utazamia

Ijue bahari: Baharini kuna misitu mikubwa yenye miti mikubwa ya kutosha kuchana mbao kama utazamia

Hivi mneri hauoti baharini, unaeza ukawa na chumvi chumvi na stimu ya kwenda 😋🤔🤔
 
Kuna kitu wenzetu huko majuu wanaita drain the ocean, kama una Dstv kuna program huwa wanaonyesha kwenye National Geographical Channel. Hii ni tekonolojia ya kisasa kabisa ambapo kwa kutumia computer program wanauwezo sasa hivi kuona kila kitu kilivyo huko chini baharini. Mfano kupitia hiyo program wameweza kujua meli kubwa au nyambizi ambazo zilipotea baharini kwenye vita kuu ya dunia ziko wapi. Sijawahi kuona hiyo miti unayosema ila nimeona makorongo makubwa, matumbawe nk
Well said... huwa napata tabu sana kuona tuna smartphones, channel nyingi za sayansi kwenye tv lakini bado tunakosa maarifa ya kawaida. Ni rahisi sana ku prove kila taarifa unayopokea kama ni sahihi ama Laa! Kama mtu anaambiwa baharini kuna miti, ya nini kukataa ama kukubali bila kujihakikishia! Kwa maelezo uliyotoa yanatoa taswira kwamba kuna wanao amini titanic iligonga mwamba wa jiwe! Kuna wengine mpaka Leo wanadhani ile filamu ya (Jesus) wanafikiri Brian Deacon ni Yesu halisi, mbaya zaidi wengine ni wasomi kabisa.
 
Na pilipili! Ipo hivi chief, huyu ndugu yetu possibly alipanda katika zile boat zenye sakafu yenye kioo maalumu kwa ajili ya kuangalia vilivyomo katika maji mafupi ya bahari ila si kuzama chini ya bahari. Hizo boat zinapatikana sana hapa bongo mfano ukienda Ruvula (msimbati) kule Maingilio ya mto Ruvuma zipo na nmebahatika kusafiri nayo, mafia nadhani ipo pia. Kinachoonekana ni majani/ maua mazuri jamii ya magugu, samaki na viumbe wengine ambao wanapatikana katika kina kifupi cha bahari kuelekea pwani ( continental shelf). Ila habari ya Hiyo misitu daah, anyway najua vichache tuache wajuvi waendelee kusema

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom