Ijue BMW x5 automatic Diesel

Ijue BMW x5 automatic Diesel

Cruise auto spare ni wauzaji wa spear party za magari
Jeep,
BMW,
Audi,
Land rover,
Porsche,
Volkswagen,
Chrysler,
Range/Land rover

Duka linapatikana MAKAO MAPYA,EDEN ROAD jirani na cafe laziz restaurant,Arusha

Kwa mawasiliano piga +255743805465,+255786050747
Email:cruisespares@gmail.com
Fb&IG:cruiseautospareparts

Pia usisite kuwasiliana nasi pia tunatoa ushauri.
 
IJUE BMW X5 AUTOMATIC DIESEL

Na Kimomwe Motors (T) Ltd- Waagizaji Magari

UTANGULIZI

Model inayoongelewa hapa ni toleo la mwaka 2000 mpaka 2007

Kwa wakati huo iliaminika kwamba gari ya SUV tamu zaidi ni Mercedes Benz M Class na Range Rover😊, lakini ukweli ni kua baada ya X5 kuingia sokoni ilifanya gari hizo zionekana za kawaida kwenye mwonekano unaovutia ndani na nje, starehe (luxurious), na hata kupanda kwake juu kuliko washindani wake hao.

Injini na Mafuta

Injini inayoongelewa leo ni inayotumia Diesel ambayo ina Cylinder 6 yenye Cc 3000. Japo ipo ya Diesel nyingine yenye Cylinder 8.

Injini hiyo ya 3.0L ina uwezo wa kwenda mpaka Km 11 kwa lita moja ya mafuta.

Utulivu na uimara

Gari hii ina speed 240 na katika barabara kuu inaelezewa kuweza kwenda Mpaka Km 240 bila kuyumba sababu ya uzito wa bodi yake upatao tani 2.1 na tairi zake za nyuma kuchanua hivyo kuipa utulivu gari iwapo katika mwendo

Katika vumbi au matuta gari hii huwapa utulivu abiria kwa kua chini imeundwa kwa booster (air suspension) ambazo hupunguza mtikisiko kwa kiasi kikubwa.

Vifaa

Vifaa kwa sasa vinapatika zaidi Dar es Salaam kwa gharama za juu kiasi chini ya vifaa vya Volkswagen Touarage. Uzuri ni kwamba vinadumu kwa mda mrefu.

Nyongeza

Radio Frequency za gari hii ni mpaka 107fm tofauti na gari nyingine zinazoishia 90fm

Pia gari hii viti vyake vya mbele ni vya mfumo wa umeme, dashboard yenye nakshi ya mbao mbao ikiwa na screen, Viti vya ngozi ngumu, baadhi zina Sunroof, Parking Sensors 6 badala ya 4, Airbags 6 badala ya 2.

Maoni na Ushauri

Kama unafikiria kupata SUV yenye ubora na uwezo wa juu hii ni moja wapo ya gari bora sana haswa kama utapata inayotumia.

Gharama

Kwa kuagiza gari hii inayotumia Diesel hughar kati ya 30m mpaka 34m kutegemea na mwaka na inavyouzwa huko nje.

Kama utataka ya Petrol itagharim kati ya 24.5m mpaka 27m

View attachment 1808154View attachment 1808156View attachment 1808157View attachment 1808158View attachment 1808159View attachment 1808160View attachment 1808161
Hii gari ilimpiga jamaa yangu mmoja mwanasheria alichezea makofi mpaka akaliuza fasta kwa hasara
 
Nyingi tu. Mfano mzuri ABS sensor.
Sio vizuri kupiga uongo mkuu hizi sensor za mabreki bei chee sana kwa gari zote European na Japanese. Urongo huwa sio uungwana.
Screenshot_20220228-180000_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom