Ijue deed poll (nyaraka inayotumika kubadilisha jina la mtu)

Vyetu vya shule havibadilishwagi
Naomba kujzwa madhara ya kubadili jina, je? kama vyeti havibadilishwi mchakato unakuaje ukitaka kutumia vyeti na ss vitakuwa na jina lako la zaman?
 
Naomba kujzwa madhara ya kubadili jina, je? kama vyeti havibadilishwi mchakato unakuaje ukitaka kutumia vyeti na ss vitakuwa na jina lako la zaman?
Wakati unabadilisha jina unaomba copy kadhaa, ukiwa una apply unapeleka na copy ya kubadilisha jina.
 
Wakati unabadilisha jina unaomba copy kadhaa, ukiwa una apply unapeleka na copy ya kubadilisha jina.
ok mkuu ila hujaniambia kama kuna madhara yyt ya kubadilisha jina ,vyeti vp vinabadilika?
 
ok mkuu ila hujaniambia kama kuna madhara yyt ya kubadilisha jina ,vyeti vp vinabadilika?
Sidhani kama unaweza badilisha jina kwenye vyeti. Kinachotokea, unapewa document inayoitwa Deed Poll ambayo inaonyesha jina la mwanzo na jipya, pamoja na picha yako.

Kwa hiyo vyeti vinabaki, madhara nadhani ni kulingana na sababu unayobadilisha jina ila vitu kama passport, vitambulisho itabidi kubadilisha pia.

Vyeti vya shule hubadilishi, ina maana, kila unapotuma maombi ya kazi uta attach Deed Poll pia.

Mimi nimebadilisha mwezi wa 11. Jina langu la passport (maana nilipata passport nikiwa mdogo) ni tofauti na jina la kwenye vyeti, na pia jina lililopo kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na ninalotumia la ubatizo.
 
Gharama ziko vp mkuu naomba kujuzwa.
 
Gharama ziko vp mkuu naomba kujuzwa.
Utahitaji document ambayo ndo Deed Poll kutoka kwa mwanasheria, ambayo inagharamu si zaidi ya elfu 50, then inatakiwa iwe filled wizara za ardhi ambapo ndo kuna ofisi ya kubadilisha jina.

Wao wana charge elfu 32,500 kwa copy 3
 
Hivi kwa usahihi majina ya ukoo/Surname yanatakiwa yakae wapi wakati wa kuandika jina,Kuna ofisi zingine wanakuambia like mwisho wakati wa kuandika majina,Ofisi zingine wanalitaka likae mwanzo na kuna ofisi nilienda wakataka likae katikati ,Je usahihi ni upi hapo?
mfano unaitwa
Bagia Karimati Sambusa
Bagia jina lako ,Karimati la baba na Sambusa la ukoo
Sambusa kama jina la ukoo ofisi zingine zinataka uwandike kama ifuatavyo:-


1.Bagia Karimati Sambusa
2.Sambusa,Bagia Karimbati
3.Bagia Sambusa Karimati
hapo wapi sahihi?
 

Kwa usahihi ni kutokana na ulivyoulizwa na taasisi husika.jitahidi tu kufuata maelekezo
 
Kwa mfano nataka kutumia majina mawili kwenye kuomba passport je inaruhusiwa mkuu?
 
Ninayo hiyo huko kote nimeenda nashangaa nssf wamenikatalia nimeenda hapo ilala boma wakanikatalia wanasema nibadilishe kwenye vitambulisho chao vifanane na kwenye vyeti ndio ninapotaka kujua zaid kisheria imekaa sawa hiyo 🙏
 
hivi ni waraka au nyaraka?
Kwa nini mnatumia kiswahili khovyo khovyo mkuu.
Nyaraka ni wingi, waraka ni mmoja. Sasa inategemea hizo karatasi zinakuwa ngapi. Kama karatasi zinakuwa zaidi ya Moja ni sahihi kuita nyaraka. Ni kweli Kuna watu wanafanya makosa sana, mtu ametoa wimbo 1. Anasema nimetoa nyimbo. Wengine utasikia nachagua nyimbo ya Rozy muhando; Secret agenda uwe dedication kwa Bunge letu tukufu.
 
Nchi gani hiyo?
 
Ilikuchukua muda gani kulifanikisha hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…