Ijue Epoxy Metallic floor, style ya kisasa ya floor!

Safi sana mkuu...kwa hapa bongo kuna kampuni tatu zinauza epoxy floor nabaki africa, sika na wazungu flani wapo mikocheni...tatizo hizi zao ni plain hazina urembo wowote,kwa kuongezea zinakua in a kit..hardener,color pack,base and powder..bei nadhani inakua kwenye laki 3 na kitu kwa kit moja na inapiga 7.5 sm
 
Ni Kweli mkuu! Na hii unaweza Ku apply hata kwenye floor ya Cement ya siku nyingi, muhimu Ni kuziba nyufa na matundu yote kabla ya Ku apply primer!
Shida ni uchanganyaji wa hizo rangi na umwagaji wake,kama hujui zinabanduka kama yale mabati ya ''Tunakopesha''
 
Hongera mkuu kwa kutujuza hayo maujanja ila mi niulize, ivi km utatengeneza kitchen countertop y floor na ukaipaka hizo rangi vipi itadumu kutokana na maji na joto o moto pale jikoni (majiko yatakuwa ni ya gesi na umeme tu)?, coz ctamani kuweka tiles jikoni.​
 
Mkuu serio nimepata Oda nyingi za kutosha, kwa sasa nimesafiri nje ya nchi.....ukiacha kilichonileta huku nafanya maongezi na Viwanda vinavyotengeza hii Epoxy angalau niwe Agent wao Tanzania, itapunguza gharama za kuagiza Materials nje!
 
Shida ni uchanganyaji wa hizo rangi na umwagaji wake,kama hujui zinabanduka kama yale mabati ya ''Tunakopesha''
Mkuu issue si uchanganyaji wa rangi au umwagaji....muhimu kwanza ni kuhakikisha floor ni kavu na haina Oil, Au Grisi.....kama floor Ina hivyo vitu hata umwage kwa utaalam wa aina gani, hata uchanganye kwa utaalamu wa aina gani haitakupa matokeo mazuri, then floor ikiwa kavu bila mafuta unapiga msasa kuondoa tabaka flani la juu, baadaye unapiga Primer, ukipiga Primer it means umetengeneza uhusiano Kati ya floor na kitu unachotaka kuweka....then unaendelea na process zingine.....
Kumbuka hizi rangi sio kama rangi za nyumba ulizozoea kuona, hizi rangi ni High powerful paint, na ni very strong, ikishaganda hapo ni zaidi ya Cement.....thats why nikasema kabla kuwa lazima floor iwe strong enough ili Ku apply hii Epoxy, kama floor yako inaweza kutobolewa na Sisimizi au mchwa then ukasema eti u apply Epoxy....baada ya muda kwa ile Power ambayo Epoxy iko nayo, itabandua hiyo floor!
 
Asante Mkuu! Kwanza Epoxy unaweza Ku apply Iwe kweenye floor ya Cement, Ukutani, kwenye floor ya Mbao, na hata kwenye Mable ama Tiles, zipo Epoxy ambazo ni transparent so zitatengeneza mng'ao na effect tofauti utazoweka zitaleta kitu tofauti bila kuaribu mmwonekano wa mwanzo wa Mbao, Mable na vitu ka hivyo, kingine ni kuwa Epoxy unaweza Ku apply mazingira yoyote Yale, Subbureni, Gereji, Chumbani, Viwanja vya michezo hasa Volleyball na Basketball n.k......kuhusu kumudu mazingira ya Joto jikoni ni kwamba, Unaponunua Epoxy lazima ujue ni wapi unaenda kupaka, coz Epoxy zimetengenezwa tofauti ili kuweza kuhimili mazingira yote, Baridi kali, joto n.k.....so zipo Epoxy Special kwa Ku apply sehemu kama jikoni......na Kuna kiwango cha hari ya hewa ambacho Mtaalamu atahakikisha kinakuwepo ili kuapply Epoxy, baada ya hapo ije joto, ije mvua, ije baridi kali...floor yako ni salama!
 
Mkuu umefika wapi na hii kitu?
Mkuu nilisafiri nje ya nchi ndo nimerudi majuzi, Kuna Wadau ambao nilikua nawasiliana nao toka nipo Safarini so now tunataka kuanza!
 
Hao wana Epoxy resigard hp ambayo ni plain.... Hawana Metallic ambayo wateja wengi wanataka.
 
Shida ni uchanganyaji wa hizo rangi na umwagaji wake,kama hujui zinabanduka kama yale mabati ya ''Tunakopesha''
Mkuu! Kwa Epoxy kubanduka inategemea na Quality ya Cement floor yako...... Asilimia chache kutokana na ujuzi mdogo wa Installer!
 
Nimeipenda na ningependa kuifanya hii kitu kwangu naomba tuwasiliane
 
Nimeipenda na ningependa kuifanya hii kitu kwangu naomba tuwasiliane
Ni miaka 3 sasa toka niweke hili Bandiko..... Kwa Kipindi chote hiki, nimefanya kazi nyingi sehemu tofauti kwa Watu Binafsi na kwenye Taasisi za Serikali hasa hizi Hospital mpya ambazo Zinajengwa nchi nzima zikiitwa Hospital za Magufuri.......

Angalau sasa nina uhakika wa kupata materials hapa hapa japo kipindi cha nyuma nilitegemea kupata materials kutokea Kenya ama South Africa.....

So mkuu kama bado upo interested karibu.
 
Picha za kazi zako hapa Tanzania tuone wadau
 
samahani pls call me at 0788504490
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…