Ijue historia ya Chifu Mkwawa (Sehemu ya kwanza)

Ijue historia ya Chifu Mkwawa (Sehemu ya kwanza)

Mkwawa.jpg

Mkwawa alikuwa chifu wa wahehe na kiongozi mkuu wa kabila la wahehe ambaye alizaliwa mwaka 1855 -1898 katika kijiji cha Lungemba mkoani Iringa.

Baba yake mzazi ni Mzee Munyigumba.Baada ya kuzaliwa Mkwawa alipewa jina la 'Ndasalasa' yaani ikiwa na maana ya kupapasa papasa. Alipoofikisha umri wa miaka 23 ulitokea uvamizi ambapo baba yake mzazi Mzee Munyigumba alivamiwa na Wangoni.

Baada ya kuvamiwa Mzee Munyigumba alikimbilia mlima wa Nyamulenge. Alipokuwa pale mlimani Wangoni walimzingira kila pande hivyo Mzee Munyigumba aliamua kuingia pangoni, baada ya kuingia pangoni Wangoni waliamua kuchoma moto pale pangoni ili basi Mzee Munyigumba afie ndani ya pangoni lakini mpango wao haukutimia kwani Mkwawa aliwahi kumuokoa baba yake.

Mzee Munyigumba alimsifu sana mtoto wake kwa ushujaa alioufanya wa kumkomboa hivyo alimtunuku jina la kishujaa yaani aliitwa "Mkwava Mkwavinyika".

Mapigano kati Mkwawa akiwa na wafuasi wake wa kabila la Wahehe dhidi ya Wangoni yalipamba moto sehemu ya Makambako ambapo Wangoni walishindwa na kuamua kukimbia.

Licha ya Wahehe kushinda lakini bado waliwasifu Wangoni kwa mapigano waliyoyaonesha wakisema kuwa " Leo tumekutana na Makambako" ikiwa na maana kuwa wamekutana na madume hivyo sehemu hiyo tangu siku hiyo ikawa inaitwa Makambako mpaka leo hii.

Lakini baada ya kumaliza mapigano dhidi ya Wangoni, Mkwawa na kikosi chake walirudi Iringa mjini. Kwa bahati mbaya alisikia taarifa mbaya kwamba baba yake amefariki hivyo ilibidi baba yao mdogo Mzee Mwaije agawanye nchi ambapo upande wa kusini alipewa Mkwawa na upande wa kasikazini alipewa Muhenga. Baada ya kupewa maeneo hayo Shemeji yao Mwambambe mwalinyungu ambaye asili yake ni mtu wa Tabora aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga.

Mwambambe alifika Iringa wakati akiwa Mdogo sana hivyo baba yake Mkwawa alikuwa akimtumia kwenda kuchukua dawa za kichifu na dawa za kivita wakati wakiwa njiani pale walipotokea maadui Mwambambe alikuwa na nguvu za ajabu alikuwa na uwezo wa kumkamata adui mmoja kila upande na kuwagonisha vichwa mpaka wanafariki hivyo baba yake Mkwawa pamoja na wahehe wote kiujumla walimpenda sana Mwambambe kufuatia sifa hizo Mzee Munyigumba alimpatia binti yake amuoe. Hivyo Mwambambe aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga kwa kumwambia Muhenga kwamba amepata eneo dogo kuliko Mkwawa hivyo alimwambia kuwa yeye yupo tayari kumsaidia ili apate eneo kubwa.

Wakaanzisha vita ya kumpiga Mkwawa hivyo Mkwawa alitoroka kuelekea Dodoma, wakati akiwa huko baba yake Mdogo aliyekuwa akiishi huko alimuuliza kuwa nchi kamuachia nani? Ilibidi Mkwawa amueleze kilichotokea na kumalizia kwamba amemuachia Mdogo, hapo ndipo baba yake Mdogo alipomwambia inabidi arudi Iringa kwa ajili ya kupambana kwani yule Mdogo wake pia anaweza kupigwa na Mwambambe akachukua nchi na Mwambambe asili yake ni mtu wa Tabora hivyo nchi itakuwa ya watu wa Tabora.

Basi ilibidi Mkwawa arudi Iringa kupambana na hao ndugu zake. Lakini kwa bahati mbaya hawa ndugu zake walishasababisha mauaji, walishinikiza mpaka mama yake Mkwawa alijiua. Baada ya Mkwawa kukimbilia Dodoma walimkamata mama yake na kumlazimisha awaoneshe dawa ya uchifu ambayo ilikuwa inaitwa "LIHOMEO" baada ya kuwa amelazimishwa sana mama Mkwawa aliamua kuwaambia kuwa dawa hiyo inapatikana sehemu inayoitwa Kikongoma hivyo waliondoka kuelekea huko Kikongoma kuchukua dawa. Walipofika Kikongoma walienda mpaka kwenye daraja la Mungu baada ya kufika hapo mama Mkwawa aliwaambia kuwa "Nimefika sehemu ilipo dawa lakini mashariti yake ni lazima nivue nguo ndipo niweze kuichukua hiyo dawa, sasa nyinyi ni wanangu nitavuaje nguo mbele yenu?" Hivyo wale jamaa ilibidi wawatume wamama wawili waende naye wao wenyewe walibaki nyuma kidogo.

Mama Mkwawa alisogea hadi karibu na daraja la Mungu sehemu ambapo kulikuwa na jiwe kubwa, mama mkwawa alivua nguo zake zote na kuziweka juu ya lile jiwe kisha akaanza kulizinguka lile jiwe Mara kadhaa halafu akajirusha ndani ya maji huku akisema, "Mwambambe ulitaka nikuoneshe dawa ili umuue mwanangu umenikosa". Alizungumza kwa lugha ya kihehe kisha akajirusha ndani ya ule mto.

ITAENDELEA......
Namkubali sana,ila kujiua ndio kitendo kilichonikwaza
 
Namkubali sana,ila kujiua ndio kitendo kilichonikwaza
Nilienda kalenga kama utalii wa ndani na kwa mujibu wa yule msimuliaji pale alisema alijiua kwasababu aliichukia ngoz nyeupe hivyo alitaka isimguse ndio maana akajiua. [emoji24] ndio maana walipo mkuta kafa waka mkata kichwa ili wapeleke uko kwao kuenda kuonesha mtu alie watesa na wanamkubali sana kwa mbinu zake maana ziliwatesa sana. But kichwa fuvu lilirudi na lipo kalenga pale yan jamaa alikua mchawi huyu alikua na kiti na chungu na mti nje pale
Kile kiti hukalia yeye tu mpaka leo kipo
Chungu kile kama kuna hatari hutoa damu automatic
Kama kuna neema hutoa maji ndio alikua akikitumia kujua what happens next
Mti wake ulikua ukikaa pale unapotea uo mti mpaka leo upo kalenga pale pale kwenye museum
 
Duh!...huku kwa kina mkwawa mzee wangu wa historia ya wazee wa kariakoo Mohamed Said sidhani kama ana ilim yoyote.
 
Bwana Mvika
Hii historia safi sana. Inaonekana sisi watu wa iringa kila msomi ana maelezo fulani ambayo yakikusanywa vizuri yanaweza kutoa picha sahihi ya utawala huu wa Wahehe. Jambo la kufanya ni kila mwandishi kuelezea vianzo vya historia ili kama mtu mwingine ana chanzo bora zaidi aweze kuongezea. Basi malizia hiyo historia kisha wengine tutasaidia kuelezea ama kwa kirefu zaidi au kuanzia mapema zaidi kabla ya Mutwa Munyigumba.
Pia historia ya Wahehe ukiileza vizuri utakuta Wahehe walianza kufikia hatua ya kuwa "taifa" linalojitambua, lenye nchi yenye mipaka inayotetewa na mgawanyo wa kazi unaotegemeana nje ya koo. Maendeleo ya taifa hili yalikatishwa na ujio wa ukoloni.
Ilifikia wakati ambao wale waliofanya mzaha kiasi cha kuhatarisha taifa hilo walishughulikiwa haraka na bila huruma. Hili suala la kusisitiza "mahomelo" katika medani za kivita ni mambo ya kisaikolojia zaidi. Kwwa hakika Wahehe walikuwa wapiganaji wenye akili ya kutisha. Ile vita ya Lugalo ambapo Mjerumani alipigwa kama mtoto ndiyo ilithibitisha uwezo wa kivita wa Wahehe. Wahehe waliwaona Wajerumani wakija wakiwa Usagara chini ya Mlima Kitonga. Lakini wakaamua wasianze vita mapema. Wakatafuta mahala ambapo wao Wahehe walikuwa wana nafuu (advantage) kivita. Wakawangoja mpaka walipoingia bonde la Lugalo. Wakawapiga hapo. Mjerumani anaandika kuwa mbinu ya aina hiyo ilikuwa ya Napoleon wa Ulaya hawakuitegemea kuikuta kwa Mwafrika. Hiki ndiyo kisa cha Wajerumani kutaka kichwa cha Mkwawa kipelekwe Ujerumani wakidhani wangeweza kubaini alikuwa na ubongo wa aina gani au pengine kichwa kingeonesha kuwa hakuwa Mwafrika!
Pia ushindi wa Wahehe ulitokana na kuwa Wahehe walikuwa taifa changa la mchanganyiko wa makabila mengi. Hiyo nguvu kazi mpya na akili mpya ya Wahehe ilikuwa tofauti na makabila jirani. Green card ya Marekani ya sasa ya kutaka vijana wenye vipawa mbali mbali kutoka sehemu yo yote nje ya Marekani kuhamia Marekani si suala la kubahatisha lilianza zamani. Taifa ambalo watu wake wanazaliana wenyewe kwa wenyewe baada ya muda mrefu linakuwa na vizazi dhaifu.
Historia ikifundishwa vizuri ni nguzo muhimu kwa taifa. Ndiyo maana nampongeza kwa dhati huyu mwandishi na tafadhali amalizie alichokusudia kutujuza. Kumbukeni imesemwa na watu wanaofikiri kwamba: Wale wanaoipuuza historia watairudia!
 
Dah nzuri ila gupi sana mtumalizie hiyo story!Pamoja na hayo wale wenye historia za machifu wengine pia watujuze itakaa njema zaidi
 
Nimebahatika kufika Makumbusho ya Mkwawa pale Kalenga. Kuna kiongozi wa Watalii( ana uhusiano na ukoo wa Mkwawa) anasimulia hiyo hadithi kama unatazama movie aisee. ..nilijaribu kumrekodi alivyosimulia mara ya kwanza nilipofika pale ni tamu zaidi kuliko mara ya pili.
Inadaiwa Mkwawa alikuwa na wake 62 ambao aliwagawa kwenye makundi takribani 7. Kila kindi lilikuwa na mke kiongozi. Sasa Mkwawa alikuwa na chungu fulani hivi chenye matundu matundu ambacho akiweka dawa kilikuwa kinamtonya iwapo kuna mmoja kati ya 62 amechepuka.....!!!!
Katika masimulizi ya yule tour guide ni kuwa katika jeshi lake Mkwawa alikuwa na wanjeshi (makomandoo) wa kike hao walikiwa balaa. Tena alikuwa na vikosi kama vinne hivi; kikiwemo cha Upelelezi (kuna jina la kihehe alitutajia nalo ni jina la eneo mashuhuri pale Iringa maeneo ya nyuma ya Ratco mpaka Idara ya Maji, pia askari wa chambo wa kumuingiza adui kwenye reli (mmoja ndiye aliwaingiza askari wa kijerumani kwenye reli wakauawa kama sisimizi kwenye sukari) hawa walikuwa dhaifu kwa mwili kama mateja wetu, lakini ni shupavu ubongoni balaa.
Kwa jinsi anavyosimulia tour guide kama tungekuwa na akina Mkwawa wa5 hakika tusingetawaliwa....
Kilichomponza ni USALITI wa Chifu wa Wabena na Wasangu, waliokuwa tayari kuwaonesha Wajerumani ya kufika Kalenga usiku usiku wakitokea maeneo ya Mafinga..
Ukienda pale utainjoi zaidi kuliko kisimuliwa hapa.
 
Hicho ni chungu kimojawapo kati ya vyungu alivyovitumia kubaini mahali walipo maadui, pia kuweka dawa kubaini UCHEPUKAJI wa wakeze.
 
20161211_112939.jpg
Hili ndilo fuvu lake ambalo limeifadhiwa vema kabisa pale Makumbusho ya Mkwawa- Kalenga
 
hapo daraja la mungu alipoenda mama mkwawa ni kule mbeya na humo alipojirusha ni pale kwenye kijungu Mbeya
 
Back
Top Bottom