Ijue historia ya Chifu Mkwawa (Sehemu ya kwanza)

Issa.....
Kama unatania ni sawa ila kama unataka ufahamu hapo umeteleza. Alikojitupa mama yake Mkwawa ni kwenye Mto Ruaha (ambao ulikuwa unapita ndani ya ngome ya Kalenga) umbali wa kilometa kama 40 hivi kutoka Kalenga kama unaelekea Ruaha National Park.
 
Kilichosababisha hasa Mkwawa kupigana vita na Wajerumani ni kuvamiwa na kupigwa kwa Abushiri. Hawa wawili walikuwa marafiki sana kwani walifanya biashara pamoja( Abushiri alimfunza kiarabu Mkwawa na alimsilimisha, kama sikakosea Mkwawa akiitwa ABDALLAH) Hata bunduki ya kwanza ya Mkwawa akipewa zawadi na Abushiri kisha Mkwawa akatengeneza ya pili (zote zipo makumbusho ya Mkwawa).
Mkwawa aliposikia rafiki yake kashambukiwa alituma kikosi kwenda kumsaidia, ndipo alipotambua ukali wa Wajerumani. Na Wajerumani walitambua ukali wa Wahehe, wakapanga kufika Uheheni kwa vita. Mkwawa alijaribu kuomba suluhu na Wajerumani bila mafanikio (kuna barua aliandika kuomba suluhu, ipo pale Makumbusho ya Mkwawa, imeandikwa kwa Kiarabu)
Mkwawa akajipanga kuwashambulia Wajerumani huko Lugalo takribani kilometa 60 kutoka Kalenga uelekeo wa Morogoro. Katika vita hiyo ( kama alivyosema mwenzetu hapo juu ) Mjerumani alipokea kipigo cha AIBU sana.
 
Na hadithi yenu ikaishia hapo!! Watu bado wamekaa kwenye mabenchi wanawasubiri kumbe mmeshakoroma?
 
Tuendelee!
Baada ya vita hiyo ambayo askari takribani 300 wa Mjerumani kuuawa akiwemo Luteni Wao (kaburi lake lipo pale Lugalo hata sasa), askari wa Mkwawa walishangilia ushindi lakini walionywa kuwa kuna kikosi kikubwa zaidi cha Wajerumani kinakuja. Katika mapambano hayo ya pili Askari wa Mkwawa walipigwa vilivyo kwa mizinga na bunduki na kusababisha vifo vya askari takribani 300 pia.
Baada ya kipigo hicho Mkwawa alituma askari wengine waliokunywa dawa maalum za kuzuia risasi "bullet proof". Hawa wakitumia mikuki na mishale dhidi ya bunduki na mabomu ya mikono ya Wajerumani waliwaua askari takribani 100 wa Kijerumani.
Ndipo Wajerumani walipoenda kujipanga upya wakishirikiana na machifu wa Ubena na Usangu ( walikataa kushirikiana na Mkwawa kwa vile alikuwa akiwashambulia kila mara) waliowaelekeza njia ya kufika Kalenga na mbinu za kumshambulia Mkwawa. Sasa Wajerumani walipitia Mafinga kufika Kalenga wakitembea zaidi usiku ili wasionekane mpaka kwenye kilima kilichoko jirani Shule ya Tosamaganga. Wakiwa hapo juu walishambulia kwa mizinga mizito Ngome ya Liringa (ilikuwa na kipenyo cha km 13 na urefu kwennda juu ft12 na upana m 3) na ngome ndogo ya Lipuli (ya kipenyo cha km 5, masalia ya tuta lake yapo mpaka sasa).
Wajerumani walisambaratisha ngome zote huku wakijinadi kuwa WANASAMBARATISHA IRINGA (ndiyo asili ya mji kuitwa Iringa). Katika mapambano haya ya Kalenga bado Wajerumani walipata hasara kubwa kwani mmoja wa MAKOMANDOO wake aliuawa(kaburi lake lipo pembeni ya mto Ruaha pale Kalenga ukivuka tu daraja kuelekea) Hifadhi ya Ruaha
 
huyu mtemi mkwawa aliendesha sana utekaji nyara kutoka kaskazini usukumani unyemwezini alikuwa na nguvu karibu kushinda watemi wote tz

alizunguka karibu pande zote za nchi kuchukuwa watumwa hasa kaskazini magharibi mwanza, shinyanga, tabora maana huko ndiko walitoka watu wenye afya zao kwa ajili ya kuwatumikisha

Kwa mfano Mwambambe mwalinyungu mwenye asili ya tabora yule alikuwa mateka kutoka tabora aliletwa kutoka tabora na mnyigumba akiwa mdogo

Au mleta uzi unaweza eleza huyu kijana wa kinyamwezi alifika vp kalenga huyu jamaa alifanya ukoloni ndani ya nchi hiyo kitu wamsifie watu wa iringa tu cio usukumani



 
Sema huyu nae aliwaingiza chaka wenzake na miujiza yake ya risasi kuwa maji
 
Risasi kuwa maji cio yeye ni yule wa kilwa kijingitile ngwale
 


Sahihisha historia yako. Uwongo mwingi kuliko ukweli. Mkwawa alifundishwa vita Dodoma kwa chief Mazengo. Alitoroshewa huko akiwa mdogo kwa hofu ya Mwambambe aliyeshikilia uchief baada ya kufa Mnyigumba/Muyinga baba yake. Inasemekana Mwambambe alinogewa ukaimu akaanza mpango wa kumpoteza Mkwawa ambaye ndiye alitakiwa kutawala ila kwa sababu alikuwa mdogo, Mwambambe akateuliwa ashike madaraka hadi mkwawa atakpofika umuri sahihi.

Wazee wa Iringa walimtorosha na waliendelea kuwasiliana na Dodoma na mipango ya kumrejesha iringa ilifanywa kisiri sana baada ya kuthibitishiwa kwamba sasa likuwa ametimu umuri na pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kupambana. Wakati anarudi watu wakajawa hamasa na wakaanza kuonyesha kiburi cha kichinichini kwa kaimu. Na lipochunguza akaambiwa Mkwawa anakuja na ndipo vita vilipopiganwa sana kati ya majeshi ya Mwambambe na Mkwawa. Ni kwlei Mwambambe alikuwa na nguvu za mwili na za kichawi pia. Rejea historia ya kijiji kilichonjiani kiitwacho Lunda Matwe!. Mafuvu yale hayakuwa na Mjerumani na Mkwawa bali ya vita vya Mwambande na Majeshi ya mkwawa.

Sitaki kuandika kukuharibia sanaa yako lakini naomba sana kabla hujaendelea nenda kalenga, au kwa kina Mwalumato wako maeneo ya Lungemba wakuelezee. Waweza pia kuwaona kina Mkwawa wapo wakupe habari sahihi badala ya kuchapia!.

Sitaki kurekebisha makosa yote uliyoaandika lakini wewe waweza kupat taarifa sahihi ukarekebisha.

ANGALIZO: HIYO PICHA HAPO SI YA MUTWA MKWAWA, WATU WASIJE WAKADANGANYIKA PIA. FUVU LILIKO KALENGA PIA SI LA MKWAWA.
 
Eleza umri aliokuwa nap mbaka unasema Mdogo na pia elezeza aliyekwenda Kumkomboa chief Mwinyiguma alikuwa ni nani kama mkwawa alikuwa na umri Mdogo
 
 
Kuna kitabu cha zamani sana kinaitwa 'Mkwava na kabila lake' kinaeleza vizuri kuhusu historia ya Iringa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…