Ijue historia ya eneo la Kisutu Dar—1

Mkuu ulikuwa umeandika historia nzuri sana mpaka ulipoanza kuwataja hawa watu.. Sijaelewa kama unajaribu kuwalinganisha kutokana na maeneo walikotoka (wa bara dhidi ya wapwani) ama dini zao (waislam dhidi ya Wakristo) vinginevyo historia nzuri umetufumbua macho wengi…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo waislamu mnataka Serikali ikihamia Dodoma (Rais akienda Dodoma) mrudishiwe majengo ya Ikulu na St Joseph Parish?

Ndo mnaanza hila za upotoshaji wa historia?


Uzuri Tanganyika Imepata Uhuru mwaka 1961. Kutokea hapo kila mtu akawa na kile alichokimiliki. Hivyo niseme tuu kwamba mpotoshe mpotosheje Tanzania Haina Dini watu wake ndo wana Dini.
 
Wapi hapo waislam wamedai warudishiwe Ikulu. hiyo ni historia ya mji wetu Mzizima Bandari Salama Dar es Salaam Sasa sijui mna tatizo gani. khs Ikulu kuhamia Dodoma itakuwa kheri kwetu ujui waswahili tunasema kuvuja kwa Pakacha...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku njema huonekana asubuhi na dalili ya mvua mawingu.
 
Historia imekaa vizuri, Kwa jinsi niujuavyo mji wetu pendwa wa Dar, kuna ushabihano mkubwa kati ya Historia hiyo na hali halisi iliyopo sasa.
Mtoa mada hongera, umejitahidi kutofungamana na upande wowote, isipokuwa wapo wenye mentality ya upinzani daima NA upotoshaji.

"We need to know more" reveal the truth.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rubawa, nipo interested na Historia kamili ya Ocean Road Cancer Institute.

1. Lini ilijengwa?
2. Nani alijenga? Na architect alikuwa nani?
3. Matumizi yake ya awali kabla ya wajerumani yalikuwa ni yepi?
4. Wajerumani walilipataje?
5. Matumizi kipindi cha Wajerumani yalikuwa yapi? Jina walilolotumia kiutambulisho ni lipi?
6. Dr. Robert Koch ni nani? Alifika lini hapo Ocean Road ku run research yake ya Malaria?
7. Baada ya vita vya kwanza vya dunia, waingereza walipoichukua nchi, walilitumiaje jengo hilo na jina gani walilolibatiza kiutambulisho?
8. Baada ya Uhuru, jengo lilitumikaje? Lini lilianza kuwa martenity wing ya Muhimbili?
9. Waingereza walifanya extension ya jengo kwa kuongeza majengo. Kuna old german building na British wing. Ni yepi majengo waliyoyaongeza waingereza?
10. Baada ya maternity wing, ni link ikaja kuwa radiotherapy unit au radiology unit ya muhimbili?

Nachokifahamu baada ya 1996, hapo ndipo rasmi kwa muswada uliosainiwa na Mh. Rais wa awamu ya tatu, hapo ndipo Ocean Road Cancer Institute ilipozaliwa.

Kama utaweza kunisaidia viongozi wa mwanzo kuiongoza Taasisi hiyo kabla ya Prof. Twalib Ngoma kuwa mkurugenzi itasaidia sana ktk kuijua historia ya Taasisi hiyo.

In case kama una reference ninayoweza kuipitia kujibu maswali hayo nisaidie ilo nijifunze.

Shukran

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu Mohammed Said na bibi FaizaFoxy msaada wenu please.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna huu muhadhara wa Sheikh Zuberi Yahya (Mungu amrehemu) kuhusu Historia ya jiji la Dar es Salaam tokea 1865.
 
Kuna huu muhadhara wa Sheikh Zuberi Yahya (Mungu amrehemu) kuhusu Historia ya jiji la Dar es Salaam tokea 1865.

Shukran, Allaah amrehemu Sheikh Zubeir. Una majibu specific kuhusu historia ya Ocean Road?

Sent from my SHV-E330K using Tapatalk
 
Shukran, Allaah amrehemu Sheikh Zubeir. Una majibu specific kuhusu historia ya Ocean Road?

Sent from my SHV-E330K using Tapatalk

German Government Hospital.
But as early as 1888, it was a mere provisional hospital, set up in Zanzibar by the German Lutheran Church to serve the needs of the Germans living and working on the East African coast.
When the British established their protectorate over Zanzibar in 1890, the hospital was now moved to Dar es Salaam.
As a hospital (and its laboratory), served as basis for Koch’s research in the field of malaria, black water fever, sleeping sickness and relapsing fever.
It was from Africa and particularly at this institution, that Koch embarked on his journey to Stockholm, Sweden, to receive the Nobel Prize in December 1905.
nilisoma mahali huyu Dr ndiye aliyegundua bakteria wa Kifua Kikuu
 
Kweli kbs upo Sahihi ndugu yngu mradi ww ni mtu mweusi mwenzangu sina tatizo kbs maana kila siku naomba radhi sie wa kusamehewa tu...
Rubawa huna makosa maana wewe umetuletea uhondo, wengine hatukujua kuna Makabburi ya Wangazija, makaburi ya WaOman, Wakorja ungemalizia basi hako kasehemu ka pili ka Mtaa huo wa Kisutu ili tuweke sawa Historia na najua kina mohame Said wapo
Mm nijuavyo Sultan Majid kaitawala Zanzibar baada ya Sultan Barghsh kufa mwaka 1856 na ujasiri wa kuja Dar na kujenga jengo la Ikulu hapana ila km yalikuwepo majengo yake na Misikiti sawa
Hapo Magogoni pamejengwa 1922 na Mhandisi Sinclar
The building was built in 1922 by the English architect, John Sinclair. John Sinclair designed a number of buildings in Tanzania like the High Court and the Bharmal Building.

 
Umejitahidi sana kutufumbua tusiyoyajua pia nimefurahi kuona una busara kwa baadhi ya watu kukupinga kwa baadhi ya mambo hapa.Mtu kukosea tu kuandika karne ya 1800 sio tatizo eti historia nzima ikaonekana haifai.Wajiongeze kama hii ni karne ya 21 unachukua 21-1 unapata 20 ndio tuko miaka ya 2000 kwa mantiki hiyo 18+1 ni sawa na 19 hivyo uliamanisha 18000 ni karne ya 19.
Watu wasiwe wavivu wa kufikiri na kupambanua hata kwenye magazeti japo kuna wahariri lakini typing errors zinatokeaga.
Wasikukatishe tamaa tuletee mambo mazuri sehemu ya pili.Wewe umezaliwa 1948 ni mkubwa si ajabu wengine humu wamezaliwa miaka ya 90 hawajui historia
 

Mimi nadhani baadhi ya watu wamesoma hii mada tayari na mawazo yao mgando.

Hayo ya karne na Ottoman Empire ni mchanganyiko tu wa mawazo lakini Mzee Rubawa ametuongezea ujuzi kwenye historia yetu ya pwani ya Africa ya Mashariki.

Ukwaju, kwa taarifa yako tu mtawala wa kwanza muarabu alikuwa Seyyid Said bin Sultan ambaye alikufa 1856 na ndiyo akatawala mtoto wake Seyyid Majid kwa upendeleo wa waingereza.

Alipokufa Majid ndiyo akatawala Barghash 1870-1886.

Wakati wa Majid na Barghash ukanda wa maili 10 (10 miles coast) kutoka Mozambique mpaka Kismayuu Somalia ulikuwa chini ya utawala wa Sultan wa Zanzibar. Kwa hivyo ardhi hiyo ilikuwa chini ya umiliki wa Sultan wa Zanzibar.

Hiyo ikulu anayozungumzia Mzee Rubawa siyo hiyo munayoiona sasa. Wakati huo mji wa mzizima haukuwa hivyo. Hata hilo jina Darussalaam alitoa Sultan Majid.

Wajerumani na Waingereza ndiyo walikuwa wakigombea maeneo ya utawala na hapo ndiyo mchezo ukabadilika.

Kumbukeni enzi hiyo hakukuwa na nchi zinazoitwa Tanganyika, Congo au Kenya.
 
Ingia ndani ikulu angalia mlango wa ikulu wa mbao. Uliochongwa kwa nakshi utaona maandishi ya kiarabu imeandikwa bismillah arrahman arrahim
Nimeshangaa alipodai mwarabu kajenga ikulu ya magogoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…