Rubawa, nipo interested na Historia kamili ya Ocean Road Cancer Institute.
1. Lini ilijengwa?
2. Nani alijenga? Na architect alikuwa nani?
3. Matumizi yake ya awali kabla ya wajerumani yalikuwa ni yepi?
4. Wajerumani walilipataje?
5. Matumizi kipindi cha Wajerumani yalikuwa yapi? Jina walilolotumia kiutambulisho ni lipi?
6. Dr. Robert Koch ni nani? Alifika lini hapo Ocean Road ku run research yake ya Malaria?
7. Baada ya vita vya kwanza vya dunia, waingereza walipoichukua nchi, walilitumiaje jengo hilo na jina gani walilolibatiza kiutambulisho?
8. Baada ya Uhuru, jengo lilitumikaje? Lini lilianza kuwa martenity wing ya Muhimbili?
9. Waingereza walifanya extension ya jengo kwa kuongeza majengo. Kuna old german building na British wing. Ni yepi majengo waliyoyaongeza waingereza?
10. Baada ya maternity wing, ni link ikaja kuwa radiotherapy unit au radiology unit ya muhimbili?
Nachokifahamu baada ya 1996, hapo ndipo rasmi kwa muswada uliosainiwa na Mh. Rais wa awamu ya tatu, hapo ndipo Ocean Road Cancer Institute ilipozaliwa.
Kama utaweza kunisaidia viongozi wa mwanzo kuiongoza Taasisi hiyo kabla ya Prof. Twalib Ngoma kuwa mkurugenzi itasaidia sana ktk kuijua historia ya Taasisi hiyo.
In case kama una reference ninayoweza kuipitia kujibu maswali hayo nisaidie ilo nijifunze.
Shukran
Sent using
Jamii Forums mobile app