Ijue Historia ya Kabila la Wapare

Ijue Historia ya Kabila la Wapare

Kweli kuna suala Zima la maendeleo ambalo linamtaka kila mmoja mwenye nguvu afike, tunaita "msaragambo" na endapo mtu hatafika bila sababu yoyote ya maana anafanyiwa "kupambuliwa" yaaani anachukuliwa kuku au mbuzi watu wakale waliofanya kazi.
 
VERY GOOD MEMORY! big UP mleta HADITHI YA HISTORIA YA WAPARE KWA KWELI NIMEBURUDIKA JAPO MIE MSUKUMA. NASHAURI NA WENGINE WAJE NA HISTORIA ZA MAKABILA YAO ILI KILA MTU AFAIDIKE HASA KIZAZI HIKI AMBACHO WATU WANAANZA KUSAHAU ASILI YAO. NINGEPENDA PIA KAKA KUNA WAANDISHI WAZURI WATULETEE LUGHA ZA MAKABILA MBALIMBALI NA TAFSIRI ZAKE.
 
Wapare tunaroho nzuri jaman...Nakumbuka wakati tupo pr kuna marafik zangu saa ya kurud walikuwa hawataki kupitia kwetu maana ukipita lazima ule.Na pote nilipopita kwa wapare ilikuwa hiyo lazima

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Hasa kama kumepikwa chakula kinaitwa kishumba! lazima ule
 
Wapare

Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, Taveta na Ukamba. Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.

Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi anaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisherani wa Kikiristo waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru,Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisla la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisala la Kiluteri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Waluteri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga manake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baade na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale

Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja etc, wana asili ya maeneo yao kama Bwambo,Mjema,Usangi,Vungi,Suya,Gonja etc.

Mifano ya majina ya watoto wakipare

Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.

Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa, Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.

Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikwepoa hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven(JB),Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.

Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande(mchanganyiko wa mahindi na maharage).Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bilaa kuwaza masuala ya upishi.Samaki pia ni kipenzi cha wapare wengi na ndio maana utawasikia watani wao wakuu yaani wachaga wakiwatainia kuwa wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki wakimaanisha kuwa ni wabahili.Wakati mwingine utawasikia wapare wenyewe wakisema "ipere ethi kindu,kindu ni mshombe"kuwa samaki si kitu kitu ni mchuzi kuonesha ubahili wao kuwa samaki anayebaki atumike tena wakati mwingine bqaada ya mchuzi kuisha.
Maeneo ya wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi yanavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya upareni kadhalika.Kuna maeneo yanayovutia kama milimani(Usangi,ugweno,misitu ya shengena n.k.Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua.

Kama ilivyo kwa makabila mengine wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya ya elimu,siasa na uchumi.Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya wapare.Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,katani,mahindi n.k zimeinua maendeleo ya uchumi.Pia Miundo mbimu kwa kiasi chake imeboreshwa,kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro,pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika Kwa upande wa siasa wapo pia wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja ya siasa kama Mh.Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu,Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe na pia Waziri,na wengineo wengi kama Anna KIlango Malechela,Pro.Jumanne Maghembe,Michael Kadeghe n.k Pia Mheshimiwa Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwnasiasa maarufu hapa nchini(waweza ongeza).

Waweza ongeza kuiedit ili kuiweka historia ya wapare vyema na kujua tulipotoka na sasa Wapare wapo wapi kwani vitu vingi vimebadilika.Edit na kuongeza historia unayoifaham ukiwa na uhakika ili ikae mtandaoni wikipedia

Kwenye list yako umemsahau Naghenjwa!
 
Itikija hutumiwa na wanaume pia
 
LIKUD, Naghenjwa,

Vava wetu weho uko wanga,

izina lako ligimbikwe,

vuvumwa vwako vuze,

kikundire chako kifunyanywe kunu he masanga, sa vuntu chefunyanywa uko wanga.

Utuinke yoo kijo chetu.

Utushighie rando jetu, sa vuntu na uswi twevashighia varando vetu;

usitugere he mighesho, mira utukije he ula mvivi.

Ambu vufumwa na nzinya na ngazo, ni vyako kae na kae.

AMEN
 
Last edited by a moderator:
Duduwasha, The hammer,

nitapenda kuwakumbuka Machifu 9 wa iliyokuwa Pare Native Authority. pamoja na kwamba napinga Uchifu, lakini nitaeleza kwanini ninawaenzi Machifu hawa pamoja na mapungufu waliyokuwa nayo.

baada ya vita kuu ya pili Muingereza aliweka lengo kwa koloni la Tanganyika kuandikisha 36% ya watoto shule ya msingi. Tanga Province ambako wilaya ya Pare waliweka lengo kwamba mpaka kufikia mwaka 1956 wawe wamefikia 50%. Machifu wa Pare Native Authority waliweza kuhamasisha wananchi wao na ilipofika 1952 waliweza kuandikisha 90% ya watoto shule ya msingi.

pia vilikuwepo VIKUNDI VYA ELIMU YA WATU WAZIMA katika maeneo mbalimbali kama Usangi, Mbaga, Same, Ugweno. wakinamama hawakuwa nyuma katika kuanzisha vikundi vya kujifunza kusoma. mwamko huo wa kinamama kujifunza kusoma ktk utu uzima ndiyo uliochochea elimu ya mtoto wa kike katika maeneo hayo. historia inapaswa kuwakumbuka kinamama hao.

kampeni ya elimu ya watu wazima ilipelekea kuanzishwa kwa GAZETI lilloitwa HABARI ZA UPARE. gazeti lilianzishwa 1951 na kuna kipindi lilikuwa likitoa makala 2000 kwa mwezi. nitatafuta makala ya gazeti hilo na kuwawekea mlisome.

shule nyingi za msingi haswa zile za WALUTHERI, SDA, na WAISLAMU, na hata SERIKALI, zilijengwa kwa mwamko wa kujitolea wa wananchi wenyewe. wananchi wa maeneo kama Usangi na Ugweno kwa miaka karibu 14 bila msaada wa fedha au utaalamu walishiriki ujenzi wa barabara za milimani kuwaunganisha na mji wa Mwanga. wananchi wa Chome, Mamba,Vudee, nao hawakuachwa nyuma katika ujenzi wa barabara kwa njia ya kujitegemea.

Machifu au Wafumwa 9 ninaowakumbuka ni Chifu/Mfumwa Sabuni wa Usangi, Mfumwa Kibacha Singo wa Same, Mfumwa Manento Sekimanga wa Mamba, Joseph Mamphombe wa Mbaga, Kigono Chuma wa Gonja, Folong'o Makange wa Chome, Minja Kukome wa Ugweno, Yoeli Mtindi wa Hedaru.

Nyumba ya ghorofa moja aliyoishi Mfumwa Minja Kukome wa Ugweno mpaka sasa ipo.
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda sana hii. Big up kwa mleta thread. Jina la Nankondo lina nihusu sanaaaaa!
 
800px-Tanzania_Kilimanjaro_location_map.svg.png

Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa

wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya
Tanzania . Wanakadiriwa kuwa 1,000,000 hivi.
Lugha yao ni Kipare (au Chasu).
Makao

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na

Mwanga , mkoa wa Kilimanjaro , lakini pia wapo
katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni ,

Himo , Mabungo , Uchira , Moshi mjini, na pia

katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na
mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika
wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za
Bumbuli na Mavumo .

Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka

nchini Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla,
kutokana na suala la utandawazi Wapare

wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli

mbalimbali, kwa mfano jamii kubwa ya Wapare
waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga
makazi, na hali imekuwa hivyo katika mikoa
yote nchini na kwingineko.

Maeneo ya Wapare yamekuwa na mvuto wake

mfano katika milima ya Upareni kwenye
maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari
ya kijani kibichi ambayo inavutia japo shughuli

za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu

mazingira ya Upareni kadhalika. Kuna maeneo
yanayovutia kama milimani (Usangi, Ugweno,
misitu ya Shengena n.k.) Pia skimu ya

umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika

shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.
Pia kuna mwamba wa kuvutia Same

unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama

ikamba la fua. mji mkuu katika kabila la upare
ni maore ulioko wilaya ya same ma chief wake
alikuwa mfumwa boaz mashambo
Asili

Wapare wanasemekana wametoka katika nchi

ya Kenya sehemu za Taita , Taveta na Ukamba .
Ni kabila la watu wachache lakini wana
ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na
uchumi wa Tanzania [ onesha uthibitisho ] .

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa

wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na
Wanguu . Ukaribu wao uko katika lugha ambapo
maneno mengi ya makabila haya yanafanana.

Vile vile majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo

kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo
wanamoishi makabila hayo. Kwa mfano, kwa

Wapare kuna majina ya maeneo kama vile

Gonja, Ndeme , Ndolwa n.k. Majina haya yapo
pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii
inaonesha kwamba makabila haya yana asili
moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni

Uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga maana
yake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa
watu wa makabila haya wote walitokea Kenya.
Wachagga walitangulia wakawahi kuishi
maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima

Kilimanjaro . Wapare walikuja baadaye na

walipotaka kuishi na Wachagga ndipo vita
vikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili
kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare
walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa
Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu
ikiwa na maana ya "vareasa" au "watu

wanaotumia pinde na mishale".ikiwemo ya

sumu
Tabia

Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo

watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni
kabila la watu wanaopenda haki (yaani
hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).

Ndiyo maana watu wengine wanadhani

wanapenda kesi , bali kesi ni njia mojawapo ya
kuhakikisha haki inatendeka katika jamii .
Utawasikia watu wengine wakidai kuwa Mpare

yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku .

Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa
kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko
yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao
wakawa hawana sifa hii tena.
Uchumi

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka

1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana,
na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare

walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na

chuma kama majembe , mapanga, visu, silaha
kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano

Wachaga , na wamekuwa na uhusiano tangu

siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa
Wasambaa .

Jamii za Wapare zimegawanyika katika

makundi ya wafugaji na wakulima. Wakati
wafugaji wengi walihamia katika tambarare za
Upareni, wakulima waliishi milimani na wafuaji

wa chuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na

uwezekano wa kupata chuma.
Utamaduni

Kwa asili Wapare hupeleka vijana wa kiume

jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi
ya kuishi na familia , japo siku hizi utamaduni
wa kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu
wachache.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya

kilimo , ufugaji na biashara , ndiYo maana hata
leo wana uchumi mzuri katika viwango vya
Tanzania.

Tamaduni, mila na desturi za wapare

zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu
zote. Hapo kale Wapare pia waliweza
kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli
za jadi, jambo ambalo wapo baadhi ya Wapare

ambao mpaka leo wanaweza. Kwa mfano

Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo,
ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais
wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania kupiga marufuku utawala wa jadi.

Kiongozi huyo aliyefariki dunia mwaka 1981
alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.
Pia walikuwepo hata watu maarufu maeneo ya

wilaya ya Same ambao waliamini dawa fulani

ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna
hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua
eneo hilo. Mambo haya na mengine mengi

kwa sasa yanapotea kama si kwisha kabisa.

Wapare pia wamekuwa wakihusishwa na imani
za uchawi na ushirikina kama ilivyo kwa
makabila mengine Tanzania, lakini suala hili ni
la mtu binafsi zaidi na si la jamii fulani peke
yake kwa sababu ni imani ambazo zipo kote

Tanzania na hatuwezi kunyooshea kidole eneo

fulani.
Kwa wapare walio wengi, uchawi na wizi
vilipigwa marufuku hadi kwenye matambiko.

Mchawi na mwizi waliombewa wafe kama

ikitokea wapo kwenye jamii. Kuna utamaduni
unaoitwa "mma" ambapo matambiko
yalifanyika mahali fulani na mwizi akaitwa pale
yanapofanyikia kisha mwombaji akaulizwa
angependa mwizi apewe adhabu gani.

Kwa kawaida adhabu mbili kuu ndizo

zilikuwepo: kumfanya mwizi augue sana kwa
muda mrefu kabla ya au kumuuwa mara moja.

Mwombaji akimamua mwizi auawe basi kwa

vile anaonekana kwenye matambiko, mtaalamu
wa matambiko humuuwana akafariki mida

hiyohiyo huko aliko. Tatizo la kuu la "mma" ni

kwamba lilikuwa linaua watu wote wa ukoo wa
mwizi au mchawi (lakini mwizi akiwa wa
kwanza). Ni mpaka watakaopjua kuwa ni
"mma" ndipo watafanya matambiko ya kutoa

mnyama kafara kwa ajili ya kuzima athari za

mma. Kwenye kuuzima mma ni lazima
aliyedhulumiwa ahusishwe kwenye matambiko
ikiwa ni pamoja na kuombwa radhi, vinginevyo
mma hautazimika. Athari zingine za "mma" ni

kwamba aliyeomba tambiko hilo (yaani

aliyeibiwa au aliyedhulumiwa), ni lazima atoe
kafara mnyama kama vile kondoo au ng'ombe
kabla na baada ya tambiko. Baada ya mwizi

kufa ni lazima mwombaji atoe mnyma kafara ili

kuzima madhara ya "mma". Vinginevyo vifo
vitokanavyo na mma humrudia mwombaji na
ukoo wake.

Kuna watu maalum waliokuwa wamebobea

kwenye mambo ya "mma". Kwa sababu ya
matambiko hayo ndio maana wapare wengi si
wezi - japokuwa siku hzi baadhi yao

wamejiingiza kwenye wizi. Tambiko lingine

linalofanana na hilo liliitwa " kubigha
nyungu" (kwa kiswahili - kupiga chungu).
Chungu hicho kilipigwa kama tambiko la

kumuuwa mtu aliyedhulumu (au ukoo wao

uliohusika na dhuluma) watu wengine. Chungu
hicho hupigwa chini mara moja kwa kishindo,
ambapo tendo hilo lilambatana na matambiko

fulani. Mara chngu hicho kipasukapo kwa

mshidno ndipo ukoo wa waliodhulumu huanza
kufa mmojammoja. Iliaminika kwamba kitendo
cha chungu kusambaratika vipande vipande
ndivyo na ukoo uliodhulumu husambaratika.

Tambiko hili lilichangia kwa kiasi kikubwa

Wapare kuwa kabila la wapenda haki. Nasikia
tambiko hili lilikuwepo hata kwa makabila ya
jirani kama vile wasambaa, Wameru n.k. Hata
hivyo matambiko hayo kwa sasa hivi hayapo.

Yamebaki historia kwenye kabila la wapare na

hayo makabila mengine.
Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalumu
kama kwenye jando au unyago, pia nyimbo za
Kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na
sherehe nyingine na kupendezesha tukio
husika. Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo

hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi

zimerekodiwa.
Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za
sanaa kama methali, hadithi , ma igizo n.k.
wakati wa mapumziko na matukio fulani. Hali
hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu

wa maigizo na nyimbo kama Halima Madiwa,

Jacob Steven (JB), Sinta, Sara Mvungi, Roma
Mkatoliki na wengineo wengi

Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi Wapare

walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa
kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,
kirutu n.k. Ipo miti maarufu kama mwori

ambayo ilitumika. Mchango wa dawa za

mitishamba kwa watoto na watu wazima
ulionesha mafanikio tangu zamani na hata
sasa.

Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande

(mchanganyiko wa mahindi na maharage).
Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya
Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze
kupumzika vizuri mwisho wa wiki bila kuwaza
masuala ya upishi .

Samaki pia ni kipenzi cha Wapare wengi na

ndiyo maana utawasikia watani wao wakuu
yaani Wachaga wakiwatania kuwa Wapare
wanakula ugali kwa picha ya samaki. Huu ni

utani ulioasisiwa na wachagga baada ya

kutembelea kaya nyingi za wapare na kukuta
wamehifadhi samaki. Hapo ndipo mchagga

mmoja alisikika akisema "Yesu yaani wapare

wanapenda samaki, kila nyumba unayoingia
utakutana na samaki. Yaani siku wakikosa
samamki watakula ugali kwa picha ya samaki".

Utani huo ulikuzwa na wachagga hadi

ukaonekana kama ni kweli, ukizingatia
wachagga wametapakaa nchi nzima.

Hata hivyo wapare nao wana utani wao kwa

wachagga unaosema "Muagha wedi ni ula
efwie". Yaani "mchagga mzuri ni yule
aliyekufa" wakimaanisha kwamba wachagga

wote ni walaghai na wadhulumishi wakati wote

wa maisha yao. Ni mpaka atakapokufa ndipo
ulaghai na udhulumishi wake vitaisha.
Miiko

Kuna miiko ya Wapare kama vile kufuatilia maji

kwenye mabirika yao yaliyokuwa yakijulikana
kama NDIVA; kwa wakinamama ilikuwa ni
marufuku kusogelea maeneo hayo hasa

wakiwa na vyungu vyao vyenye masizi au hata

bila kitu.
Pia kulikuwa marufuku kwa wakinababa kula
meza moja na wakinamama: walikula sehemu
tofauti wanaume na wanawake bila kujali umri
walizingatia jinsia tu.
Dini

Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti, kwa

kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne
ya 19 hadi 20 wamisiorani wa Kikristo
waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana

kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya
ya Same katika maeneo ya Ndungu , Kihurio,
Bendera , Hedaru, Makanya , Suji, Chome , Tae ,
Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa

kanisa la Sabato wengi sana. Maeneo kama

Chome , Mbaga , Gonja , Vudee yana waumini
wengi wa kanisa la Kilutheri. Katika Wilaya ya
Mwanga kuna idadi kubwa ya Walutheri na
Waislamu . Wakatoliki, japo ni wachache,

wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara

Juu, Vumari na Mbaga.
Koo
Wapare wana koo nyingi na majina mengi
yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au
mazingira ya kuzaliwa kwao, mfano Mbwambo,
Mjema, Msangi, Mgweno, Mvungi, Msuya,
Mgonja n.k. wana asili ya maeneo yao kama

Bwambo, Mjema, Usangi, Vungi, Suya, Gonja

n.k.
Mifano ya majina ya watoto
wa Kipare
Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)
Ingiahedi, Itikija, Kafue, Kapingu, Kapwete,
Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho,

Kondisha, Ludao, Mchikirwa, Mshinwa,

Mwajuma, Naanjela, Nacharo, Naelijwa,
Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete,
Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,

Namkunda, Nabera, Namangi, Nangasu,

Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu,
Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji,

Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza,

Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero,
Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri,
Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe,

Nietiwe, Ntevona, Sangiwa, Shode, Yunesi.

Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema,
Chedieli, Chuma, Elieseri, Eliesikia, Elinighenja,
Elibariki, Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni,

Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio,

Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo,
Kalinga (jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa ),
Kalutu, Kambaita (jina hili lipo pia kwa

Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (jina hili

lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni,
Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi,
Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho

(Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe,

Kileng'a, Kinenekejo (wengine hufupisha na
kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo,
Kisenge, Kitojo, Koshuma, Kutua, Letei, Liana,
Linga, Lukiko, Lukio, Lukungu, Lusingu, Macha

(jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao

ni ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina
hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya
majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve,
Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo,

Mding'i, Mgheni, Mhando (jina hili pia lipo

mkoa wa Tanga), Minja (jina hili pia lipo kwa
Wachaga ambapo kwao ni ukoo), Mkodo,
Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (jina hili lipo pia kwa

Wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa

Wapare lina maanisha "mtafuta mali"), Mnaro,
Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa,
Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio,

Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera,

Mteti, Mwanyika (jina hili pia lipo Mkoa wa
Njombe ), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai,
Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo
(Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe,

Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (jina hili

lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata
kwa Wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo
kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao,

Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea,

Ringo (jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo
kwao ni ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue,
Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu,

Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji,

Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota,
Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (jina hili pia

lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni ukoo),

Tenshigha, Teri, Twazihirwa, Warema, Zihirwa,
Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali

ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza
akachukua au akamwita mtoto wake. Pia
majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi

ya Wapare yakiwa na maana tofautitofauti.

Maendeleo

Kama ilivyo kwa makabila mengine Wapare nao

wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya
elimu, siasa na uchumi. Zipo shule nyingi za

zamani na mpya katika maeneo ya Wapare.

Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,
katani, mahindi n.k. zimeinua maendeleo ya
uchumi.

Pia miundombinu kwa kiasi chake

imeboreshwa, kuna mabasi ya Kilenga
yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro, pia

magari yafanyayo safari za mikoani kama

Ngorika.

Kwa upande wa siasa wapo pia Wapare ambao

wamepiga hatua kubwa katika nyanja za siasa
kama Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri

Mkuu , Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi

kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la

Kawe, na wengineo wengi kama Anna Kilango

Malechela, Profesa Jumanne Maghembe,
Michael Kadeghe n.k. Pia Chediel Yohane
Mgonja aliyewahi kuwa mwanasiasa maarufu
nchi.

attachment.php

Attachments

  • Mkoa wa kilimanjaro.jpg
    Mkoa wa kilimanjaro.jpg
    40.6 KB · Views: 3,453
Kuna upungufu kwenye makala yako. Kuna kabila la Wagweno naona unalivhanganya na Wapare. In fact ni makabila yanayochangamana lakini lugha zao ni tofauti kabisa. Moja kati ya koo za Wagweno ni Msuya, wewe umetaja kuwa ukoo wa Wapare. Fanya utafiti tena. Hata hivyo makala yako ni nzuri.
 
Nakupongeza kwa kutupa historia ya wapare lakini wagweno ni kabila na kuna koo zake,zimeingiliana na wapare pia wanamwingiliano na wachaga mfano wapo wasechu/wamari/waringo kwa uchache,hebu changanua tena ili taarifa yako iwe timilifu .
 
Unaonaje na wewe ukanisaidia kuchanganuwa tena? ili na wewe Taarifa yako iwe timilifu?
 
Wapare, wachaga na wamasai tunaambiwa walitokea Kenya. Wamanyema Kongo, waha Burundi, wamakonde, wamachinga na makabila mengine ya kusini Msumbiji, makabila yanayopakana na Malawi tunaambiwa asili yao ni Malawi, yanayopakana na Zambia tunaambiwa walitokea Zambia, wahehe na makabila mengine ya Kagera tunaambiwa asili yao ni Uganda na Rwanda, yan ukifata mlolongo wa makabila utaambiwa makabila yote yanaasili ya nchi za nje. Sasa swali ninalouliza inamaana kabla ya hayo makabila kuingia Tanganyika kutoka katika hizo nchi Tanganyika ilikuwa ni nchi ya misitu tu na wanyama au ilikuwaje? Na kama watu walikuwepo je walikuwa ni wa makabila gani? Naomba kujulishwa km unafaham chochote kuhusu haya
 
Nakupongeza kwa kutupa historia ya wapare lakini wagweno ni kabila na kuna koo zake,zimeingiliana na wapare pia wanamwingiliano na wachaga mfano wapo wasechu/wamari/waringo kwa uchache,hebu changanua tena ili taarifa yako iwe timilifu .
wapare wamegawanyika nao kama walivyogawanyika wachaga wa Rombo,Machame,Marangu n.k Wagweno sio kabila
 
Tafuta kitabu kilichoandikwa na Nicodemus banduka usome mila na desturi za wagweno,ndipo ndugu yangu utatambua kuwa wagweno ni kabila,kigweno hakina mwingiliano na kipare hata kidogo.kabila tofauti ila mazingira yao yapo pamoja
 
image.png
betlehem,
elangwa shaidi alikuwa Inspector General wa Polisi baada ya uhuru. Prof.abdulrahman msangi mtanzania wa kwanza kupata shahada ya sayansi toka London University[makerere college], na dean wa wa kitivo cha sayansi UDSM. Balozi Akili Bernard Chagi Danieli "a.b.c.danieli" alikuwa balozi wa tanzania UN, mwaka 1968. bahati mbaya alifariki akiwa bado ni kijana. Nassoro Mnzava alikuwa Jaji Kiongozi, anakumbukwa kwa kusimamia kesi ya uhaini miaka ya 80. Mishael Muze ni mhadhiri wa hisabati, mwandishi wa vitabu vya kiada, na alipata kuwa kamishna wa elimu. Mahamoud Mwindadi alikuwa katibu wa bunge wakati wa awamu ya kwanza. Mahamoud ni ndugu na Prof.Idi Mwindadi Mmbaga. Keto Elitabu Mshigeni professor wa botany, ni mmoja wa waasisi wa University of Namibia. Kuna jengo limepewa jina " Keto Mshigeni Mariculture Building" kwa kutambua mchango wake kwa Univ of Namibia.
Iki uu purofetha mshingeni efum mamba mpinji hala kitala hala ejengie nyumba yake tumwekirairwa iti ni yakwe purofetha mshigheni.. Huyu jamaa sasa yupo kairuki hapo nadhnia na juzi juzi katunukiwa sijui nini hapoa angalia mwenyewe hapa attached
 
Hongera yake,profesa Mshigeni.
Kwenye misitu ya SHENGENA kuna bwawa moja linaitwa 'NDIVA NGUNDU' (sijui kama spelling ni sahihi - bwawa la maji mekundu). Hapo wale wapare wanaopenda uganga huenda kukutana na mizimu. Inahadithiwa kuwa mizimu ikiwa haikupendi ukifika bwawa lote hufunikwa na majani ya miti na hutaliona na ikiwa mizimu itakupenda utaliona. Ukifika unachinja mnyama uliyeenda naye na kumwaga damu yake ndani ya maji na nyama mnachoma na kula na kutupia nyingine ndani. Kisha unaomba ukitakacho iwe UTAJIRI, UGANGA WA JADI, UCHAWI nk.
 
HISTORIA YA WAPARE!!
Wapareni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, TavetanaUkamba. Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.

Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi anaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisherani wa Kikiristo waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru, Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisla la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisala la Kiluteri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Waluteri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Gonja Kighare, Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga manake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baade na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale

Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mv ungi,Msuya,Mgonja etc, wana asili ya maeneo yao kama Bwambo,Mjema,Usangi,Vungi,Suya ,Gonja etc.

Mifano ya majina ya watoto wakipare

Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Naman gi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.

Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli, Chikira, Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibarik i,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa , Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.
Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikwepoa hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven(JB),Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.

Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande(mchanganyiko wa mahindi na maharage).Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bilaa kuwaza masuala ya upishi.Samaki pia ni kipenzi cha wapare wengi na ndio maana utawasikia watani wao wakuu yaani wachaga wakiwatainia kuwa wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki wakimaanisha kuwa ni wabahili.Wakati mwingine utawasikia wapare wenyewe wakisema "ipere ethi kindu,kindu ni mshombe"kuwa samaki si kitu kitu ni mchuzi kuonesha ubahili wao kuwa samaki anayebaki atumike tena wakati mwingine bqaada ya mchuzi kuisha.
Maeneo ya wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi yanavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya upareni kadhalika.Kuna maeneo yanayovutia kama milimani(Usangi,ugweno,misitu ya shengena n.k.Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua.

Kama ilivyo kwa makabila mengine wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya ya elimu,siasa na uchumi.Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya wapare.Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,katani,mahindi n.k zimeinua maendeleo ya uchumi.Pia Miundo mbimu kwa kiasi chake imeboreshwa,kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro,pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika Kwa upande wa siasa wapo pia wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja ya siasa kama Mh.Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Wjaziri Mkuu,Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe na pia Waziri,na wengineo wengi kama Anna KIlango Malechela,Pro.Jumanne Maghembe,Michael Kadeghe n.k Pia Mheshimiwa Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwnasiasa maarufu hapa nchini(waweza ongeza).

Waweza ongeza kuiedit ili kuiweka historia ya wapare vyema na kujua tulipotoka na sasa Wapare wapo wapi kwani vitu vingi vimebadilika.Edit na kuongeza historia unayoifaham ukiwa vna uhakika ili ikae mtandaoni wikipedia
 
Back
Top Bottom