Mifano ya majina ya watoto wakipare
Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)
Ingiahedi(ingia pazuri) Msianze usisimkwa au kutoa maana tofauti, Gaijin umenisikia!
Itikija(Kibwagizo)
Komkwavi(Mkwavi ni mmasai hapa akimaanisha binti Mkwavi, mwanaume ni Mkwavi)
Mchikirwa( Aliyesusiwa, hapa single mother ndipo hasa,kama mtu kasepa hakuna DNA wewe unaita Mchikirwa)
,Mshinwa( Mwenye haya au haiba), Naanjela(Asifiwaye), Naetwe( Aliyeletwa), Nahuja( Mkimya),
Nakadori( kadogoo), Nakiete( Wasokoni), Nakijwa(Alieyeponywa), Nakunda( Loveness), Nakundwa(Aliyependwa) ,Namkunda(Nimempenda) ,Nangasu( wa sherehe),Nanzano( wa kiangazi) , Narindwa( Nalindwa), Nasero, Nashumbwe, Natujwa( Nimefarijika) , Navuri( wa vuli) ,Nghuhia(Nipokee), Niendiwe( Niliyetafutwa), Nietiwe(Niliyeletewa), Ntevona(Nimeona) n.k
Majina ya kiume:
Bunija( Dumisha) Charema( Kilichoshindikana) , Chedieli( mungu mwema) ,Chuma, Eliesikia(Mungu msikivu) ,Elinighenja(Mungu nisaidie) ,Elibariki(Mungu bariki) ,Elitumaini(Amtumainiye mungu) ,Ghuheni(Chukueni), Gurisha(Aliyeshika hasa katika imani) , Ibwe(Jiwe), Kakore(Kigogo) , (Mbuzi), Mding'i, Mgheni, Mshigheni(Mwacheni), Ngasu(celebrity) , Nzao(Fahali la ng'ombe) , Nziajose(Njia zote), Nziamwe(njia moja), Senzia(Wa ,Twazihirwa(Tumefurahi) Zihirwa(Furaha), Zihirwani(Furahini) n.k.
Majina hayo mengine yametojana na maneno ya dini. Wapare waliandika Bibilia ya lugha yao wakati wa ukoloni na waliweza kwenda kanisani na kusali kwa kutumia biblia yao. Jambo moja la kushangaza, kama ilivyo katika vitabu vya dini, lugha ya kipare katika biblia ni ngumu sana kuielewa hadi apatikane mtu anayeweza kufafanua. Hilo pia lipo katika vitabu vyote vya dini zote vilivyotafsiriwa.
Wapare wana koo na koo zingine zina umaarufu wa aina fulani
Wasuya ni koo ya utawala
Washana ni wahunzi na kama ni kizungu hawa wanaitwa ''smith'' iwe iron smith, Gold smith etc.
Watu wakumbuke kuwa jina Smith kwa kizungu ni koo ya wahunzi.
Wambaga ni maarufu kwa kuleta mvua.
Majina hayo pia yametafsiriwa kiswahili. Kwa mfano Ziharwani kwa kiswahili ni Furahini na aghalabu ukiwa kule kwao utasikia sana jina la Furahini. Pia, Nkundiwe ni kama pendo na siku hizi utasikia sana Pendo au loveness.
Uzuri wa majina haya ya asili ni ile hali ya uasili na maana ya jina.
Hata siku moja hutasikia mtu anaitwa Msuya Mshana, au Mbwambo Mbaga, au Mziray Mdeme. Maana yake ni kuwa haya ni majina ya koo na huwezi kuwa na jina la ukoo kwa ubini wa ukoo.
Ikumbukwe kuwa ukisikia mtu anitwa Msuya, basi lazima anajina kwa wazungu Msuya ni Sir Name.
Kutokana na kuiga majina ya nje sikuhizi utasikia mtu anaitwa Martin Wallace Smith, hii ni sawa na kumuita mtu Msangi Mshana Msuya ambayo haina maana. Hili ni tatizo la waafrika. Tena lipo pande zote.
Kwa waislam mtu atajiita Said Abudulah Kharef, ukiangalia hayo ni majina ya koo.
Mimi napenda sana Majina kama ya akina Kokubanza, kokushubirwa, Navonaiwa, Nkundiwe, senzota, Mahiza( kule nyumbani Tanga), Semahonge, Mhina, Makame, Akida, Shetui, Mchili, Mwakifufule, Mwaigomole, Ng'abi, Odera, Onyango, Mwita, Wambura.
Kule kwetu Kicheba na mjasani Tanga majina ya asili yanatoweka sasa! Mwaka jana nilipofika Magoroto, Mkanyageni na Lusanga hadi Mtindiro nilishangaa majina yamekuwa imported yote.
Just to add spices, thank you mleta mada
.........