Ijue huduma ya Kinabii

Ijue huduma ya Kinabii

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!
Shalom
Kuna huduma kuu 5 ambazo ni Utume, unabii, Uchungaji , ualimu na Uinjilisti.
Kwasababu ya watu kukosa MAARIFA ya ndani juu ya huduma wengi huishia kujiita Wachungaji, Walimu na Wainjilisti. Kuna watu wanafanya huduma ambazo hawakuitwa kwazo, kuna watu wanaogopa kufanya huduma ya kinabii au kitume ingawa wameitwa kwazo kwasababu hawakumpata mentor wa kuwafungua ufahamu juu ya huduma zao , sometimes Mungu amewaita na wanethibiisha lakini wachungaji wao wamekuwa kwazo.
Ukijiita mwinjilisti kanisa au jamii wala haishituki, ukijiita mwalimu pia jamii ya kanisa haishituki the same ukijiita mchungaji.
Ila siku ukijiita Mtume au Nabii kanisa litahamishia vita nyumbani kwako.
Kwanini?
Mungu hawezi kukupa kitu ambacho hukifahamu, kwakuwa wengi wamefunga fahamu zao na kukosa MAARIFA juu ya hizo huduma 2 ambao zinaonekana zina mvuto na kuwa tishio kwa Huduma ya kichungaji basi wachungaji wengi wametamatisha kuwa hakuna huduma ya kinabii sasa na wanasema kila mmoja anaweza kuwa nabii. Big no.
Mungu sio chizi
Karama ya kinabii ambayo haiwi permanent ndani ya mkristo ndio inaweza kufanya kazi kwa kila mkristo aliyejawa Roho Mtakatifu lakini huduma ni kwa waliopewa tu. Ni ofisi yao ya kudumu.
AINA ZA MANABII
Kuna aina kuu 3 za manabii
1.Unabii ambao mtu anazaliwa nao.
Mfano: Jeremia, Yohana mbatizaji, n.k
2. Nabii wa kuitwa
Mfano : Amosi
3. Nabii wa kuwa mfuasi (mpambe)
Mfano: Elisha
Kwanini nabii anaweza kuona future, past na present ya mtu bila kuambiwa?
Jibu: Mbele za Mungu vitu vyote ni past . Yaani kwa Mungu hakuna kipya, yote yametendeka. Hivyo nabii ili atabiri anakuwa na uwezo wa kufanya forecasting ya maisha ya mtu.
Nabii ni sauti ya Mungu kwa wanadamu huku kuhani /mchungaji ni sauti ya watu kwa Mungu.
Iko hivi : Mchungaji anatoa ya wanadamu kupeleka kwa Mungu huku Nabii anatoa ya Mungu kuleta kwa wanadamu.
Yeyote anayetaka kuwa nabii anaweza kuwa nabii kwa mujibu wa aina 3 nilizoweka hapo juu.
Pia kuna makundi ya manabii
A. Manabii wadogo
B.Manabii wakubwa.
Acha wivu juu ya huduma ya kinabii unajilaani wewe mwenyewe na kizazi chako.
Note: Wapo wachungaji wa uongo, mitume wa uongo, walimu wa uongo, Wainjilisti wa uongo na manabii wa uongo lakini kwakuwa watu wamekosa maarifa wameishia kusema manabii wa uongo tu huku wakiacha makundi mengine yaendelee kulipotosha kanisa.
Sijaweka andiko hata moja. Kama kutakuwa na swali nitajibu kwa kunukuu maandiko.
Pia anayetaka kuwa nabii nitamfundisha bure.
 
Hello!
Shalom
Kuna huduma kuu 5 ambazo ni Itume, unabii, Uchungaji , ualimu na Uinjilisti.
Kwasababu ya watu kukosa MAARIFA ya ndani juu ya huduma wengi huishia kujiita Wachungaji, Walimu na Wainjilisti.
Ukijiita mwinjilisti kanisa au jamii wala haishituki, ukijiita mwalimu pia jamii ya kanisa haishituki the same ukijiita mchungaji.
Ila siku ukijiita Mtume au Nabii kanisa litahamishia vita nyumbani kwako.
Kwanini?
Mungu hawezi kukupa kitu ambacho hukifahamu, kwakuwa wengi wamefunga fahamu zao na kukosa MAARIFA juu ya hizo huduma 2 ambao zinaonekana zina mvuto na kuwa tishio kwa Huduma ya kichungaji basi wachungaji wengi wametamatisha kuwa hakuna huduma ya kinabii sasa na wanasema kila mmoja anaweza kuwa nabii. Big no.
Mungu sio chizi
Karama ya kinabii ambayo haiwi permanent ndani ya mkristo ndio inaweza kufanya kazi kwa kila mkristo aliyejawa Roho Mtakatifu lakini huduma ni kwa waliopewa tu. Ni ofisi yao ya kudumu.
AINA ZA MANABII
Kuna aina kuu 3 za manabii
1.Unabii ambao mtu anazaliwa nao.
Mfano: Jeremia, Yohana mbatizaji, n.k
2. Nabii wa kuitwa
3. Nabii wa kuwa mfuasi (mpambe)
Mfano: Elisha
Kwanini nabii anaweza kuona future, past na present ya mtu bila kuambiwa?
Jibu: Mbele za Mungu vitu vyote ni past . Yaani kwa Mungu hakuna kipya, yote yametendeka. Hivyo nabii ili atabiri anakuwa na uwezo wa kufanya forecasting ya maisha ya mtu.
Nabii ni sauti ya Mungu kwa wanadamu huku kuhani /mchungaji ni sauti ya watu kwa Mungu.
Iko hivi : Mchungaji anatoa ya wanadamu kupeleka kwa Mungu huku Nabii anatoa ya Mungu kuleta kwa wanadamu.
Yeyote anayetaka kuwa nabii anaweza kuwa nabii kwa mujibu wa aina 3 nilizoweka hapo juu.
Pia kuna makundi ya manabii
A. Manabii wadogo
B.Manabii wakubwa.
Acha wivu juu ya huduma ya kinabii unajilaani wewe mwenyewe na kizazi chako.
Note: Wapo wachungaji wa uongo, mitume wa uongo, walimu wa uongo, Wainjilisti wa uongo na manabii wa uongo lakini kwakuwa watu wamekosa maarifa wameishia kusema manabii wa uongo tu huku wakiacha makundi mengine yaendelee kulipotosha kanisa.
Sijaweka andiko hata moja. Kama kutakuwa na swali nitajibu kwa kunukuu maandiko.
Pia anayetaka kuwa nabii nitamfundisha bure.
naomba tutajie nabii wa kweli hata mmoja tu hapa Tanzania.
 
Nimepitw kwa mwamposa.nasikia ushuhuda kuna mtu kabarikiwa kwenye biashara yake mpaka anawakimbia wateja😁😁😁.
Kuna mwingine anasema siku anakwenda kwa mwamposa alienda kwa usafiri wa kuunga unga,akaandika kumuomba mungu ampe biashara na anunue magari,sasa hivi ana biashara na magari.😁😁😁.
Mimi uwa napita tu
 
naomba tutajie nabii wa kweli hata mmoja tu hapa Tanzania.
Hapo unataka nifanye kazi ambayo shetani anaifanya .
Ukweli au uongo wa kwanza kuujua ni mtu mwenyewe.
Kwahiyo Nabii yeyote muulize kuwa wewe ni nabii wa MUNGU au wa shetani na mwambie aape kwa Mungu wa mbinguni kama kweli kamtuma.
 
kwa hiyo sisi hatuwezi kuwatambua kwa matunda yao? mfano, hao wanaojiita manabii wakuu, ila wanapinga Biblia na kuiquestion credibility yake, na wengien wengi wanaopiga pesa. walinganishe hao na Nabii Yoel, Nabii Musa, Nabii Daudi, Nabii Eliya Mtishbi, Nabii Elisha na Isaya. Isaya angekuwepo hapa leo, angefanana na hao wa instagram? eliya au elisha angekuwepo wangefanana na hawa?

kama MKristo, sipingi kwamba hata leo manabii wapo, wapo ila wachache sana, wengi wao mnatakiwa kusoma Biblia ili muwatambue kwa matunda yao. hata Mungu hawajui. Nabii anazunguka mwaka mzima hajawahi kufundisha waumini wake kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu ambaye hakuna atakayestahimili bila yeye, anazingatia tu matoleo na uhuni.
 
Binafsi naona ni vyema tuhubiri Injili kuliko kupoteza muda kusema huyu nabii wa uongo au huyu wa Mungu.
Huduma yoyote kama haileti watu kwa Yesu hiyo haijazaa, itakatwa.
Huduma ya kinabii ni huduma muhimu sana katika zama hizi za giza ila kwasababu ya umuhimu wake shetani anawatia watu giza wasiijue na kuitambua.
Kanisa kama halina nabii hilo kanisa linapigwa na Ibilisi muda wowote
 
hapo umekosea, kwamba kanisa kama halina nabii linapigwa wakati wote? usilinganishe enzi za agano la kale ambazo Roho Mtakatifu alikuwa haishi ndani ya mtu na enzi hizi ambazo Mungu mwenyewe anaishi ndani yetu na anaweza kuongea na sisi bila kupitia nabii. jiulize kwanini zamani watu walikuwa wanafuata kwenda kusikia toka kwa nabii? na kwa nini leo hii Yesu alituambie tutapokea Roho Mtakatifu atakayekuwa mwalimu na kiongozi, alimaanisha kiongozi na mwalimu kwamba tutegemee toka kwa mtu mwingine? au yeye anakuwa ndani yetu? na je? manabii wa sasaivi watakuwa type ile ya eliya na elisha na isaya au ni tofauti? mtu ambaye amejazwa Roho na anaongozwa na Roho atahitaji kusikia toka kwa nabii muda wote?

hao wanaotembea na machawa, mapapaaa wanaojifanya kubashiri, mara kaka yako ana jina herufi K, mara anafanya kazi fulani? nao tuseme ni unabii? na tuwaite manabii? hawa hawa wanaovaa kisharobaro na kutembea na mabodigadi.
 
Back
Top Bottom