Last time nilisoma hii kitu kutoka kwa mkuu
Kithuku miaka mingi iliyopita,jikumbushe kidogo jibu lake kwa mkuu
hamisi Kigwangala-->
Kithuku
February 12, 2008 at 2:10 AM
Nimeona ni vema nirudi kujibu maswali ya baadhi ya wadau hapa. Orodha ya freemasons duniani ni ndefu sana. Ikumbukwe wamekuwako tangu karne nyingi zilizopita, lakini ujasiri wa kuji-organize na kuendesha shughuli zao kama kundi una miaka kama 300 hivi. Katika miaka hiyo, wale wenye vyeo vya juu katika jumuiya yao wamefikia hatua ya kutoficha tena uanachama wao. Kiutaratibu, mwanachama hupanda ngazi taratibu ambazo huitwa "degrees", na ziko degree 33. Wale mabosi wa juu huwa ni "33rd degree masons", hao ndio wenye siri zote za kundi. Wale wa degrees za chini mambo mengi hawayajui.
Nianze na orodha ya freemasons maarufu duniani. Kwa heshima ya Dr Hamisi Kigwangalla aliyeanza kuuliza swali hili, naona nimwanzie na madaktari wenzie: Dr Edward Jenner aliyegundua "vaccination" alikuwa freemason maarufu (haimaanishi chanjo ni mbaya, la hasha!). Wengine ni Drs William na Charles Mayo, waanzilishi wa kliniki maarufu ya Mayo huko Marekani (Dr utakuwa unazo habari za hii kliniki bila shaka au utakuwa umesoma machapisho yake wakati wa training yako, maana ni maarufu sana pia katika ufundishaji wa madaktari).
Gen Mustafa Kemal Ataturk, shujaa mwanzilishi wa taifa la Uturuki pia ni miongoni mwa waliokuwa katika orders za juu sana. Kule Uturuki mtu akitaka kushinda uchaguzi anajinadi kuwa anamuenzi Ataturk, na ukitaka kukosana kabisa na waturuki basi watukanie huyu General. Uhusiano kati ya Uturuki na madola mengine yaliyokubuhu katika freemasonry uko wazi, mwenye interest afuatilie atathibitisha.
Viongozi maarufu wa kidini (hapa nataja wale waliowahi kukiri katika maisha yao na walioorodheshwa rasmi na freemasons wenzao, wale wa tetesi-ambazo pia zaweza kuwa kweli-nimewaacha, na wako wengi pia): ni pamoja na Rev William Booth (mwanzilishi wa Salvation Army), Fr Francisco Calvo (padre mkatoliki aliyeanzisha tawi la freemasonry huko Costa Rica mwaka 1865), Rev Jesse Jackson (mwanzilishi wa RainBow Coalition), Aga Khan (aliyekuwa kiongozi wa madhehebu ya Ismailia, aliishi 1877-1957), Aga Khan III (sina uhakika kama huyu ndiye Prince Aga Khan wa sasa, atakayepata data zaidi anaweza kutuongezea hapa). Kuwapa clue zaidi kuhusu hawa watu, angalieni uhusiano wao na serikali (wana nguvu sana). Mnakumbuka nani alikuwa spiritual advisor wa Bill Clinton wakati wa kashfa yake na Monica Lewinsky? Yote niliyotaja hapa si ya siri, hawa ni wale ambao walikuwa hawafichi tena chochote!
Freemasons wengine maarufu ni kina Thomas Watson (angalia computer yako kama imeandikwa IBM, ndiye mwanzilishi), J.Edgar Hoover (mkurugenzi wa FBI). Orodha nzima ya hawa kwa mujibu wa website ya masonic Lodge no.406 inapatikana kwenye ukurasa huu:
http://www.calodges.org/no406/FAMASONS.HTM
Freemason mwingine maarufu ambaye anataka kukamilisha kazi ya kuwawekea binadamu wote alama ili iwe rahisi zaidi kuwakontrolu (kwamba asiyekuwa na alama hii hataweza kushiriki manufaa ya ulimwengu huu ambayo yatakuwa ni makubwa sana) ni Rockfeller, tajiri mwenye Foundation/Institute inayo-sponsor mambo mengi ya maendeleo duniani. Rockfeller na freemasons wenzie wana vision yao ya wanachokiita "New World Order" (pata details hapa: Downloads). Katika vision hiyo, Rockfeller anapendekeza mradi wa kuwawekea binadamu wote "microchip" mwilini, ili rekodi za kila binadamu ziweze kufuatiliwa katika computer moja ulimwenguni kote, na ziwe accessible kupitia connection ya satellite. Kwa hiyo hicho ki-microchip kinakuwa na unique identification number kwa kila mwanadamu (kama zile identification codes za bidhaa kwenye supermarkets), ukipita popote hakuna haja ya kuulizwa kitambulisho, hiyo microchip ndiyo access code. Asiye na microchip akitaka kupita kama ni kwenye huduma (airport, hospitali, maktaba etc) milango inakataa kufunguka! Kwenye hospitali huhitaji kutaja jina lako, ukiingia tu chumbani kwa daktari, kuna chombo kinasoma microchip iliyoko mwilini mwako, mara moja rekodi zako zote zinatokea kwenye screen ya computer ya daktari! Hakuna kuulizana majina, sijui umri nk. Mengi kuhusu mradi wa microchipped population yanapatikana hapa: Illuminati News: Rockefeller Admitted Elite Goal Of Microchipped Population.
Wasioelewa athari za hiyo microchipped population wanaweza kudhani ni maendeleo makubwa haya! Sivyo ndugu zanguni, ni mbinu ya kuwaingiza watu wote kwenye freemasonry kwa lazima (maana kila asiye na alama hiyo atakosa huduma muhimu). Kwa taarifa yenu huu mradi umeshajaribiwa kwenye wanyama kama mbwa na umeonekana kuwa unafanya kazi kama inayokusudiwa (rejea:
Does Microchipping Dogs and Cats really work?). Ukiwa na hiyo microchip implant mwilini mwako, wanaweza kukufuatilia popote ulipo na chochote unachofanya kwa wakati huo kupitia satellite (hata ujifiche wapi!). Huku UK kuna campaign za kupinga kitu hicho ambacho watu wanahisia kinakusudiwa kuanzishwa katika miaka 10 ijayo. Lakini kutokana na mradi wenyewe kuwa hi-tech, ni wachache wanaoujua, na hata kampeni za kuupinga ziko kwenye mtandao wa internet zaidi ambako watu wanaombwa ku-sign petition kuupinga. Details hapa:
http://web.ukonline.co.uk/mandrob/html/id_cards_microchipped_populati.html
Freemasons wa Tanzania? Waliojitokeza waziwazi na wanaojitambulisha ni kina JK Chande "Andy Chande" ambao ni matajiri wafanyabiashara maarufu. Katika mahojiano aliyofanya na mwandishi Muhiddin Michuzi wa gazeti la Sunday News la tarehe 3 April 2005, Sir Andy Chande alikiri kuwa anao wanachama zaidi ya 3,000 (yeye mwenyewe ni District Grand Master), na kuwa wamekuwa wakishirikiana na Rais Yoweri Museveni, Makamu wa Rais wa Kenya Moody Awori, na Rais Mstaafu Ben Mkapa (hakutaka kutamka wazi kuwa ni wanachama, lakini wapo watu wengine wanaofahamu kuwa hao aliowataja ni wanachama wa hiyo kitu, pamoja na Mzee Mengi).Alitamka kuwa mtu yeyote akishajiunga na freemasonry hawezi kutoka tena, kwa maneno yake "Once a freemason, always a freemason".
Tazama jibu la Sir Andy Chande alipoulizwa na Muhiddin Michuzi kuhusu yalipo makao makuu ya Freemasons nchini Tanzania: "It is located along Sokoine Drive, just behind the Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam. We have a licence to sell drinks to members; we have also been exempted by the government of Tanzania from registration We have the full blessings of the government. Once that
building was about to be taken over for public purpose, but when I sent a memorandum to the State House, we got it back. You know, Mwalimu Julius Nyerere was not a Freemason, but he knew what Freemasonry is".
Soma hilo jibu uniambie, ni nguvu za kawaida hizi walizo nazo juu ya dola? Ni zaidi ya kawaida! Wameruhusiwa wasisajiliwe (wajua lengo lake? Ili msajili asiwe na madaraka ya kuhoji shughuli zao au kukagua chochote! Nitajie NGO nyingine iliyoruhusiwa kufanya kazi bila usajili!) Nyerere alivyokuwa mkali wakati wa Azimio la Arusha 1967, ati walimtumia "memorandum" huko ikulu kuwa asitaifishe jengo lao, na akatii! Hawa watu bwana achaneni nao. Haya mahojiano ya Chande na Michuzi yalichapishwa kwenye gazeti la Sunday la tarehe 3 April 2005. Wakati huo Mkapa alikuwa madarakani, kwa hiyo tunaweza kuwa na uhakika hakuna alichompakazi