Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Yah ndiyo kipindi hicho.
Wana prince wao mmoja bishoo sana kila birthday huwaalika wanamziki mashuhuri wa marekani na kuwalipa maela mengi.
Ashawahi kumwalika usher raymond akamlipa ela nyingi na kumpa viatu vimenakshiwa kwa almasi, mariah carley, paris hilton na wengine kibao.
Pia mfalme wa brunei aliwahi mkodishia kinyozi ndege toka uingereza aende kumnyoa nywele.
Yule prince anakula bata ya hatari niliona wakati usher anakabidhiwa ile snicker alikua haamini anatoa meno tu! pia huyu dogo no miongoni mwa young billionaires duniani!
 
Huko nasikia kwa MTU asiye raia hususan kutoka Afrika ili akubaliwe ni aidha aoe mlemavu au awe na taaluma inayohitajika sana huko,,ukioa mlemavu ambaye amekosa mume huko unapewa stahiki zote kama raia wa hiyo nchi!!unakula maisha tu,ukirudi huku unakuta ndugu zako wote washakuwa makini maana washapitiliza ushetani!
 
Na tanzania ni ya pili duniani ambayo wananchi wake hawali pi kodi wazazi wakienda hospital hula la sakafuni hawalipi kodi wazee hulipwa maneno elimu bure lakini hulipi unafukuzwa rain wake wanapo oa serekali huwa pa risiti ni nchi yenye waenda kwa miguu na yobayoba rais wake ndie anae milk kila kitu ni rais wa kwanza duniani anae wasomesha namba raia wake
 
Kwa kuongezea tu,Kasri la sultan ndio nyumba ya gharama kuliko ya kiongozi yeyote duniani.
Na mwana sultan kwa kipindi fulani alikuwa akisoma nchini Uingereza na alikuwa ananunua urafiki na masuper stars mbali mbali kwa kuwapelekea vito vya thamani na pesa, kuna kipindi alimnunulia Usher raymond sneaker yenye nakshi za almasi.
 
Nakumbuka kibao cha JB MPIANA kiitwacho Sultan de Brunei akimsifu sana sultan huyo kwa urafiki wao.
 
Si bure! Hapo ni Sharia inafanya kazi ndio maana mambo yanakwenda, Wakiingia Mishetani ya Kimagharibi kama walivyoingia Libya mambo yanaharibika

Sahihi kabisa huwo ndio uhondo wa utawala wa shariah maanayake watawala nao kumuogopa mungu, sio hapa tunadanganyana, natumbua mjipu nafukua makaburi. Halafu ooh eti makaburi mengine hayafukuliki. Usawa uko wapi?
 
FAHAMU ZAIDI..
1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu.
Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.
GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....
2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).
Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.
3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali
4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................
5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei
6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk..........
7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali
8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)...mwenye kujua zaidi kuhusu hii nchi atujuzee...vip tanzania nasi tunaweza kufata mfumo kama huu wa brunei..?
 
na siku si nyingi unaingia stage ya jini.........


Unachanganya mambo.

Jinni ni kiumbe ambae wapo wengine wao ni mashetani. Kama ilivyo kwa binaadam, wapo wengine ni mashetani.

Shetani si lazima awe ni katika majinni, wapo binaadam mashetani, mfano huyu mchungaji:

nigeria-abus-pasteur.jpg
 
Back
Top Bottom