Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Typographical error mkuu

Hiyo ya hemisphere sijaielewa hata mm ndio mana nimecite source boss!
Nchi zote ambazo zimepitiwa na mstari wa Ikweta zipo katika northern na southern hemisphere. Uganda na Kenya zijiwemo.

Huyo aliyeandika hiyo habari hajui Jiografia.
 
Kuna mdogo wake sultan alishawahi spend usd 750,000/day in one year..uzuri wao nchi nzima ni km familia tu
$750,000 in one year si kitu cha ajabu.

Kuna watu si masultani wala nini wanaspend hiyo hela over a weekend.
 
750,000/day for a year..alishawahi alika miss Amerika aje adansi tu kwa malipo ya usd3000/saa
 
Ok, 750,000 a day for one year that is something else.

Ulikuwa hujafafanua hiyo "a day for one year". "In one year" na "for one year" zina maana mbili tofauti.
 
1. Nchi ya kiislam iko chini ya sultani, ukubwa km 5786sq ina watu 438,720 tu mpk Feb 2016

2. Free education, free health, ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiwno mkubwa wa watu na magari (1:209)

3. Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba ty hutumika kupoint kitu

4. Sultan Hassanal Bolkiah, ni wa 29 anamiliki magari zaid ya 5,000 ya kifahari;
20 Lamborghinis,
160 Porsches,
130 Rolls Royces,
360 Ferraris,
170 Jaguars,
180 BMWs,
360 Bentleys, and 530 Mercedes-Benzes.

5. 93% ya watu wote wameenda shule au wanasoma

6. Marufuku kuuza au kununua au kunywa pombe hadharani

7. Hakuna nguruwe hata 1 nchi nzima

8. Nchi pekee iliyo northern & southern Hemisphere

9. Mwaka mzima ni joto ikiwa na relative humidity ya 93% na mvua ni ya kutosha

10. Per capital income ni usd~39,970

11. Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

12. Brunei ni nchi ambayo watu hawalipi kodi yeyote-tax free country

13. Sultani wa sasa bi ukoo uliotawala kwa miaka 600

#kwa_hisani_ya_google & personal visit
Planet x unakuta kutumbua Lamborghini zote[emoji15] [emoji15] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Uwiano wa 1:209 ni mkubwa kivipi?

Uwiano mkubwa ni 1:1

Halafu, namba 8 "nchi pekee iliyopo northern and southern hemisphere" unaelewa umeandika nini? Ushawahi kutazama ramani ya dunia?
Kwamba uwiano wa watu na magari ni 1:209? Kama ndivyo inamaanisha kuna wastani wa magari 209 kwa kila mtu mmoja. Kwa hiyo ni sahihi kwamba uwiano wa 1:209 ni mkubwa zaidi ya ule 1:1 uliodai kuwa ndiyo mkubwa kwa sababu tafsiri ya uwiano wa 1:1 ni kwamba kwa kila mtu mmoja kuna gari moja.
 
Unajua kua Bruney mwanamke hapigi kura mpaka leo? Hiyo ni haki kweli? Mwanamke anatakiwa kuazwa kwenye mazungumzo na sio yeye kuanza

Hijabu is a dress code to any woman plus visitors haaa ww jamaa
Sasa ndugu yangu unataka wanawake wapige kura wamchague nani wakati hii thread ni wewe mwenyewe ndie umeleta na umeshasema inatawaliwa na Sultan! Sasa ushawahi kuckia Sultan anapigiwa kura?!

In short, sio wanawake tu bali suala zima la election Brunei halipo!
 
Kwamba uwiano wa watu na magari ni 1:209? Kama ndivyo inamaanisha kuna wastani wa magari 209 kwa kila mtu mmoja. Kwa hiyo ni sahihi kwamba uwiano wa 1:209 ni mkubwa zaidi ya ule 1:1 uliodai kuwa ndiyo mkubwa kwa sababu tafsiri ya uwiano wa 1:1 ni kwamba kwa kila mtu mmoja kuna gari moja.
Unafahamu maana ya uwiano? Uwiano maana yake ni mlinganyo wa vitu viwili, anything that deviates from 1:1 is disproportional.

Uwiano ni mlinganyo unaolinganisha pande mbili. Ukisema "uwiano ni mkubwa" maana yake unasema usawa wa pande mbili ni mkubwa.

Katika uwiano wa 1:209 uwiano si mkubwa, kwa sababu hakuna usawa kati ya watu na magari. Kama kuna magari 209 kwa kila mtu mmoja hakuna uwiano mkubwa, kuna kutowiana kati ya watu na magari.

Halafu hiyo ratio ni ya uongo.

Will cars outnumber residents in Brunei?

"Brunei has one of the world's highest car ownership rates in the world, with 2.65 people per vehicle, according to the Department of Economic Planning and Development. There were 148,186 vehicles registered with the Land Transport Department in 2011, an increase of 30 per cent from the previous year."

Hiyo ratio imetokaje 2.65 people per car in 2011 to 1 person per 209 cars now?

Inaonekana aliyeandika amejitungia tu mambo.
 
1. Nchi ya kiislam iko chini ya sultani, ukubwa km 5786sq ina watu 438,720 tu mpk Feb 2016

2. Free education, free health, ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiwno mkubwa wa watu na magari (1:209)

3. Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba ty hutumika kupoint kitu

4. Sultan Hassanal Bolkiah, ni wa 29 anamiliki magari zaid ya 5,000 ya kifahari;
20 Lamborghinis,
160 Porsches,
130 Rolls Royces,
360 Ferraris,
170 Jaguars,
180 BMWs,
360 Bentleys, and 530 Mercedes-Benzes.

5. 93% ya watu wote wameenda shule au wanasoma

6. Marufuku kuuza au kununua au kunywa pombe hadharani

7. Hakuna nguruwe hata 1 nchi nzima

8. Nchi pekee iliyo northern & southern Hemisphere

9. Mwaka mzima ni joto ikiwa na relative humidity ya 93% na mvua ni ya kutosha

10. Per capital income ni usd~39,970

11. Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

12. Brunei ni nchi ambayo watu hawalipi kodi yeyote-tax free country

13. Sultani wa sasa bi ukoo uliotawala kwa miaka 600

#kwa_hisani_ya_google & personal visit
UMESAHAU...
Ni Nchi ya kiislamu, ambayo raia 90% ya raia wake wameisha enda HIJJA. mipango ya hija na gharama za hija hufanywa na serikali, uratibu wa kwenda hijja huanzia mama anapobeba mimba.
NI Nchi isiyokuwa na polisi ama pia kiwango cha uhalifu ni 0%.
 
Unafahamu maana ya uwiano? Uwiano maana yake ni mlinganyo wa vitu viwili, anything that deviates from 1:1 is disproportional.

Uwiano ni mlinganyo unaolinganisha pande mbili. Ukisema "uwiano ni mkubwa" maana yake unasema usawa wa pande mbili ni mkubwa.

Katika uwiano wa 1:209 uwiano si mkubwa, kwa sababu hakuna usawa kati ya watu na magari. Kama kuna magari 209 kwa kila mtu mmoja hakuna uwiano mkubwa, kuna kutowiana kati ya watu na magari.

Halafu hiyo ratio ni ya uongo.

Will cars outnumber residents in Brunei?

"Brunei has one of the world's highest car ownership rates in the world, with 2.65 people per vehicle, according to the Department of Economic Planning and Development. There were 148,186 vehicles registered with the Land Transport Department in 2011, an increase of 30 per cent from the previous year."

Hiyo ratio imetokaje 2.65 people per car in 2011 to 1 person per 209 cars now?

Inaonekana aliyeandika amejitungia tu mambo.
Mkuu ahsante kwa masahihisho. Nilisahau kwamba kwa kadri tofauti kati ya vitu viwili vinavyolinganishwa inapokuwa kubwa ndipo uwiano wake unapokuwa mdogo zaidi.
 
Jerrymsigwa unajua haramu tamu? Tena raha ya pombe inywewe kunako kadamnasi, thanka God kwa kuzaliwa kwangu Tz
Mkuu wangu maneno haya si mazuri kumbuka muumba wa mbingu na ardhi hapendi, nadhani wajua pia kwamba hiyo tamu ya haramu hugeuka chungu zaidi ya shubiri pale unapokamatwa.
 
Sasa ndugu yangu unataka wanawake wapige kura wamchague nani wakati hii thread ni wewe mwenyewe ndie umeleta na umeshasema inatawaliwa na Sultan! Sasa ushawahi kuckia Sultan anapigiwa kura?!

In short, sio wanawake tu bali suala zima la election Brunei halipo!
Mkuu kura sio raisi tu, hata monitor darasani anapigiwa kura.
 
Nchi inakosa mahitaji muhim. Kilaji, mkuu wa meza haiyamkini hata 'mambo yenu yale' hakuna!
 
Back
Top Bottom