Ijue MECCO ya Mbeya

Ijue MECCO ya Mbeya

Itakuwa Omary Jongo au Abubakary Liyongo, walikuwa na mbwembwe hao lkn mwisho wa mbwembwe alikuwa Dominick Chilambo (RIP) alikuwa anaipamba pamba hadi raha, kama bado hujaingia uwanjani unasikiliza kwa radio unatamani upae, manake ukiangalia msululu ulivyo mrefu na geti lilipo unahisi utakuta mpira ushaisha
Ukisikia anamtaja Kitwana Suleiman mara tatu ujue kuna goli hapo
 
  • Thanks
Reactions: ram
Asante kwa kumbukumbu nzuri. TFF hawana records, poor them.
Nataka nitengeneza database archive ya soka LA Bongo
Acha Urongo.... Una uhakika na unachokinena? ni uchochezi kuandika kitu ambacho huna uhakika nacho....Yaani TFF au FAT zamani wakose Kumbukumbu za timu zao za ligi? Mabwaku haya ya karne. ila Record zipo Nikienda Arusha nikikutana na Rashid Chama ana mapicha kibao sana hadi walipoenda na timu ulaya na mataifa kibao Africa anazo... Mtafute atakusaidia Sana Kocha.

Kwanza Huyo Abeid Kasabalala ni mchezaji beki hiyo ya winga nawasiwasi nayo maana namfahamu vizuri yupo anaishi Kiwalani na ni Mjumba wa Mtaa huko kwake na huwa anamashindano yake ya ndondo ya kikampeni ccm damu damu.
 
Rashid Chama ni TFF?
 
Long live jf, Lipuli wanapaluhengo, Iringa tuliingia kwa mbwembwe toka mikoani enzi hizo chuo cha NBC kiko Iringa, ukirudi Songea kwa wangoni ipo Majimaji wacha mchezoo mpira unachezwa huku wana njata njata wanakuburudisha, ukija Mwanza kinehe bha gishimba enzi zile iko pamba walikua wanachangiwa pesa na wakulima karibu mkoa mzima.
 
Coastal ubabe kwa Simba ulianza miaka hiyo hadi leo hii, wachezaji walikua warefu na waliojengeka kimisuli sana ile fiziki ilikua sio ya kutafuta, RTC kigoma, hii timu ilianza kuharibika baada ya kusajili warundi wengi, enzi hizo kwenye treni bado mnakunywa maziwa acheni tu.
 
Enzi hiyo mashirika ya umma yana timu zake, kulikua na magari ya mashirika hayo kama KAUMA, KAUDO. Dunia ilikua na mambo raha tupu, akina dada wanakuja kuangalia mpira wakiwa smart na mikanda yao ya vipepeo kiunoni na huku mashati ya Bahama ikiwa ndio fashion.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Mecco (ambayo ndio waliokuwa wamiliki wa team ya mecco) ilikuwa kampuni ya ujenzi ya serikali ambayo makao makuu yake yalikuwa mbeya.Miaka ya mwanzoni mwa themanini walikuwa wanajenga barabara za mwanza,kuanzia buzuruga stand hadi buzuruga shuleni, mpaka nyakato sokoni.Na kambi yao ilikuwa hapo nyakato (mecco) .Hivyo jina la mecco lilitokana na kambi ya hii kampuni ya ujenzi.
Mwananchi Engineering and Construction Company (MECCO).
 
MECCO YA MBEYA ilikuwa issue nyingine. jmaa walikuwa na pumzi haijawah tokea inasemekana wao mazoezini walikuwa kipindi kimoja wana cheza kwa dk 90 na kingine dk 90. sasa wakija kutana na mechi ya kawaida ambayo kipindi cha kwanza wanacheza dk 45 unaona kuwa walikuwa bado wapo fit kabisa. jamaa walikuwa wanakimbiza sana. sijui ilipotelea wapi hii team. walikuwa wapinzani sana pia wa TUkuyu stars ya mbeya.
 
Rashid Chama ni TFF?
Hapo Nilipoandika sijaonesha Chochote au kuelezea kama Rashid ni TFF soma quote yangu upya uelewe mkuu. bali utaona kuwa TFF hawawezi kosa records pale utakuwa hujaenda tu. Chama nae Anahistoria kubwa sana kahifadhi.
 
Back
Top Bottom