Ijue mgogoro ya kimataifa kuanzia miaka ya 1920

Ijue mgogoro ya kimataifa kuanzia miaka ya 1920

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Wadau kwema?

Ni kawaida kwa taifa moja kuwa na mgogoro na taifa lingine, kama tu jinsi mtu na mtu wanaweza kuwa na migogoro baina yao. Migogoro hii huibuka pale tu ambapo kuna mwingiliano wa kimaslahi baina yao.

Sasa basi baada ya vita ya kwanza ya dunia kufikia tamati mwaka wa 1918, kulikuwa bado kuna migogoro ya chini kwa chini baina ya mataifa kadhaa duniani. Hivyo jukumu la kusimamia migogoro na kuisuluhisha lilikuwa ni jukumu la baraza la umoja wa mataifa la wakati huo likijulikana kama league of Nation.

Ikumbukwe kuwa miaka ile ya kumalizika kwa vita , kuna mikataba kadhaa ilisainiwa na mataifa yaliyokuwa wanachama wa umoja huo ili kuepuka uwezekano wa kutokea kwa vita tena.

Nyingi ya mikataba hii ilisainiwa huko ufaransa.

Sasa mikataba iliyosainiwa huko ufaransa kulipelekea kuundwa kwa mataifa mengine mapya, na vilevile mipaka ya nchi ikabadilishwa . Sasa kumbuka mikataba ikisainiwa ya kubadilisha mipaka ya nchi kwenye karatasi ni rahisi , lakini kwenye uhalisia( kwa ground) ni tofauti. Hii ni kwa sababu jamii ya watu wanaweza kujikuta kwenye nchi nyingine na wengine kujikuta wameangukia upande mwingine wa taifa ambalo sio Lao.

Sasa kikawaida ni jukumu la baraza la umoja wa mataifa kugawa mipaka ya kimaeneo au ya kikanda kwenye nchi. Na majukumu haya ya kugawa mipaka husimamiwa na kamati ya mabalozi wa nchi wanachama .

Kipindi league of nation ikiundwa baada ya vita Ww1 , wanachama wa kudumu walikuwa ni ufaransa ,uingereza na italia.

Kwa hiyo wao ndio waliotoa maamuzi ya mwisho kutokana na wao wana ile kura ya turufu(veto power) katika kuchukua maamuzi.
Sasa basi hii hapa ni migogoro michache ya kimataifa iliyokuwepo kipindi cha League of Nation .

1. Mgogoro wa Vilna wa mwaka 1920.


Taifa la Poland na lile la Lithuania yalikuwa ni mataifa mawili yaliyoundwa baada ya mikataba ya amani ilyosainiwa na huko ufaransa baada ya vita ya kwanza ya dunia 1914-1918. Sasa mji wa Vilna (kwa sasa unajulikana kama vilnius) , ukaamuliwa ndio uwe mji mkuu wa Taifa la Lithuania, lakini changamoto ni kwamba mji huu asilimia kubwa waliokuwa wanaishi ni wa Poland.

Kutokana na mji huu kuwa na raia wengi wa Poland, kikosi cha waasi waliojihami kwa silaha cha Poland wakauchukua udhibiti wa mji huu. Hili swala lilipofika kwenye baraza la umoja wa mataifa yaani league of Nation ikaonekana Poland ndiye mchokozi. LEAGUE OF NATION ikaitaka nchi ya Poland iondoe majeshi yake ndani ya Lithuania, lakini Poland haikufanya hivyo. Kutokana na hilo, Lithuania ikaomba msaada wa kijeshi lakini ikashindikana. Hata wanachama kama Uingereza, Ujerumani ni Italy walishindwa kuingilia huu mgogoro kuepuka kuhatarisha maslahi yao ya kiuchumi.

Hivyo mgogoro huu haukusuluhishwa wakati huo. Na Poland akaendelea kuukalia mji wa vilna wa Lithuania kama wa kwao.


2.Mgogoro wa upper silesia wa mwaka 1921.

2011425_Upper_Silesia_Map_1.jpg


Eneo la upper silesia lilikuwa ni jimbo na eneo la kiviwanda lililokuwa kati ya Ujerumani na Poland. Kutokana na eneo hili kuwa la kimkakati kiviwanda , mjerumani na mpolish kila mmoja akitaka kulidhibiti ili liwe eneo lake.

Hii ni kwa sababu eneo hilo lilikuwa linazalisha madini ya chuma kwa ajili ya viwanda. Sasa ilipofika mwaka 1920, iliamuliwa ipigwe kura kwenye eneo hili la upper silesia. Kura hii ilijulikana kama PEBLISCITE. Hii kura ilikuwa inawataka raia wa eneo hili wachague wanataka wawe sehemu ya nchi gani kati ya Poland au Ujerumani.

Vikosi vya Majeshi ya uingereza na ufaransa vilitumwa eneo hili kusimamia uchaguzi kwenye vituo vya kura. Sasa wale raia wa vijijini wa eneo hili la upper silesia walipiga kura wawe sehemu ya Poland, ila wale wa mjini mjini walipiga kura yao ikionyesha wao wanataka kuwa sehemu ya Ujerumani.

Na kweli eneo likagawanywa kwa matokeo haya.Kuona hivi league of Nation ikaamua ku balance mambo ili kuepuka migogoro ya baadaye.

Ikaamuliwa ijengwe miundombinu kama vile reli na miradi ya maji iungwanishwe kati ya hii miji miwili. Na makubaliano yakaafikiwa

3.Mgogoro wa visiwa vya Aaland.

Hivi vilikuwa ni visiwa ambavyo mataifa ya sweeden na Finland kila mmoja akitaka viwe katika milki yake. Hii ni kwa sababu visiwa hivi vya aaland vilikuwa katikati ya bahari iliyokuwa inaitenganisha Finland na Sweden. Baada ya mkwaruzano wa muda mrefu , league of Nation ikatoa amri kwamba visiwa hivyo viwe chini ya Finland.

4.Mgogoro wa visiwa vya Corfu mwaka 1923.
Benito-Mussolini.jpg

Huu ulikuwa ni mgogoro uliokuwa ukihusisha nchi ya ugiriki na Albania. kila mmoja kutaka kudhibiti visiwa vya corfu vilivyokuwa kati ya mataifa hayo mawili kwenye bahari ya Mediterranean kutokana na mgogoro huu kuwa mzito baraza la umoja wa mataifa likateua jopo la ma balozi wa nchi kadhaa kwenda kusuluhisha huu mgogoro.

Jopo au kamati hii ilikuwa ikisimamiwa na jenerali wa kijeshi wa italia aliyejulikana kama Enrico tellini. Huyu bwana siku moja tarehe 27 august 1923 yeye na wasaidizi wake wakaamua kwenda hadi ugiriki ili kufanya field survey kuweza kutambua eneo hilo lenye mgogoro la visiwa vya Corfu.
Untitled.jpg
Lakini kwa bahati mbaya aliuliwa na watu wasiojulikana yeye pamoja na wasaidizi wake kwenye eneo la mpakani la kakavia kwenye mji wa loannina huko ugiriki.

Kuuliwa kwa jenerali huyu kukazusha tafrani nyingine. Kiongozi wa Italia wakati huo bwana Benito Mussolini akailaumu serikali ya ugiriki kwamba inahusika na tukio hili. Akaitaka ugiriki ilipe fidia na kuwakamata wasiojulikana wote waliohusika na kuwamaliza.

Serikali ya ugiriki ikiwa haijui ifanye lipi au iache lipi. Mgiriki akiwa hajui cha kufanya,benito Mussolini akatuma vikosi vya majeshi kwenda kuviteka visiwa vya Corfu vilivokuwa upande wa ugiriki.

Hili likapelekea watu 15 kuuliwa. Kuona hivi ugiriki ikaomba msaada wa umoja wa mataifa yaani league of Nation. Na ilipofika September 7 1923, league of Nation ikatoa Rulling(uamuzi/hukumu) ikilaani kitendo cha Mussolini kuivamia sehemu ya ugiriki kimabavu, na vilevile baraza la umoja wa mataifa ikatoa uamuzi kwamba ugiriki ilipe fidia ya kifedha kutokana na mauaji ya jenerali wa kijeshi wa italia tellini.

Na pesa hizi zingeshikiliwa na league of Nation kabla ya kulipwa italia endapo wauaji wa tellini wangepatikana. Maamuzi haya , Mussolini aliyakubali, lakini akaamua kutumia hila kuzunguka mlango wa nyuma. Hivyo akaamua kuwashawishi jopo la mabalozi (aliwahonga)kwenye umoja wa mataifa wabatilishe baadhi ya maamuzi yaliyotolewa, na kuitaka ugiriki iombe msamaha hadharani ili aondoe majeshi yake kwenye visiwa vya corfu.

Na kweli alifanikiwa kwenye hili. Na ilipofika tarehe 27 September alitoa vikosi vyake vya kijeshi ugiriki na pesa ya fidia akalipwa .
Achille_Beltrame_-_Disembarkation_of_Italian_soldiers_at_Corfu.jpg

Gazeti la kiitaliano la la domenica del corriere, likiripoti mgogoro huu wa corfu kwenye ukurasa wa mbele.


5. Mgogoro wa Bulgaria na ugiriki mwaka 1925.

Mwezi October mwaka 1925 , vikosi vya ugiriki viliivamia Bulgaria eneo la mpakani ambapo likapelekea mauaji kadhaa ya wanajeshi wa ugiriki. Bulgaria ikaiomba league of Nation iingilie kati.

Na kweli baraza la umoja wa mataifa likatoa hukumu likiishutumu ugiriki , na ikaitaka ilipe fidia kwa Bulgaria. Na kweli ugiriki ikakubali ili kuepuka kutengwa na jumuiya ya umoja wa mataifa , japo ililaani ikisema kwamba umoja wa mataifa una upendeleo wa kuegemea upande mmoja.

Hivyo unaposikia migogoro baina ya mataifa, haya mambo hayakuanza leo wala Jana. Na hata hapa Tanzania tumeshawahi pitia changamoto hii ya migogoro na majirani mfano ule wa Malawi...................

Lakini ikumbukwe haya mabaraza ya umoja wa mataifa muda mwingine yanakuwa kama mbwa asiyekuwa na meno. Ikumbukwe league of Nation haikuweza kuzuia kutokea kwa vita kuu ya pili ya dunia . Ni kama tu sasa U.N imeshindwa kumaliza mgogoro wa urusi na Ukraine.

Au mgogoro wa huko Kongo na waasi wa M23. Na pia mgogoro wa Sudan kati ya waasi na serikali .
 
Ukisoma usiache kumtag member mmoja rafiki yako.📍📍📌😊
 
Back
Top Bottom