Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,211
- 12,538
mwaka 1999 kuingia mwaka 2000 saa saba na robo usiku, tukiwa katika jahazi na masheikh sijui niwaite maustazi ama niwaitaje ila tangu mwanzo wa safari walikuwa ni wachangamfu sana, huku wao wakiwa na mizigo mingi katika jahazi lile nikimaanisha karibia robo ya mizigo yote iliyokuwemo katika jahazi ilikuwa ni ya kwao....spendi kuandika mengi ila kabla hatujafika unguja wale watu walisema wamefika na wakaanza kushusha mizigo wakiitosa ndani ya maji, watu wote tulishikwa na butwaa na mimi kiranga cha kudandia majahazi kiliisha siku hiyo..ila mwisho kabisa kulikuwa kuna pesa wanadaiwa ambayo waliahidi kuimalizia watakapo fika safari yao......nakumbuka kauli yao ya mwisho ilikuwa ni hii .....sisi si watu wa dhulma, mteueni mmoja wenu afuatane nasi tukampatie kiasi kilichobakia....nahodha akajibu tunashukuru wala hatuwadai sisi nyie nendeni tuu kwa roho nyeupeee...hatukufika unguja..je kuna ambaye ashausikia huo mji ulio karibu na unguja?