Ijue Mikoa ambayo 90% ya Nyumba zake za Kulala Wageni zina Kunguni,Panya na Inzi wengi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwa kama Mtanzania ambaye nimewahi ama kupata bahati sana ya kutembelea karibu 98% ya Mikoa iliyopo nchini Tanzania nimegundua ya kwamba kuna Mikoa ambayo ukibahatika tu kuitembelea na kama huko huna Mtu unayemjua basi ikitokea tu ukaamua kwenda Kulala / Kumbonji Gesti au Loji basi jiandae kuwa mvumilivu wa Kuumwa na Kunguni kama siyo Kusumbuliwa mno na Panya na kila mara Kuzingirwa na Inzi.

Kwa kuanza kabisa nichukue fursa hii Kuipongeza hii Mikoa ifuatayo kwa kuwa na Gesti au Loji nzuri ambazo nimejaribu kwa juhudi zangu zote kutafuta Kunguni,Panya na Inzi huku na kule lakini sikubahatika kukutana nao hadi siku naondoka huko......

  1. Arusha
  2. Mbeya
  3. Kilimanjaro
  4. Mara ( Musoma )
Mikoa ambayo kwakweli imenishangaza na ambayo siku zote nilizobahatika kuwepo huko na nikawa nimelala katika Gesti na Loji zao nikawa kila siku iwe asubuhi, mchana na jioni nafanya tu Kazi ya kupambana kutokung'atwa na Kunguni, Kusumbuliwa na Panya hadi Kuzingirwa hovyo na Inzi hadi nikakereka na kuahidi kuwa sitothubutu kwenda tena hata ikitokea nimekaribishwa ni hii ifuatayo na Mimi GENTAMYCINE nawataka wajirekebishe haraka kwani wanatutia aibu Watanzania......
  1. Singida
  2. Kigoma
  3. Dodoma
  4. Kagera ( Bukoba )
Ni imani yangu kubwa sana Members wa JF mnaotoka katika hiyo Mikoa yenye kuwa na Gesti au Loji zenye Kunguni, Panya na Inzi wengi mtasaidia Kupaza Sauti huko Kwenu ili aibu hii muweze Kuikwepa. Halafu mkiwa humu mijini huwa mna shobo / nyodo kweli kumbe huko makwenu hali ni tete.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba kwa bahati nzuri GENTAMYCINE sina Mkoa wowote ninaotoka hapo katika hiyo yote iliyotajwa kwa upande wa ile isiyo na Kunguni, Panya na Inzi wala ile ambayo inayo ila nadhani nitakuwa nimesaidia kuwatahadharisha wenyeji wa huko wachukue hatua za haraka mno.

Nawasilisha.
 
Mara nyingi kunguni huwa hawaishi kwenye baridi, Nimekaa Arusha sana sijawahi kuona Kunguni.
 
Mara nyingi kunguni huwa hawaishi kwenye baridi, Nimekaa Arusha sana sijawahi kuona Kunguni.

Ni kweli Mkuu ila huko Singida, Kigoma, Dodoma na Kagera kumekithiri kwa hao Kunguni, Panya na Inzi. Yaani wamezidiwa kwa mfano na hata Mkoa tu wa Mara ambao ni msafi, mzuri na kila siku unakimbiliwa na Wageni kutaka Kuutembelea kutokana na kwamba huko Kunguni, Panya na Inzi hutothubutu kuwakuta ng'o.
 
Huwa unalala gesti za buku 5 nini?
 
unatafuta gesti za 5000 utakosaje kunguni sasa mjomba......kwa bei hiyo kunguni halali yako
 
Mkuu dodoma nakupa 100% nilishawahi kulala loji fulani ivi na demu yaani ilitubid usiku tutoe mashuka tutandike sakafuni ndo tulale
 
Nilikua na data collection pembezoni mwa tz huko kigoma mwaka fulani.
Tumeshindwa kurudi town sababu ya mvua na ukungu ikabidi tucheki "gesti hausi"
Alooo, kwanza room nimepewa ndo warundi wametoka kupigana "miti" ikabidi PRIMUS zinihusu till down.
 
mbona unakuwa muongo sana kagera kuna chawa kunguni wanaishi kwenye joto na chawa kwenye baridi uwezi kukumkuta chawa dar...
 
Starehe garama. Sa we Una 5000 mfukoni unataka uish Kama Una U$500???
 
Suala la Nyumba za kulala Wageni ni mtihani kwa Watz wengi...wakishajenga basi wao wanatulia.na kuacha uchafu kila sehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…