Omuzirambogo
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 685
- 751
Acha ubahiri wa kulala guest za vichochoroni za 5,000 au 3,000/ nenda zile zenye adhi. Au mpiga chabo maana huko wanakaa watu wa show timeNikiwa kama Mtanzania ambaye nimewahi ama kupata bahati sana ya kutembelea karibu 98% ya Mikoa iliyopo nchini Tanzania nimegundua ya kwamba kuna Mikoa ambayo ukibahatika tu kuitembelea na kama huko huna Mtu unayemjua basi ikitokea tu ukaamua kwenda Kulala / Kumbonji Gesti au Loji basi jiandae kuwa mvumilivu wa Kuumwa na Kunguni kama siyo Kusumbuliwa mno na Panya na kila mara Kuzingirwa na Inzi.
Kwa kuanza kabisa nichukue fursa hii Kuipongeza hii Mikoa ifuatayo kwa kuwa na Gesti au Loji nzuri ambazo nimejaribu kwa juhudi zangu zote kutafuta Kunguni,Panya na Inzi huku na kule lakini sikubahatika kukutana nao hadi siku naondoka huko......
Mikoa ambayo kwakweli imenishangaza na ambayo siku zote nilizobahatika kuwepo huko na nikawa nimelala katika Gesti na Loji zao nikawa kila siku iwe asubuhi, mchana na jioni nafanya tu Kazi ya kupambana kutokung'atwa na Kunguni, Kusumbuliwa na Panya hadi Kuzingirwa hovyo na Inzi hadi nikakereka na kuahidi kuwa sitothubutu kwenda tena hata ikitokea nimekaribishwa ni hii ifuatayo na Mimi GENTAMYCINE nawataka wajirekebishe haraka kwani wanatutia aibu Watanzania......
- Arusha
- Mbeya
- Kilimanjaro
- Mara ( Musoma )
Ni imani yangu kubwa sana Members wa JF mnaotoka katika hiyo Mikoa yenye kuwa na Gesti au Loji zenye Kunguni, Panya na Inzi wengi mtasaidia Kupaza Sauti huko Kwenu ili aibu hii muweze Kuikwepa. Halafu mkiwa humu mijini huwa mna shobo / nyodo kweli kumbe huko makwenu hali ni tete.
- Singida
- Kigoma
- Dodoma
- Kagera ( Bukoba )
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba kwa bahati nzuri GENTAMYCINE sina Mkoa wowote ninaotoka hapo katika hiyo yote iliyotajwa kwa upande wa ile isiyo na Kunguni, Panya na Inzi wala ile ambayo inayo ila nadhani nitakuwa nimesaidia kuwatahadharisha wenyeji wa huko wachukue hatua za haraka mno.
Nawasilisha.