Ijue nchi ya Cambodia

Ijue nchi ya Cambodia

cna uhakika 100% kwa hilo but nachojua kitabu cha The Monk who sold his ferrari ni kizuri sana kiasi cha kumfanya msomaji akaona thamani ya maisha yake...coz jamaa kaelezea vitu vingi sana
Ni kweli..
 
Wakati nikiwa kidato cha pili nliwahi kusoma kitabu flani kuhusu Khmer regime.

Nilitia nia kwamba ni lazima nifike Cambodia maishani mwangu. Katika harakati zangu za kula bata, nilifanikiwa kufika Cambodia mwishoni mwa mwaka 2018.

Nlijifunza mengi na kuona mengi, ntarudi ku-share nanyi.

Angkor wat is real.

20200207_100917.jpg
 
Nchi ya Cambodia inapatikana kusini mashariki mwa bara la Asia. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2019 inaaminika kuwa Cambodia ina raia zaidi ya Million 15.

Nchi ya Cambodia kwa upande wa mashariki imepakana na Vietnam, Upande wa kusini magharibi imepakana na Ghuba ya Thailand, upande wa kaskazini magharibi imepakana na nchi ya Thailand huku upande wa kaskazini mashariki imepakana na nchi ya Laos

Nchi hii ipo chini ya mfalme Norodom Sihamon huku Waziri mkuu wake akiwa ni Hun Sen

Hun Sen Waziri mkuu wa Cambodia ndio anashikilia rekodi ya Waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani... Alianza kuwa Waziri mkuu Mwaka 1985 hadi sasa

Mji mkuu wa Cambodia ni Phnom Penh ...asilimia 95 ya raia wa Cambodia ni waumini wa ubudha

1) Mfalme wa Cambodia ana miaka 57 lakini mpaka muda huu bado hajaoa na wala hana mtoto

2) Tokea mwaka 1953 hadi sasa nchi ya Cambodia imeshabadilishwa jina mara 6, baadhi ya majina yaliyowahi kuitwa ni kama ufalme wa Cambodia 1953- 1970.
Jamhuri ya Khmer 1970-1975

Kampuchea 1975-1979

Jamhuri ya watu wa Kampuchea 1979-1989

Cambodia 1989-1993

Ufalme wa Cambodia 1993 -sasa

Ilikuwa kila serikali inayotawala inakuja na jina Lake

3) Ni nchi yenye vijana wengi karibia nusu ya raia wake ni vijana wasiozidi miaka 20

4)Cambodia ndio nchi yenye jengo kubwa zaidi duniani kwa ajili ya kuabudia Angkor Wat. Jengo hili limetambulika kama mojawapo ya ajabu la duniani na kwa kiasi kikubwa imechangia kuongeza idadi ya watalii katika nchi hiyo

5) Ndio bendera pekee duniani yenye alama ya jengo....

6) Mazishi ndio kitu chenye gharama zaidi katika nchi ya Cambodia ...inakadiriwa haipunguwi chini ya dola za kimarekani 5000 ambazo ni zaidi ya Million 10 za kitanzania... Gharama kubwa ni Mahala pa kuzikia

7) Tofauti na nchi nyengine za bara la Asia nchi ya Cambodia haina vikwazo vikubwa kwa mashoga

8) Kichwa ndio kiungo chenye heshima zaidi nchini Cambodia huku miguu ikionekana ni kitu kisicho na thamani kwahiyo kumuonyeshea mtu soli ya mguu wako mtu wa Cambodia ni kama umemvunjia heshima kwa kiasi kikubwa sana

9) Kutoka mwaka 1975 hadi 1979 palitokea mauaji makubwa sana katika nchi ya Cambodia na kutokana na hii ndio imesababishwa Nchi hii kuwa na vijana Wengi na inasemekana asilimia 63 ya raia wa Cambodia ni chini ya miaka 30

10) Cambodia wanasherehekea mwaka mpya katika mwezi wa nne (April) ambapo ni mwisho wa mavuno huitwa Choul Chnam Thmey

11) Usafiri wa rahisi na haraka ni bodaboda (tuk tuk)

12) Cambodia ilitawaliwa na ufaransa kuanzia mwaka 18863 hadi mwaka 1953

13) Nchi ya Cambodia ina zaidi ya landmines (ni kama mabomu yaliofukiwa chini ya ardhi) million 4.... Cambodia ni nchi ya tatu kuwa na landmines duniani... huku nchi ya kwanza ikiwa ni misri

14) Duniani kuna nchi tatu tu ambazo hazina huduma ya McDonald's ikiwemo Cambodia

15) Mchele ndio chakula Kikuu nchini Cambodia...katika lugha ya Khmer ambayo ndio lugha Kuu nchini Cambodia neno chakula na neno mchele ni moja

16) Cambodia ndio nchi inayoongoza duniani kwa ukataji wa miti

17) Utalii na biashara ya nguo ndio vitu muhimu katika nchi ya Cambodia

18) Kima cha chini cha mshahara ni kuanzia dola za kimarekani 100 ambazo ni sawa na 230000 za kitanzania
Ahsante mkuu kwa elimu nzuri,naomba kufahamu nchi zilizopo maeneo ya Gabon,afrika ya kati,na Guinea zote zile hasa maeneo hayo,hasa wananchi idadi yao na tamaduni na maendeleo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom