Bakwata ni tawi la ccm.Naunga mkono HOJA..CDM endeleeni kuyahusisha makundi mbalimbali ya kijamii, hasa TEC na BAKWATA
Ndio hasa, ikiwa ni mwizi zisikike kelele...Kelele za Mwiiiziii!!! Mwiiizii wa kuuraa!!! kutoka unguja.

It makes sense!Joseph at Gwajima anapiga kelele kudai maono ya nchi yaandikwe ubaoni Ili Kila Rais ajaye asome na kutekeleza maono hayo, SI kila mmoja kuja na lake
Sio kususia uchaguzi,Chadema kupitia Tundu Lissu wanatekeleza kile ambacho nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi ...No reform No election. CCM waendelee tu kujipa moyo kuwa uchaguzi utakuwepo wakati mimi mpigakura na watu kadhaa ninaopata wasaa wa kuteta nao wakijiapiza kutokwenda kupigakura kama hakutakuwa na mabadiliko katika mfumo wa kusimika viongozi. Moto umeisha washwa na joto linaendelea kupanda polepole.....Tutaelewana tu.![]()
Vyovyote itakavyokuwa, kura yangu na kundi kubwa tu la watu hazitapigwa bila kupata Katiba mpya, Referendum kuhusu uwepo wa muungano na Tume huru ya uchaguzi. No reform No election!.Sio kususia uchaguzi,
Ni kwenda kuuzuia usifanyike bila TUME HURU YA UCHAGUZI. Na katiba mpya
Uhuru aliopigania Nyerere una thamani ipi ikiwa sanduku la kura zinaongezwa kura fake kumpa ushindi muuza mihadarati kuwa kiongozi wetu?Ukiangalia historia ya Nchi zilizoingia kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe kwanza huwa yaanza mang'uniko yanapuuzwa, halafu yanafuatia malalamiko na kelele za kuonya zinapuuzwa na wale wanaopaza sauti wanatekwa na kupotezwa halafu kunakuja kaukimwa kidogo haka kaukimya ni kama kama ka miezi kadhaa.
Halafu inatokea spark ndogo tu hata ya polisi kupiga raia machafuko yanaanza nguvu kupita kiasi zinatumika halafu full blown civil war.
Angalia Liberia na kwengineko CCM msituharibie Nchi, hakuna anayetaka kwenda kukaa ukimbizini.
Kuna Babu mmoja aliiibiwa akawa Mbogo lakini yeye sasa ndio kila siku anamlaumu Lissu.Uhuru aliopigania Nyerere una thamani ipi ikiwa sanduku la kura zinaongezwa kura fake kumpa ushindi muuza mihadarati kuwa kiongozi wetu?
Huyo bado anaamini ukombozi utatoka CCM.Kuna Babu mmoja aliiibiwa akawa Mbogo lakini yeye sasa ndio kila siku anamlaumu Lissu.
View attachment 3290561
: Mtu yeyote asikudangaanye kuwa kelele KUPITIA keyboard JF na majukwaa mengine hazisikiki, kelele ni kelele. Piga kelele.📌📌🔨🔨🔨🔨Hellow!
Utapingana na Mimi kama hujawahi simama Katika umma wa wananchi kama kiongozi, ila utakubaliana nami kuwa Katika halaiki yoyote, kelele za umati wa watu kushangilia au kuzomea zina nguvu kubwa sana Katika kuongeza ujasiri au kuingiza hofu kwa kiongozi asimamaye jukwaani.
Niliwahi kushuhudia umma wa wananchi ukimpigia kelele hayati Nyerere alipokuwa jukwaani akimnadi Hayati Mkapa jukwaani, Kila alipojaribu kuongea kelele ziliongezeka, Kila alipoinua kifimbo chake kutuliza sauti zile ,sauti hazikukoma, ilifika time wapiga kelele wale walienda kumchukua mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kiboko Nyerere Ili aje kuongeza kelele Katika mkutano ule, baada ya kelele kuzidi alipofika ndugu yule, Mwalimu alisikika akisema nilidhani Niko Kenya, na baada ya kusema hayo, aliteremka jukwaani na mkutano uliishia pale. HAYO yalitokea mwaka 1995 kwenye kuanza mfumo mpya wa vyama vingi, Mrema akiwa mgombea wa upinzani uwanja wa Mukendo Primary School.
Mji wa Yeriko uliangushwa kwa kelele za sifa kwa Mungu mkuu, kelele ziliingiza hofu kwa maadui wakakosa Cha kufanya. Hilo linarufunza nguvu ya kupaza sauti kuzomea au kushangilia.
Kuelekea Katika majukwaa mbalimbali ya kisiasa 2025, wananchi wanatakiwa kupiga tu kelele, kelele ni kelele,
Kuimba ni kelele,
Kulia ni kelele pia,
Kuzomea ni kelele pia,
Kushangilia ni kelele pia.
-Martin Luther alipiga kelele Amerika ikasikia,
-Desmond Tutu alipiga kelele, ubaguzi wa rangi ukayeyuka,
-Mwl Nyerere alipiga kelele ya haki, nchi ikazukiwa na Nuru, tukapata uhuru.
-Tundu Antipas Lissu anapiga kelele kutafuta kuondoa haramu ndani ya sanduku la kura. "NO REFORMS, NO ELECTION". Amesikika🔥💪
- Joseph at Gwajima anapiga kelele kudai maono ya nchi yaandikwe ubaoni Ili Kila Rais ajaye asome na kutekeleza maono hayo, SI kila mmoja kuja na lake.
-Rabbon anapambana kuuleta ufalme wa Mungu Katika siasa za nchi yetu, viongozi walevi wa namna mbalimbali wasipate fursa kuongoza watu, haki itawale ,hofu ya Mungu itawale, UOVU utokomee, elimu ishamiri nchi istawi.
Kila asimamaye jukwaani apate kelele anayostahili kulingana na matendo yake.
1. Anayestahili kelele za shangwe, apewe shangwe,
2. Anayestahili kelele za kuzomewa, apewe haki yake.
Karibuni tupige kelele 🙏,
Na hakika adui atakuwa mdogo sana, nguvu zitamwisha, vifundo vya miguu vitakosa nguvu, hatoendelea kutoa hadaa na uongo kwa wananchi Tena.
NOTE: Mtu yeyote asikudangaanye kuwa kelele KUPITIA keyboard JF na majukwaa mengine hazisikiki, kelele ni kelele. Piga kelele.
Nawasiiisha 🙏
Ni ukoo wa Simba huyo.Ni mara kadhaa unamtaja Gwajima, umeona nn Mkuu Kwa huyu mtu
Ogopa teknolojia na mitandao.: Mtu yeyote asikudangaanye kuwa kelele KUPITIA keyboard JF na majukwaa mengine hazisikiki, kelele ni kelele. Piga kelele.📌📌🔨🔨🔨🔨