Ijue Premio ya Kijerumani, Volkswagen Passat 1.4 L TSI

Ijue Premio ya Kijerumani, Volkswagen Passat 1.4 L TSI

Joined
Jun 13, 2023
Posts
32
Reaction score
31
Habari wadau!

Leo ningependa tuzungumze kusuhusu hii mashine ya kijerumani brand ya Volkswagen iitwayo Passat 1.4L TSI.

So ningependa ku summarize kidogo baadhi ya mambo.

Ni gari aina ya saloon au sedan yenye Turbo charge petrol engine inayokutumia mafuta 16-18 L/km, tanki la mafuta ni litre 70,ina gear 7 kwa automatic na 6 kwa manual na inavuta mbele. Kwa upande wa size ya ndani ni kubwa.

Vipuli vya hii gari vinaingia kwa wingi Tanzania na Kenya so sio ishu.

Ina ride quality nzuri na bei yake kwenye market ni affordable

Kama unataka kumiliki hii gari nakupa go ahead, cha msingi kuzingatia service hasa kwenye DSG gear box upate oil original na engine oil inapswayo na pia.

MSISITIZO! Usiweke mafuta yasiyo na viwango kwenye hii gari, itaharibu turbo, peleka sheli ya PUMA, TOTAL au sheli nyingine bora.
 

Attachments

  • w400_Volkswagen-Passat-B7-2.jpg
    w400_Volkswagen-Passat-B7-2.jpg
    11.4 KB · Views: 43
  • x5_12368221125vk.jpg
    x5_12368221125vk.jpg
    59.2 KB · Views: 47
Vipi itaweza kumudu barabara zetu?
Ninachoamini, saloon nyingi ni zimeundwa kwa ajili ya barabara za mijini japo kwa nyingine unaweza kuendesha kwenye light gravel ila sio barabara mbovu zenye mashimo, mawe na utelezi mkubwa.

Japo ground clearance yake iko chini Gari hii ni ngumu, inamudu barabara inategemea na uendeshaji wako, Ila usiendeshe mara kwa mara kwenye barabara mbovu, utaongeza gharama za badilisha bushi na shocks.
 
Back
Top Bottom