Ijue Rhesus factor na ujauzito

Naomba kufaham kuhusu hii Rh negative na Rh positive kwenye kubeba mimba
 
Mwanamke mwenye blood group ya negative akibeba mimba ikatokea mtoto ni positive basi huyo mtoto atashambuliwa na na red cells kutoka kwa mama ikitokea damu ya mama na mtoto zimegusana.

Kwa hivyo kuna sindano mwanamke huchomwa baada ya mtoto kuzaliwa. Au akiwa mjamzito ikiwa ni mimba ya pili au mimba iliwahi kutoka. Mwone dr kwa ushauri zaidi.
 
Mama ana group positive
 
Kama wewe (yaani Mama) ni Rhesus positive na baba wa mtoto ni rhesus negative hakuna shida.

Ila kama Rhesus yako mama ni negative na ya baba ni positive , kiumbe kitakachoanza kukua tumboni kitakua na Rhesus positive kinyume na mwili wa mama ambao una Rhesus negative.

Wakati wa kujifungua , wanapontenganisha mama mwenye Rhesus negative na mtoto mwenye Rhesus positive ilotokana na kwa baba yake, mchanganyiko wa damu uta-Stimulate/initiate kuzalishwa kwa kinga ya mwili ambayo chochote chenye Rhesus positive kitakachokuja baadae kitakuta tayari mwili umeki-identify kama adui na kukishambulia na kufa chap....

So kuzuia Hilo Kuna sindano mama huchomwa Ili kuzuia utengenezwaji wa hiyo kingamwili itakayokua inaua Kila chenye positive kikija baadae (mimba za baadae)...

Tembelea kituo Cha afya Karibu nawe kwa msaada zaidi.
 
nina O+ na mume O-, mtoto wa kwanza yupo ila nimeambiwa kwa watoto wanaofwata lazima nichome Anti D la sivyo hakuna mimba itafika 10 weeks
 
nina O+ na mume O-, mtoto wa kwanza yupo ila nimeambiwa kwa watoto wanaofwata lazima nichome Anti D la sivyo hakuna mimba itafika 10 weeks
Hapo mbona hakuna shida mkuu. Shida ni endapo mama akiwa O -ve ila kama mama ni O +ve baba O -ve mbona hakuna tatizo
 
Vipi mkuu shemeji alijifungua salama??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…