Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mama ana group positiveMwanamke mwenye blood group ya negative akibeba mimba ikatokea mtoto ni positive basi huyo mtoto atashambuliwa na na red cells kutoka kwa mama ikitokea damu ya mama na mtoto zimegusana.
Kwa hivyo kuna sindano mwanamke huchomwa baada ya mtoto kuzaliwa. Au akiwa mjamzito ikiwa ni mimba ya pili au mimba iliwahi kutoka. Mwone dr kwa ushauri zaidi.
Haina issue kama ni hivyo. Ila muhimu upate ushauri wa dr. Mimi sio dr ila nina uzoefu wifi wangu ni negative na kama nakumbuka vizuri inahusu tu wanawake negative.Mama ana group positive
nina O+ na mume O-, mtoto wa kwanza yupo ila nimeambiwa kwa watoto wanaofwata lazima nichome Anti D la sivyo hakuna mimba itafika 10 weeksBila shaka umewahi kuwasikia wataalamu wa afya wakisisitiza umuhimu wa wenza kufanya vipimo mbalimbali kabla ya kuamua kuwa pamoja kwa ajili ya kutengeneza familia (kuzaa).
Moja ya vipimo vinavyosisitizwa ni cha makundi ya damu na Rhesus factor.
Kipimo hiki ni muhimu sana kwa sababu utofauti wake baina ya wenza unaweza kuathiri watoto watakaozaliwa na hivyo lengo na kuwa na muendelezo wa familia lisifikiwe hivyo kuzua migogoro baina ya wana ndoa, ndugu au watu wengine wa karibu mara nyingi ikihusianishwa ni uchawi.
Binadamu wameundwa na makundi manne ya damu, yaani A, B, AB na O.
Makundi haya hutengenezwa katika seli nyekundu za damu (Red Blood Cells) au RBCs.
View attachment 2980679
Nje ya kundi husika la damu, chembe hizi nyekundu za damu zinaweza kuwa ama kutokuwa na protini maalumu juu yake iitwayo Rhesus factor.
View attachment 2980680
Seli yako ya damu ikiwa na protini hii tunasema wewe una Rhesus factor positive (Rh+) na kwa yule ambaye seli zake hazina protini hii tunasema ni negative (Rh+).
Kazi ya Rhesus factor (antigen) ni kuimarisha ukuta wa seli nyekundu za damu lakini antigen nyingine huupa mwili taarifa juu ya kitu kigeni kinachoweza kuudhuru mwili (foreign body) ili mwili uweze kutengeneza kinga (antibodies) za kuulinda dhidi ya mashambulizi tarajiwa.
Sasa huku kuwepo ama kutokuwepo kwa protini hii ya Rh baina ya wenza huweza kuathiri ujauzito kama ambavyo nitaelezea hapo chini.
RH FACTOR NA UJAUZITO.
Itakapotokea mwanamke ana group la damu ambalo halina protini ya Rhesus (Rh-) akakutana na mwanaume ambaye yeye group lake la damu lina protini hii (Rh+) na mwanamke kupata ujauzito na mtoto huyu akarithi vinasaba vya baba yaani Rh+ inaweza kuleta tatizo kwani endapo utatokea mwingiliano wa damu ya mtoto na ya mama ikitokea mimba imetunga nje ya kizazi (ectopic), kutoka damu kipindi cha ujauzito (placenta previa/ abruptio placenta) au wakati wa kujifungua. Mwingiliano huu hutengeneza kitu kiitwacho kitaalamu Rh Incompatibility.
Hii hutokea pale ambapo seli nyekundu za damu za mama (Rh-) zitagusana na Seli nyekundu za mtoto (Rh+) hivyo seli za kinga za mama (antigen) zitatambua seli za mtoto kama kitu kigeni kinachotaka kumdhuru na hivyo zitazalisha seli kinga (antibodies) ili kushambulia seli za Rh+.
Kwahiyo mtoto huyu wa kwanza atazaliwa salama kabisa bila tatizo kwake, lakini itakapotungwa mimba nyingine yenye Rh+ mimba hii haitaweza kukua kwani mfumo wa kinga wa mama utaitambua kama kitu kigeni na hivyo mwili utafanya kila kitu kuhakikisha unaiharibu, kuiua na kuitoa.
Hivyo seli nyekundu za mtoto aliyeko tumboni zitaharibiwa vibaya na hivyo ujauzito wa mtoto huyu na wanaofuatia (Rh+) kushindwa kukua na kuharibika.
Kumbuka: Ikiwa mwanamke huyu aliwahi kupata ujauzito akautoa/ ukaharibika au mimba kutunga nje ya kizazi na mwingiliano wa damu ya mtoto ambaye alitarajiwa kuwa (Rh+) na damu yake yenye (Rh-) kutokea basi mimba zote zinazofuata za watoto zenye Rh+ zitaharibika.
Kwa maana hiyo inaweza kuwa mimba yake ya kwanza aliyoamua kuzaa na kulea lakini mimba hii itaharibika sababu awali alishapata mimba kama hiyo.
Japo mtoto hakuzaliwa ila damu zilishagusana na hivyo mwili wake kutengeneza kinga dhidi ya ujauzito mwingine wa kufanana na huo (Rh+).
Sasa swali la kujiuliza ni je wakikutana watu kama hawa wenye Rh factor tofauti hawapaswi kuoana/ kupata watoto? jibu ni WANAWEZA KUZAA.
Inapotokea wamepima makundi yao ya damu na kukutwa ni Rh+ na Rh- kabla ya kuamua kuzaa ambapo mwanamke akiwa mjamzito atapaswa kuchomwa sindano maarufu kama Anti-D / (Rho) au RhoGAM wiki ya 28 ya ujauzito na mara baada ya kujifungua.
Sindano hii inapaswa kuchomwa pia ikiwa mama mjamzito amepoteza ujauzito (misscariage), mimba imetunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) au limetokea tukio lolote la kumsababishia kutoka damu kipindi cha ujauzito kabla ya kujifungua.
Nini umuhimu wa sindano hii?
Sindano hii huzizuia seli kinga za mama kuzalisha antibody ambazo zingeweza kuja kushambulia seli za ujauzito unaofuata wa mtoto ambaye ni Rh+ na kwa kufanya hivyo mimba nyingine zote zitakazokuja ambazo ni za Rh+ zitaweza kukua na kuzaliwa bila ya tatizo lolote kwa mama au kwa mtoto.
Kumbuka: Ikiwa mama ni Rh- na mtoto ni Rh- hakuna madhara kwao.
Ni matumaini yaku kuwa uzi huu mfupi umekusaidia kuelewa jambo hili kwa lugha rahisi na utakusaidia kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuamua kuwa na mtoto na mwenza wako. Kama si wewe hata watu wako wa karibu. La msingi kufanya ni VIPIMO mbalimbali kabla ya kuamua KUZAA.
Hapo mbona hakuna shida mkuu. Shida ni endapo mama akiwa O -ve ila kama mama ni O +ve baba O -ve mbona hakuna tatizonina O+ na mume O-, mtoto wa kwanza yupo ila nimeambiwa kwa watoto wanaofwata lazima nichome Anti D la sivyo hakuna mimba itafika 10 weeks
Vipi mkuu shemeji alijifungua salama??Hiyo kitu ndo napambana nayo saizi kwa mpenzi wangu. Mtoto wa kwanza alizaliwa kama ulivyosema na ana miaka 6. Changamoto ni mimba ya saizi. Amechomwa hiyo sindano moja, gharama ni laki 2. Walisema sindano ya pili mwezi huu wa tano gharama ni ileile laki 2. Na itakuwepo nyingine tena ya mwisho 😬😬. So mimba moja sindano za laki 6 😬😬😬😬