Maelezo yako ni marefu lakini hayana usahihi wa asilimia mia moja kuna sehemu ni dhana tu mfano ni pale unapoandika mauaji ya Kabila na Savimbi yalikuwa na mia moja huo ni upotoshaji umeandika unachodhani huna ushahidi.
Samahani kwa usumbufu mkuu, ni makosa ya kiuandishi, nilikuwa na maana ya "mwaka mmoja"
Kwa faida ya wasomaji nikuwa
Laurent-Desire Kabila (27 Novemba 1939 16 Januari 2001) alikwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Mei 1997 hadi kuuawa 2001. Alifuatwa na mwanawe Joseph Kabila.
Kabila alifika ikulu kwa kumpindua Mobutu Sese Seko.
Laurent Kabila alizaliwa katika familia ya Waluba huko Baudouinville (sasa Moba) karibu na Albertville (Kalemie) kando la Ziwa Tanganyika. Alisoma huko Ujerumani ya Mashariki na Paris akarudi Kongo baada ya uhuru wa nchi alipojiunga na umoja wa vijana wa chama cha Patrice Lumumba.
JONAS SAVIMBI
Jonas Malheiro Savimbi alikuwa ni kiongozi wa vita vya msituni nchini Angola. Savimbi alizaliwa 3 Agosti 1934 na kufariki 22 Februari 2002. Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la UNITA (kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.
UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana. UNITA ilianza kama kikundi chenye itikadi ya kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA iliyosaidiwa na Urusi. Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Savimbi alipata a kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA (kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho).
Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire), Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua.
Savimbi aliuawa vitani 22 Februari 2002.