Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Katika dunia ya leo, watu wengi wanatamani kuishi maisha marefu na yenye baraka. Kwa sababu hiyo watu wana struggle kutafuta njia zitakazowasaidia kuishi miaka mingi kupitia tiba, lishe bora, mazoezi ya mwili au kuwa na ulinzi mkali. Hata hivyo, bado tu tunashuhudia watu wengi wakifa mapema sana kabla ya umri unaostahili.
Kama huna habari, Biblia inatuonesha siri ya kuishi maisha marefu na yenye baraka. Siri hii ipo katika Waefeso 6:2-3. Imeandikwa hivi: “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”
Siri ndiyo hiyo: kuwaheshimu baba na mama. Ukifanya kinyume na hivyo, maana yake unajipunguzia baraka na muda wako wa kuishi.
Kwa mantiki hiyo, ukosefu wa heshima kwa wazazi ni moja ya sababu kubwa inayowafanya vijana na watu wengi kufa mapema kabla ya wakati wao.
Wazazi wako wanaweza kuwa maskini, wasio na elimu, au hata wasio na uwezo mkubwa wa kukusaidia – lakini bado ni wazazi, waheshimu tu.
Hata kama mzazi anakukera, anakupa vijembe, au hakuweza kukulea kwa viwango ulivyotarajia, bado jukumu lako la kumheshimu halibadiliki.
Ni hatari sana, mzazi wako akikulaani. Neno la mzazi lina uzito mkubwa – linaweza kukuinua au kukushusha chini. Maandiko yanatuambia kwamba laana isiyo na sababu haimpati mtu. Hii ina maana kwamba laana yenye sababu inaweza kumpata mtu. Kwahiyo ukimdharau mzazi wako, akaamua kukulaani, laana yake inaweza kuharibu maisha yako na kukupunguzia miaka ya kuishi.
Kwahiyo mtu akifa kwa sababu ya ugonjwa, ajali, kupigwa nk, inawezekana kabisa kwamba 'mzizi' uliosababisha kifo chake sio mambo hayo, bali ni kutowaheshimu wazazi wake.
Kumbuka pia baba yako na mama yako, sio wale tu waliokuzaa. Hata wengine wenye umri sawa na umri wa wazazi wako, ni wazazi - usiwadharau, waheshimu.