Ijue sababu Kuu ya kwanini Injinia Hersi Said aliambatana na Haji Manara kwenda kumuomba Radhi Rais wa TFF Karia

Ijue sababu Kuu ya kwanini Injinia Hersi Said aliambatana na Haji Manara kwenda kumuomba Radhi Rais wa TFF Karia

Kwa mlundikano wa Makosa ya Mhamasishaji wa Yanga SC na Jeuri zake pamoja na Dharau anazowafanyia Watendaji wa TFF Injinia Hersi Said na hata Watu wa Yanga SC wenye Akili wanajua kuwa kwa Haji Manara kuingia Kwake Mwenyewe katika 18 za TFF na Sekretarieti yake safari hii haponi na anaenda Kufungiwa.

Kwakuwa tayari Injinia Hersi Said ndiyo anaenda kuwa Rais mpya wa Yanga SC (japo Uchaguzi Mkuu wao bado) ila kwa Ukaribu mkubwa wa Haji Manara na Injinia Hersi Said ni kwamba tayari kuna Kitengo Kipya cha Habari na Mawasiliano kimeandaliwa na aliyeandaliwa kuwa hapo kama Mkuu wake ni Haji Manara.

Injinia Hersi Said anajua kuwa endapo Rafiki yake Mkubwa Haji Manara atafungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF itampa wakati mgumu wa Kumtafuta Mtu wa kufanya nae Kazi kwani siyo Siri Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli hatakiwi na Injinia Hersi Said japo wakikutana Wawili hawa huonyesha wana Mahusiano mema ila wanaojua wanasema ni Paka na Panya ndani ya Yanga SC.

Na endapo Haji Manara hatofungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF tutaamini Tetesi zilizopo kuwa hata ile Juzi Injinia Hersi Said alipoambatana na Mhamasishaji wa Yanga SC Haji Manara kuna Ahadi ya Fedha (kutoka GSM) iliahidiwa Kwake Rais wa TFF Wallace Karia na Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya TFF kama wasipomuadhibu Haji Manara ambaye Injinia Hersi Said anamhitaji sana katika Sekretarieti yake mpya ya Uongozi ndani ya Yanga SC mara baada ya Kuchaguliwa rasmi kuwa Rais Jumamosi ya Wiki hii.

Hassan Bumbuli anza Kutafuta Ajira ( Kazi ) Kwingineko au rejea pale ulikokuwa kwa muda mrefu kama Mwandamizi MWANANCHI Tabata, ila Injinia Hersi Said akiwa Rais wa Yanga SC rasmi Jumamosi hii ijayo basi jua hutohitajika tena Klabuni.
Waganga wa kienyeji miaka hii wamekuwa wengi sana
 
kwanini wengine wameomba msamaha ila adhabu zimebaki vilele yeye aombe msamahaa afu apunguziwe yeye ni nani kwenye huu mpira wa Tz
Nasubiri kuona Majibu juu ya hili Swali lako lililokwenda Kidato ( Shule ) kabisa.
 
Si ubadili tu title iwe "Bumbuli tafuta kazi nyingine"
Maana Uzi wote unamnanga Bumbuli kuhusu kibarua chake
 
nadhan hata kocha wa mbeya kwanza alifungiwa miaka 5 na aliomba msamaha the some to shaffi dauda endapo manara atafungiwa basi nitaamini TFF nichombo imara cha kusimamia mpira Tz ila akisamehewa nitajua TFF na GSM ni tako na chupi na ndani yake kutakua kumejaa harufu za rushwa
MAKOLO Tulia
 
Leo nimemsikiliza huyu mgombea wa yanga jinsi kampun itakavokuwa baad ya yanga kuingia mfumo wa kisasa,, kwa mfano pale simba Mo alijipangia bei nakumbuka alitoa mpaka muda simba waamue kama hawataki hizo pesa pesa bilion 20 anaweza kununua Bank.

Yule muhindi ni tapeli, hebu soma jinsi yanga watakavoipata thaman halisi ya Club yao na uwekezaji utakavo kuwa.

“Asilimia 49 zimegawanywa kwa watu wanne tofauti ambao watakuwa na uwiano wa asilimia 12 kutoka taasisi au watu tofauti tofauti ambao vyanzo vya mapato hawashabiani kimapato kutakuwa na kampuni maalumu itakayofanya kazi ya kujua thamani ya klabu na wataweka wazi hadharani na mwenye uwezo wa kununua hisa atapata nafasi hiyo bila upendeleo wowote” - Injinia Hersi kuhusu uwekezaji ndani ya Yanga

Sisi mbumbumbu rage hakukosea kutubatiza hili jina,, leo hii mo anaweza kuamua kisusa tu na uwekezaji wake hewa na tutakarudi matopeni
 
Makolo msimu huu walianza na Yanga kama kawaida yao uwa wanaongoza round ya kwanza tu ikifika round ya pili tunarudi kwenye nafasi yetu

2-Oooh!GSM ananunua match

3-Haiwezekani GSM awe mdhamini wa ligi sababu ya fair competition(juzi hapa wakaumbuka kwenye fa maana Yanga na coastal wote wanadhaminiwa na GSM lakini mpira waliocheza kila mtu aliona)

4-mayele wa kawaida sana tu(ingawa usiku na mchana walikua wanapambana hadi kichawi ili asiwe mfungaji bora,hili walifanikiwa

5-wakaja kwa abdul sopu

6- sasa hivi wapo kwa karia huku kwa mbali wakiwa na fukuto ndani ya uongozi wao kuna baadhi hawamtaki dada ceo
Cha ajabu aliyetunga jina "makolo" ambalo tunalishabikia kikasuku ndiye aliwahi sema "sisi wananchi hatuna akili isipokuwa baba yake na JK tu".
 
Back
Top Bottom