Ijue Sheria ya Ardhi: Taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi


Kupokonywa ardhi kunatokea pale ambapo utakuwa umekwenda kinyume cha masharti yaliyowekwa kwenye hati husika.Masharti haya huwa yamewekwa wazi sio swala la kusema to hujaendeleza.

Kuendeleza sio lazima kujenga hata kulima. Dhana ya kuendeleza inategemeana na matumizi yaliyokubaliwa.

Hata hivyo kwa ardhi za vijijini hati za kimila nyingi nilizoona hazina hayo masharti hayo. Hivyo si rahisi kupokonywa.
 
Mkuu nakuhitaji PM
 
Sehemu unapoweza kujua kama document ni halali au la ni ofisi za ardhi za mamlaka serikali ya mtaa (halmashauri) na pia kwa msajili wa nyaraka..sasa nendeni huko mkajiridhishe kama document ni halali au la..
2. Kama wakati mnanunua eneo lilikuwa limekwishapimwa (japo wananchi hawajaukubali upimaji huo) ilikuwa ni wajibu wenu kupita ofisi za serikali (halmashauri) ili kujua matumizi yaliyopangwa katika maeneo yenu hayo..

3. Ukipata majibu ya vitu hivyo (upimaji ulifanyika lini, nyie mlinunua lini na huyo mtu mwenye shule alinunua lini, pia kama muuzaji wenu alistahili kupewa fidia je alipewa fidia, yalete hapa tutashauriana
 

Kwa kuongeza, kama walivamia eneo na wakakaa miaka zaidi ya 12 bila bugudha..watakuwa wamethibitisha adverse possession hivyo wanastahili kumiliki eneo hilo
 
Kwa kuongeza, kama walivamia eneo na wakakaa miaka zaidi ya 12 bila bugudha..watakuwa wamethibitisha adverse possession hivyo wanastahili kumiliki eneo hilo
Mkuu adverse possession ina apply kwenye ardhi iliyo na hati na si vinginevyo...
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba kulingana na mgawanyiko wa ardhi makundi yote matatu ya ardhi yana taratibu tofauti ya usimamiaji

tukiongelea hili kundi la ardhi ya kijiji ambapo ndipo shauri lako lilipo ni kwamba hakuna barua ya toleo inayotolewa kwenye kundi hili (leter of offer) hadi ardhi hii ihaulishwe na kuwa ardhi ya kawaida hivyo kwenye ardhi ya kijiji kunatolewa hati miliki za kimila ambazo utaratibu wa kuzipata alishaeleza hapo juu mwanasheria msomi

Sasa kimsingi ili kijiji kiweze kupata hati miliki za kimila ni lazma kijiji hicho kiwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi

Mpango wa matumizi bora ya ardhi unaainisha maeneo tofauti tofauti kijiji kulingana na ardhi iliyopo na uhitaji pia

Matumizi haya hupangwa na halmashauri ya kijiji na kupata baraka ya mkutano mkuu wa kijiji ili kukweba double alocation

Katika mpango huu kunaainishwa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, zahanati,maeneo ya makanisa, misikiti, makaburi na nk. Pia hutenga eneo la makazi na maeneo ya mashamba yaani kimsingi kwenye kipindi cha mpango kila eneo hutambuliwa kwa hiyo hakuna hati yeyote itakayotoka kabla ya mpango katika ardhi ya kijiji ikawa halali hivyo hizo document ambazo hao wengine wanazo hujatuambia kuwa ni document za namna gani au ni ile mikataba ya kienyeji ya mauziano?

Na kama hao wanaosema ni eneo lao la shule ya private kama watakuwa wana hati ya kamishina (yaani hilo eneo lilisha badilishwa kutoka ardhi ya kijij kuwa ardhi ya kawaida) lazma aoneshe mchakato jinsi alivyopata ikiwa na maana kuwa lazma awe na mhtasari wa halmashauri ya kijiji na ule wa wa mkutano mkuu sasa kama mwenyekiti naye hajui kuna maswali ya kujiliza hapa?

Na nyie mlinunua hilo eneo kutoka kwa nani je mliwashirikisha viongozi wa kijiji kama ushahidi wakati mnanunua?
Ni eneo lenye ukubwa gani?
Ili tuweze kujua mamlaka na taratibu za upatikanaji wa eneo hili lazma pia tujue ukubwa wa eneo

Karbu kujibu hayo hapo juu then tutaendelea pia mwanasheria msomi anaweza kuongezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu adverse possession ina apply kwenye ardhi iliyo na hati na si vinginevyo...
Aisee, hebu naomba unielekeze kidogo kuhusu hii with authority ikibidi maana kuna watu wengi tu wamepoteza ardhi hata ambayo haijapimwa kwa base hiyo ya mtu kutumia zaidi ya miaka 12 with no disturbance..
Kama ni kwa maeneo yenye hati tu naomba nielekeze vizuri mzee
 
nafikiria kupitia mkutano mkuu wa kijiji wananchi wakiibua hoja , wahusika wanawezwa itwa na kuadhibiwa
 
nafikiria kupitia mkutano mkuu wa kijiji wananchi wakiibua hoja , wahusika wanawezwa itwa na kuadhibiwa
Naraza la ardhi la kijiji linasimamiwa na halmashauri ya kijiji, kama ambavyo baraza la kata linavyosimamiwa na kamati ya maendeleo ya kata (WDC).. Kama baraza la kijiji linatoa usuluhishi (maana lenyewe halina nguvu ya kutoa maamuzi- uwezo wake ni kusuluhisha tu mgogoro) basi halmashauri ya kijiji inaweza kulivunja lakini ushauri kama baraza hili linasumbua ni bora mtu mwenye malalamiko kwenda katika baraza la kata ambalo lina mamlaka ya kutoa uamuzi na uamuzi huo kuwa na nguvu ya kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…