Habari za majukumu wana jamii foroum. Kuna issue moja inanisumbua nataka kufahamu kisheria imekaaje. Kuna eneo tumenunua mimi na wenzangu na pia yumeshaanza kujenga, aliyetuuzia ni mmiliki halali wa eneo ila kuna issue kwamba lile eneo lilipimwa na kuna plani ya shule ya sekondari ya private. Ila wanazengo wanasema yale mapimo sio halali kwani hawakuwashirikisha wanazengo wa lile eneo na Mwenyekiti wa kijiji nae pia hajashirikishwa na wanasema mapimo ya lile eneo sio halali ukienda ardhi wanakuonyesha plani kua ni eneo la shule na kunajamaa anakuja anasema ni lakwake na documents zake zinaonesha ni za kitapeli. So kisheria imekaaje hii ama kwa mnaofahamu sheria mnaweza kutusaidia apa.
Kwa uelewa wangu ni kwamba kulingana na mgawanyiko wa ardhi makundi yote matatu ya ardhi yana taratibu tofauti ya usimamiaji
tukiongelea hili kundi la ardhi ya kijiji ambapo ndipo shauri lako lilipo ni kwamba hakuna barua ya toleo inayotolewa kwenye kundi hili (leter of offer) hadi ardhi hii ihaulishwe na kuwa ardhi ya kawaida hivyo kwenye ardhi ya kijiji kunatolewa hati miliki za kimila ambazo utaratibu wa kuzipata alishaeleza hapo juu mwanasheria msomi
Sasa kimsingi ili kijiji kiweze kupata hati miliki za kimila ni lazma kijiji hicho kiwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi
Mpango wa matumizi bora ya ardhi unaainisha maeneo tofauti tofauti kijiji kulingana na ardhi iliyopo na uhitaji pia
Matumizi haya hupangwa na halmashauri ya kijiji na kupata baraka ya mkutano mkuu wa kijiji ili kukweba double alocation
Katika mpango huu kunaainishwa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, zahanati,maeneo ya makanisa, misikiti, makaburi na nk. Pia hutenga eneo la makazi na maeneo ya mashamba yaani kimsingi kwenye kipindi cha mpango kila eneo hutambuliwa kwa hiyo hakuna hati yeyote itakayotoka kabla ya mpango katika ardhi ya kijiji ikawa halali hivyo hizo document ambazo hao wengine wanazo hujatuambia kuwa ni document za namna gani au ni ile mikataba ya kienyeji ya mauziano?
Na kama hao wanaosema ni eneo lao la shule ya private kama watakuwa wana hati ya kamishina (yaani hilo eneo lilisha badilishwa kutoka ardhi ya kijij kuwa ardhi ya kawaida) lazma aoneshe mchakato jinsi alivyopata ikiwa na maana kuwa lazma awe na mhtasari wa halmashauri ya kijiji na ule wa wa mkutano mkuu sasa kama mwenyekiti naye hajui kuna maswali ya kujiliza hapa?
Na nyie mlinunua hilo eneo kutoka kwa nani je mliwashirikisha viongozi wa kijiji kama ushahidi wakati mnanunua?
Ni eneo lenye ukubwa gani?
Ili tuweze kujua mamlaka na taratibu za upatikanaji wa eneo hili lazma pia tujue ukubwa wa eneo
Karbu kujibu hayo hapo juu then tutaendelea pia mwanasheria msomi anaweza kuongezea
Sent using
Jamii Forums mobile app