Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Ni jambo lisilopingika kuwa Marekani ni taifa lililoendelea zaidi kiteknolojia, kisayansi, kiuchumi, na hata kijamii. Mataifa mengi yanaiangalia Marekani kama mfano wa mafanikio na ubunifu wa hali ya juu. Lakini swali ni hili: Je, ni nini kinachoifanya Marekani kupiga hatua kubwa kiasi hiki katika nyanja mbalimbali za maarifa?
Tofauti na mataifa mengine yaliyojengwa juu ya msingi wa siasa au falsafa za kibinadamu, Marekani imejengwa juu ya msingi wa kumcha Mungu. Wahamiaji wa kwanza waliowasili kutoka Ulaya walienda katika taifa hilo kutafuta uhuru wa kumwabudu Mungu bila mateso. Hivyo, misingi ya taifa hilo iliwekwa kwa kuzingatia Maandiko Matakatifu(Biblia). Hadi leo, fedha ya taifa hilo inasema: "In God We Trust."
Shule za awali kama vile Harvard, Yale, na Princeton zilianzishwa kwa lengo la kuandaa watumishi wa Mungu waadilifu na wenye maarifa. Mitaala yao ilikuwa imejengwa juu ya Biblia.
Katika mazingira hayo ya kumcha Mungu, maarifa ya kweli yalizaliwa. Mungu ametimiza ahadi yake – kwamba wale wanaomcha, anawapa hekima na uwezo wa kuvumbua mambo ya ajabu. Kwa mfano: Marekani imekuwa kinara katika uvumbuzi wa teknolojia za hali ya juu kama kompyuta, intaneti, na sasa Artificial Intelligence (AI).
Tovuti na programu kama ChatGPT, zinazotumia akili unde kutoa maarifa, ni zao la fikra zilizotokana na uhuru wa kiroho na kimaadili ulioasisiwa na kumcha Mungu.
Vituo vya utafiti kama NASA, MIT, na Silicon Valley vinathibitisha kiwango cha maarifa ambacho hakikutokea kwa bahati bali kwa msingi wa kiroho.
Biblia haikuandikwa ili isomwe tu kama kitabu cha dini; ni mwongozo wa maisha na maendeleo ya kiakili. Mtu akiyafanyia kazi yaliyoandikwa ndani yake, anapewa hekima na ubunifu. Yesu alisema:
“Mtu ye yote anayesikia maneno yangu na kuyatenda, nitamfananishia na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” – Mathayo 7:24
Hivi majuzi, Rais Trump alitangaza kwamba lazima wairudishe dini katika taifa hilo. Kauli hiyo imekuja baada ya yeye kugundua kuwa watu katika taifa hilo wameanza kusahau kwamba baraka na mafanikio waliyo nayo yametokana na kumcha Mungu.
www.jamiiforums.com
"Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa; bali wapumbavu hudharau hekima na adabu." – Mithali 1:7

Rais Trump asema: "Lazima tuirudishe Dini"
Kwanini Rais Trump amesema lazima wairudishe dini katika nchi yao? Jibu la swali hilo utalipata katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa maombi ya kitaifa(National Prayer Breakfast) yanayofanyika kila mwaka katika nchi ya Marekani. Kwa kifupi alisema hivi: "Kuanzia siku za mwanzo za Jamhuri yetu...